Posts

Showing posts from May 18, 2017

Wamarekani Wafanikisha Upasuaji Mkubwa wa Wanafunzi Lucky Vincent

Image
May 18, 2017 Mtoto Wilson      Watoto watatu wa shule ya msingi ya Lucky Vicent walionusurika katika ajali ya basi, wamefanyiwa upasuaji na sasa wapo wodini wakiendelea na mazoeazi, ila Doreen, jana alipewa MAPUMZIKO maalumu akiwa anaandaliwa tayari kwa UPASUAJI wa uti wa mgongo ‘spine’  unaofanyika leo.   Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliyeshiriki katika kuwasafirisha watoto hao, ameandika katika ukurasa wake wa facebook akisema  watoto hao kwa sasa wamewekwa kwenye vyumba vya peke yao.   Mtoto Doreen Upasuaji huo umefanyika katika Hospitali ya Mercy, Sioux City, Marekani.   Amefafanua upasuaji waliofanyiwa na kusema mtoto Saidia alifanyiwa upasuaji wa mfupa wa kulia wa nyonga, mkono wa kulia na kuwekewa ngao kwenye shingo atakayotakiwa kukaa nayo kwa wiki sita.   “Kwa upande wa mtoto Wilson, yeye amefanyiwa upasuaji wa nyonga ya kulia, kiwiko cha kulia kilichokuwa kimevunjika mara tatu na kiwiko cha kushoto,” amesema

IMEFICHUKA! Mume wa Zari anasumbuliwa na ugonjwa huu

Image
KAMPALA: Habari mbaya zilizolifikia mtandao huu zinadai kuwa, aliyekuwa mume wa staa wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tycoon Ivan Ssemwanga yu hoi bin taaban akisumbuliwa na maradhi ya shambulio la moyo (Coronary Artery Disease). Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya jijini Kampala, Uganda ambako ndiko maskani yake yalipo maeneo ya Munyonyo, pamoja na kwamba ana makazi Pretoria, Afrika Kusini, Ivan alionekana hadharani kwa mara ya mwisho akiwa amedhoofu na rangi ya ngozi kupauka, tofauti na alivyozoeleka kuwa na rangi nyeusi yenye mng’aro alipotinga kwenye Pati ya Blankets and Wine iliyofanyika Kampala hivi karibuni. Chanzo kilichomshuhudia Ivan kilitonya: “Sisi wenyewe tulipomuona kwenye Blankets and Wine Party akiwa na rafiki yake, Ed Cheune, kwanza hatukumtambua, lakini tulipomuangalia vizuri ndipo tukamjua ni yeye. Ukweli tulishtuka sana na tulijua anaumwa. “Tofauti na alivyozoeleka kuwa ni mtu wa bata, lakini siku hiyo alikuwa mpole sana. Al

Vladimir Putin nipo tayari kutoa siri za mkutano wa Trump na maafisa wa Urusi

Image
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameingilia sakata inayomkabili Rais wa Marekani Donald Trump kutokana na uhusiano wake na Urusi. Rais Putin amepinga madai ya uvujaji siri za Marekani kwa Urusi na kueleza kuwa yuko tayari kutoa kumbukumbu za mkutano wa viongozi hao kwa bunge na Seneti za Marekani ikihitajika. Putin ametania hali hiyo na kusema kuwa mkutano haukufanyika unavyodhaniwa. Majarida mbalimbali ya Marekani yamefichua kuwa Rais Trump aliwapa viongozi wa Urusi taarifa kuhusu Islamic State ambazo zina uwezo wa kuhatarisha watoaji wa taarifa hizo. Haya yanajiri huku taarifa zikienea kuwa Bw Trump alijaribu kushawishi uchunguzi unaoendelea kuhusu ushirikiano wa wawakilishi wake na Urusi. Bwana Trump alikutana na waziri wa kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov na Balozi wa Urusi nchini Marekani Sergei Kislyak katika ikulu ya White house Jumatano, wiki iliyopita. Mkutano huo unajiri wakati uchunguzi

MARADHI YA GESI TUMBONI (COLIC): Msokoto wa tumbo

Image
MARADHI YA GESI TUMBONI (COLIC): Msokoto wa tumbo Ikiwa mtu atakula kwa wingi vyakula vinavyoleta gesi halafu vyakula hivyo visisagike vizuri tumboni, hukusanya gesi tumboni na kufanya mingurumo humo na kumsababishia maumivu, humkosesha mtu utulivu na kumfanya kutoka jasho na machovu bila ya kufanya kazi. Mtu hujisikia mara kwa mara aende haja kubwa na akienda hapati choo. Pia humsababishia mtu kuumwa kwa mgongo au kiuno. Ikiwa gesi hii itakosa kutoka kwa njia ya haja kubwa, basi yaweza kupanda juu na kufanya presha sehemu au karibu ya moyo na kusababisha maumivu ya moyo. TIBA:  Chukua asali robo lita , unga wa arki susi vijiko vitatu vikubwa na unga wa habat soda vijiko viwili vikubwa. Koroga zote pamoja kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni.

