MBINU TANO(5) ZA KUISHI NA WAFANYAKAZI WENZAKO AMBAO NI WAKOROFI
Huyu mtu siku zote ni mkorofi na mwenye kukusababishia hasira. Hata ukiongea naye kwa utaratibu lazima alete maudhi, anakusababishia kazi uione mbaya kila unapomwona. Unahitaji mbinu za kuishi naye. 1. Utambue ya kuwa sio wewe peke yako Unaweza kusema kwamba huyu mtu ana visa na wewe tu, mara nyingi watu wa namna hii ni kwa jinsi tu ya tabia zao na namna walivyokuzwa. Jitahidi kwa kadri uwezavyo kutotilia maanani wanachokiongea ili usiingie kwenye ugomvi bila sababu. Wengine huwa hawajui kwamba wanakera wenzao kwa namna ambavyo wanafanya au kuongea, wao hupenda namna wanavyojisikia kila wanachofanya au kusema ndio furaha yao. 2. Jiepushe nao Punguza au ujiepushe kukutana nao mara kwa mara ili kupunguza kero. Hata kama watafika ofisini kwako, onyesha uko kikazi zaidi kuliko utani na mambo yasiyo ya msingi. Kama kuna jambo wanauliza waombe kukutumia barua pepe au kuacha ujumbe kwenye dawati lako la kazi. Unapopunguza kukutana nao mara kwa mara unaboresha...