Posts

Showing posts from April 20, 2016

Watuhumiwa wa ujambazi, wala kichapo hevi Kariakoo

Image
WATU wawili wanaodaiwa kuwa majambazi wamenaswa leo Kariakoo jijini Dar es Salaam na kupewa kichapo ‘hevi’ kutoka kwa wananchi wenye hasira kali waliokuwa eneo la tukio. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, majambazi hao wawili akiwemo mmoja ambaye ni raia wa Kihindi wamekamatwa Mtaa wa Swahili na Mchikichi, Kariakoo na wanadai raia huyo wa Kihindi anajulikana kwa jina la Samir.

MSANII BONGO MOVIE AFARIKI AKIJIFUNGUA

Image
Ni simanzi! Nyota ya msanii Leila Gabriel ‘Lissa’ ambayo ndiyo kwanza ilikuwa imeanza kuchomoza kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, ilizimika ghafla mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya msanii huyo kupoteza maisha muda mfupi baada ya kujifungua kwenye Hospitali ya St. Benard, Kariakoo jijini Dar es Salaam. Filamu alizowahi kucheza? Aishiwa nguvu wakati wa kujifungua. Aabainika kutokuwa na damu ya kutosha. Madaktari washindwa kumfanyia upasuaji Bahati nzuri ajifungua salama. Apatwa balaa lingine baada ya kujifungua, afariki dunia. Mama wa Marehemu afunguka mazito kuhusu kifo cha mwanaye. Simulizi ya kifo chake inasikitisha sana! “Inauma sana, mwanangu amefariki kwa maumivu maana shida ilikuwa ni ambulance, kama ingepatikana kwa wakati naamini angepona lakini ndiyo hivyo tena, kazi ya Mungu haina makosa,” alisema mama huyo kwa uchungu huku akitokwa machozi. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina! -Chanzo: GPL