Posts

Showing posts from March 13, 2016

JPM awathibitisha watendaji wakuu TRA, TAKUKURU

Image
Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Alphayo Kidata. Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola.

Mambo 5 yanayoleta uadui kwa wapenzi!

Image
Ni matumaini yangu kuwa msomaji wangu umzima wa afya njema na unaendelea na majukumu yako ya kujitafutia mkate wa kila siku. Namshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema na kunipa tena nafasi ya kubadilishana mawazo kuhusu mambo yanayohusu uhusiano wa kimapenzi. Rafiki, bila shaka ipo wazi kwamba kila mmoja anapenda kuwa na mpenzi ambaye mbali na kumpenda kwa moyo wake wote, atapenda kumfanya awe kama ndugu, rafiki au zaidi ya hapo. Atakayekuwa tulizo la moyo, kivuli kwenye jua kali, maji jangwani na tiba kwenye maradhi. Hakuna anayeweza kuukabidhi moyo wake kwa mtu ambaye anajua fika kwamba atamtesa, atamnyanyasa, kumsababishia maumivu ya moyo, kuwa kero kwenye maisha yake na ‘kum-treat’ kama adui yake. Mapenzi ni sanaa kama zilivyo sanaa nyingine. Kwa mfano, ili kumudu kupiga gitaa au kinanda na kupata muziki mzuri, ni lazima ujifunze. Kwenye mapenzi ni hivyohivyo, ili kuishi vizuri na mpenzi wako ni lazima ujifunze. Usichoke kujifunza kila kukicha ili kuwa na u

Mjue Katibu Mkuu mpya wa Chadema!

Image
Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vicent Mashinji, akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho, usiku wa kuamkia leo mara baada ya kuchaguliwa, kwenye Mkutano Mkuu uliokuwa ukifanyika Jijini Mwanza. Dkt. Mashinji anaziba nafasi iliyoachwa wazi na Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Willbload Slaa. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, Makamu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Mh. Said Issa Mohamed pamoja na Mjumbe wa Mkutano Mkuu, Mh. Edward Lowassa wakifarilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu mpya wa Chama hicho, Dkt. Vicent Mashinji (hayupo pichani). Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA wakishangilia baada ya kupatikana bila kwa Katibu Mkuu mpya, Dkt. Vicent Mashinji. WASIFU WA DK. VECENT MASHINJI Dk. Mashinji aliyezaliwa katika Wilaya ya Sengerema, alianza elimu ya msingi katika Shule ya Iligamba Januari 1981 hadi Oktoba 1987 na kisha kue

RAIS DKT MAGUFULI ATEUA WAKUU WA MIKOA LEO MACHI 13 2016

Image