Posts

Showing posts from August 22, 2016

Mghwira wa ACT-Wazalendo Azindua ‘Tanzania Role Model’

Image
       Mwenyekiti wa Chama cha  ACT-Wazarendo, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo,  Anna Mghwira, akizindua mashindano hayo. …Akifafanua jambo mbele ya warembo wanaoshiriki shindano. Mratibu wa mashindano hayo, Samweli Charles (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha  Mghwira. Viongozi wakifuatilia nyendo za warembo waliokuwa wakipita mbele yao. Baadhi ya washiriki wa Tanzania Role Model wakifanya vitu vyao mbele ya mgeni rasmi. Baadhi ya ‘manjonjo’ yaliyoonyeshwa na warembohao. Washiriki wakitambulishwa mbele ya mgeni rasmi. Mshereheshaji ‘MC’ wa hafla hiyo, Sufian Juma (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo baada ya shindano kuzinduliwa. MWENYEKITI wa  ACT-Wazalendo na aliyekuwa mgombea urais kupitia chama hicho, Mama Anna Mghwira,  jana alizindua shindano lijulikanalo kama ‘Tanzania Role Model’ lililoandaliwa na kampuni ya Mass Television  Company (MTV) chini ya mkurugenzi wake, Samweli Charles. Uzinduzi huo ulifanyika katika

PICHA LOWASSA BAADA YA KUTUA MBEYA

Image
 

Beki Simba aanguka bafuni, apasuka kichwani

Image
Mchezaji wa Coastal Union,Hamad Juma akiwa ameanguka chini huku mchezaji wa Simba, Hassan Kessy (kulia) akichanja mbuga kuelekea golini kwao mechi ya Ligi Kuu msimu uliopita. Wilbert Molandi, Dar es Salaam BEKI mpya wa kulia wa Simba, Hamad Juma, jana asubuhi alianguka bafuni akiwa nyumbani kwake na kusababisha achanike kisogoni kwake. Juma alijiunga na Simba msimu huu wa Ligi Kuu Bara akisaini mkataba wa mwaka mmoja akitokea Coastal Union baada ya mkataba wake kumalizika. Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumatatu limezipata jana jioni na kuthibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, tukio hilo lilitokea nyumbani kwake kabla ya kukimbizwa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam alipokwenda kulazwa. Manara alisema, beki huyo mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo, madaktari walishauri alazwe kutokana na damu nyingi zilizokuwa zinamtoka. “Hamad ameanguka na amepoteza damu nyingi sana, alipata matatizo hayo akiwa ny

Askari wa Upelelezi Mwanza Auawa Club Akidai Laptop

Image
  Tarehe 21.08.2016 majira ya 10:00 usiku katika eneo la Club ya Villa Park Resort Kata ya Kirumba Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza, askari namba g.5092 PC John Nyange wa Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Mkoa wa Mwanza (RCP), aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali eneo la shingoni na mtu aliyekuwa anaugomvi nae. Inadaiwa kuwa marehemu alikua na ugomvi wa muda mrefu na mtu aliyejulikana kwa jina Magina Hussein miaka [27] fundi computer Msukuma na mkazi wa Mtaa wa Kigoto, ambapo marehemu alikuwa akimdai Bwana Magina Hussein computer aina ya laptop.  Ndipo usiku wa leo majira tajwa hapo juu walikutana eneo la club ya Villa Park huku mtuhumiwa wa mauaji hayo ikisemekana kuwa alikuwa na wenzake watano ndipo walimvamia na kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni na kufariki dunia njiani wakati akipelekwa hospitali. Marehemu kwa sasa alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Stefano Moshi Memorial University College cha Mjini Moshi, alikuwa anas