Image copyrightGETTYImage captionKiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda Osama bin LadenMwanaye aliyekuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda Osama bin Laden, ameapa kulipiza kisasi kwa mauaji ya babake.Katika ujumbe wa sauti uliochapishwa katika mitandao Hamza bin Laden ameapa kulipiza kisasi kwa Marekani kwa kumuua babake 2011 huko Pakistan.Ujumbe huo wa dakika 21 wenye kichwa "We Are All Osama,", Hamza ambaye inaaminika kuwa alikuwa na babake makomando wa Marekani walipowavamia na kumtwaa ameapa kuendeleza kazi aliyoianza babake. Image copyrightFLAGG MILLERImage captionUjumbe huo ni wa dakika 21 wenye kichwa "We Are All Osama," ''Tutaendelea kuwasaka na kuwapiga popote pale mtakapokuwa mumejificha ati nyuma ya pazia za usalama kwa maovu munayoyaendeleza ,Palestina, Afghanistan, Syria, Iraq, Yemen, Somalia na kote kwenye ardhi ya waislamu mnayokalia '' shirika la habari la Reuters linamnukuu. ''na kwa wale wanaodhan...