Posts

Showing posts from October 26, 2013

"Sijawahi vua nguo na kufanya mapenzi na mwanaume yeyote tangu niachane na Diamond"...Jokate Mwegelo

Image
Mtangazaji wa Channel O mwenye mvuto wa aina yake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amefunguka kuwa tangu amwagane na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ hajawahi kungonoka na mwanaume mwingine. Penzi la Jokate na Diamond lilichanua kwa takriban miezi miwili mwaka jana wakati Kidoti alipomwagana na aliyekuwa mpenzi wake, mcheza kikapu wa Ligi ya NBA ya Marekani, Hasheem Thabit. Alipoulizwa anamudu vipi hisia za matamanio ya kufanya mapenzi, Jokate alisisitiza kuwa kazi pekee ndiyo silaha kubwa ya kumuepusha na vishawishi ingawa anatambua upo umuhimu wa kuwa na mpenzi. “Akitokea mkweli, nipo tayari ingawa hadi sasa hata sijajua nani anaweza kuwa kama alivyokuwa Hasheem, nilimpenda sana,” alisema.

Rais Kikwete awatoa hofu watanzania kuhusu sakata la Mafuta....Amesema kwamba hiyo siyo mali ya wazungu, ni yetu watanzania

Image
RAIS Jakaya Kikwete amewatoa hofu Watanzania kwamba kuwaruhusu wawekezaji wa nje kufanya utafiti wa mafuta na gesi nchini, kuna hasara kubwa itakayolikumba taifa. Pia amewataka kupuuzia dhana kwamba kuwaruhusu wawekezaji hao kunaweza kusababisha wahamishe rasilimali za gesi na mafuta zitakazogunduliwa kunufaisha mataaifa ya nje. Rais Kikwete alitoa kauli hiyo, Dar es Salaam jana kabla ya kuzindua awamu ya nne ya ugawaji vitalu baharini katika kina kirefu Kaskazini mwa Ziwa Tanganyika. “Kumekuwa na maneno mengi kuwa mfumo huu wa sasa wakutoa leseni za utafutaji wa mafuta na gesi kwa wawekezaji wa nje, kuwa hakuwanufaishi Watanzania. Alisema sheria, mfumo na mikataba iliyowekwa haiwezi kuruhusu mianya hiyo ya kupata hasara na kwamba asilimia 75 ya faida itakayopatikana baada ya wawekezaji kurudisha gharama zao za utafiti, itakuwa ni ya taifa na asilimia 25 ndiyo itakayokuwa stahili yao. Kwa mujibu wa Rais Kikwete wapo baadhi ya watu wanaoeneza maneno potofu, kw...

Wema Sepetu atumia milioni 13 kuibadili ngozi yake akiwa China baada ya kuharibiwa sana na Mkorogo

Image
IMEVUJA! Kumbe ile safari ya nchini China ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ‘Madam’ lengo lilikuwa kubadili ngozi ya mwili wake katika mwonekano mpya ambayo ilishaharibika kwa mkorogo. Wema Sepetu ‘Madam’. Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, staa huyo aliingia nchini humo na mdogo wake aitwaye Bite ambaye kazi yake kubwa ilikuwa kufanya mawasiliano na nyumbani, Tanzania endapo lingetokea baya wakati wa zoezi hilo. KWA NINI ALIAMUA KUDILI NA NGOZI? Mpashaji wetu aliliambia Amani kwamba, Wema alichoshwa na ‘vijembe’ vya watu mbalimbali wakiwemo wabaya wake kuwa ngozi yake imebabuka kwa kutumia mkorogo kupitiliza. Miguu ya Wema Sepetu ‘Madam’ kabla ya kubadili ngozi. “Kuna wakati Wema alikuwa akikosa amani kutokana na maneno ya watu, wengine waliokuwa wakimrushia vijembe ni masupastaa wenzake, ndiyo maana akaamua kwenda China kubadili ngozi yake iwe na mwonekano mpya,” kilisema chanzo. Habari zaidi zilidai kwamba, supastaa huyo hakupenda kabisa Wabong...

CHADEMA wasalitiana na kufukuzana....Mbowe apigwa ngumi baada ya kudaiwa kuiba milioni 80 za chama , polisi waingilia kati huko Arusha

Image
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya Kaskazini, kimemsimamisha Uongozi Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba kwa madai ya kukihujumu chama hicho. Taarifa ambazo tumezipata kutoka ndani ya kikao cha Baraza la uongozi kanda ya Kaskazini, kilichofanyika katika Hotel ya Corridor Spring leo usiku, zimedai uamuzi wa kusimamishwa Mwigamba umefikiwa na Kikao hicho baada ya kuwasilishwa kwa vielelezo kadhaa vya Mwigamba na yeye kukiri kuwa ni vyake huku vingine vikimuonyesha kuwa ndiye mmiliki wa Akaunti ya Jina la ‘Maskini Mkulima’ ambalo limekuwa likitumika kukichafua chama kwenye mitandao ya kijamii. Hakuna kiongozi ambaye amekuwa tayari kuzungumzia suala hili kiofisi, lakini taarifa za uhakika ambazo tumezipata kutokana na maamuzi ya kikao hicho zimebainisha kuwapo kwa maamuzi hayo pasipo shaka. “Kikao hicho kimemsimamisha Uongozi kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili, hivyo kuanzia sasa mwigamba siyo kiongoz...

DIAMOND PLATINUM ALIVYOPOKELEWA AIRPORT AKITOKEA CHINA

Image
Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' (katikati) akilakiwa na m ama yake mzazi, Sanura Kassim 'Sandra' alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini China leo. Mama Diamond akisalimiana na rafiki wa Diamond aliyetua naye leo.… Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' (katikati) akilakiwa na m ama yake mzazi, Sanura Kassim 'Sandra' alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini China leo. Mama Diamond akisalimiana na rafiki wa Diamond aliyetua naye leo. Diamond akipozi na mama yake mzazi alipowasili uwanjani hapo majira ya saa nane mchana leo. Bi. Sandra akimlaki Rommy Jones uwanjani hapo. MSANII mahiri wa Muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' leo ametua nchini akiambatana na ndugu yake pamoja na rafiki yake wakitokea nchini China. Msanii huyo pamoja na alioambatana nao, wamewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira y...