Mastaa wa Bongo waonyesha hisia zao walivyoguswa na msiba wa Dogo Mfaume

Image
 Leo May 17, 2017 tasnia ya muziki Tanzania imejawa na huzuni baada ya kutangazwa taarifa za kifo cha Mwimbaji Dogo Mfaume aliyefariki akiwa Muhimbili Hospital ambako alitarajia kufanyiwa upasuaji wa kichwa. Kutokana na kusambaa kwa taarifa hizo za majonzi ambazo zimegusa hisia za watu mbalimbali wakiwemo mastaa wa muziki, watu hao wameelezea masikitiko yao kupitia social media wakiongozwa na mastaa Diamond Platnumz, Nay wa Mitego na wengine…

PRINCE WILLIAM AMTEMBELEA MTOTO MWENYE KANSA

Image
Prince William kutokea familia Malkia Elizabet II, Siku ya jana alifanya ziara ya kutembelea hospitali ya Royal Marsden iliyopo Sutton- Uingereza. Katika ziara hiyo Prince William aliweza kumtembelea mtoto Daisy Wood mwenye miaka 6, anaeugua ugonjwa wa kansa, kisha kuzungumza nae pamoja na wazazi wake. Hii ni mara ya 10 kwa mwana wa mfalme Prince William kutembelea hospital hiyo tangu kuchaguliwa kuwa anasimamia Royal Marsden NHS Foundation Trust.

Wanawake 11 wateuliwa kuwa mawaziri Ufaransa kati ya mawaziri wote 22

Image
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameteua baraza la mawaziri lenye usawa wa kijinsia kuambatana na ahadi ya mapema ambapo 11 kati ya mawaziri 22 ni wanawake. Sylvie Goulard ndiye waziri mpya wa ulinzi huku bingwa wa olimpiki wa mchezo wa kupigana na panga Laura Flesseng, akiteuliwa kuwa waziri wa michezo. Bruno Le Maire ameteuliwa kuwa waziri wa uchumi, Gérard Collomb waziri wa masuala ya ndani, huku naye François Bayrou ndiye waziri wa sheria. Rais huyo mpya wa Ufaransa ana matumaini kuwa kikosi hicho kitazoa kura nyingi kwenye uchaguzi wa ubunge mwezi ujao. Alitimiza ahadi yake ya kuwepo usawa kwenye baraza la mawaziri, lakini kati ya nafasi muhimu tano , ni moja ya tu ya ulinzi ilimuendea mwanamke. Mawaziri wengine ni pamoja na Jean-Yves Le Driana, ambaye ameteuiliwa kuwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni. Wengine ni pamoja na: Agnès Buzyn - Afya Murielle Pénicaud - Kazi Mounir Mahjoubi - Masuala ya dijitali Françoise Nyssen - Utamaduni Jean-Michel

DAWA ZA KULEVYA ZAMUUMIZA MSANII MADEE ALI

Image
Rais wa Manzese, Madee Ali amefunguka kwa uchungu kuwataka vijana wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya kuacha mara moja na kutafuta njia za kupunguza mawazo ili kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na janga hilo. Madee amefunguka hayo akiwa kwenye Planet Bongo ya East Africa radio na kusema kuwa janga la dawa za kulevya limezidi kukithiri hali ambayo kwa vijana wa sasa kutimiza miaka 40 limekuwa  jambo la nadra sana. Aidha Madee amelazimika kuwaasa vijana kutokana kifo cha Msanii mwenzake Dogo Mfaume kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na za dawa ya kulevya. "Madawa yanatumaliza sana jamani. Nawaomba wadogo zangu, ndugu zangu tubadilishe njia za kupunguza mawazo.  Najua stress ni nyingi na ndio zinatukimbiza huko, tuachane na madawa maana hayana msaada zaidi  kutumaliza kwa wingi. Ukiangalia matokeo ya dawa za kulevya kwa umri huu ukifikisha miaka zaidi ya 40 inakubidi umshukuru Mungu sana'' - Madee alliongeza.