Yanayojiri Bungeni Dodoma Muda Huu..Wabunge wa Ukawa Walianzisha na Kutolewa Nje ya Bunge na Spika
Wabunge wanaounga umoja wa Katiba Ya Wananchi, UKAWA wametolewa nje ya ukumbi wa bunge muda huu baada ya kugoma kutambua ujio wa Dr Shein bungeni na kuanza kuzomea huku wakisema Maalim Seif....Maalim Seif Spika wa bunge,Job Ndugai aliwataka wabunge hao waache kuzomea na badala yake wakae chini lakini wakakaida, hali iliyomfanya awaamuru watoke nje kwa hiari yao kabla nguvu ya dola haijatumika kuwatoa.