Posts

Showing posts from September 9, 2015

MAGUFULI AHIDI KUFUFUA VIWANDA MKOANI TANGA,KUONGEZA AJIRA KWA VIJANA

Image
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akifafanua jambo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika katika viwanja vya Tangamano jioni ya leo mjini Tanga.      Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tanga kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya angamano,jioni ya leo ambapo aliahidi kuboresha Bandari ya Tanga, kujenga Viwanda vya matunda na samaki ili kuweza kupunguza tatizo kubwa la ajira kwa vijana.  Naibu Waziri wa Sheria na Katiba,ambaye pia ni mgombea Ubunge viti maalum upande wa akina Mama mkoa wa Tanga (UWT),Mh Ummy Mwalimu akimuombea Kura za kutosha mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ili aweze kuibuka mshindi na kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano.  Wakazi wa mji wa Tanga waliofika kwenye mkutano huo wakishangilia jambo....