Prince William, Kukutana na Rais Magufuli
Mwanamfalme William wa Uingereza Mwanamfalme (Prince) William wa Uingereza anapangiwa kukutana na Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli wiki ijayo wakati wa ziara yake ya siku saba Afrika. Anatarajiwa kuzuru pia Kenya na Namibia katika ziara hiyo ambayo si ya kikazi. Ziara hiyo itafanyika kuanzia 24 Septemba hadi 30 Septemba. Lengo kuu litakuwa kufuatilia juhudi za kukabiliana na ujangili na uhifadhi wa wanyama. Atafanya ziara hiyo katika wadhifa wake kama rais wa mashirika yanayotetea uhifadhi wa wanyama ya United for Wildlife na Tusk Trust. Amekuwa pia mlezi wa shirika la Royal African Society linalolenga kukuza uhusiano kati ya Afrika na Uingereza na hushiriki sana juhudi za kukabiliana na ujangili. Akiwa ziarani Tanzania, atafanya mashauriano na Rais Magufuli kuhusu juhudi zinazopigwa na taifa hilo katika kukabiliana na ujangili kwa mujibu wa shirika la habari la Press Association. Kadhalika, atazuru bandari ya Dar es Salaam kujifahamisha zaidi kuhusu ju...