Posts

Showing posts from June 21, 2016

Nafasi ya Kazi Stamigold

Image
STAMIGOLD COMPANY LIMITED EMPLOYMENT OPPORTUNITY ‘STAMIGOLD Company Limited -Biharamulo Mine is a subsidiary company of the State Mining Corporation (STAMICO) operating a gold mine. The Mine is located in the Biharamulo Forest Reserve South West of Mwanza in Kagera Region. In order to run the mine effectively and efficiently, the Company invites applications from qualified candidates to fill the existing vacancy as detailed below THE ROLE: Work Station: Biharamulo Mine Site Work Roster: 6/3 (42 days on, 21 days off) Contract Duration: Not exceeding two years, subject to renewal SENIOR SUPPLIES OFFICER (01) The Senior Supplies Officer-will be reporting to the Procurement Superintendent and should ensure effective supplying of goods and services in response to internal needs by providing support, ,guidance and professional advice within the requirements of the Procurement and Supplies Professionals and Technician Board (PSPTB) and Public Procurement Regulatory A...

Mahakama Yagomea Pingamizi la Mbowe kwa Jeshi la Polisi

Image
KESI ya madai iliofunguliwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuiomba mahakama kupiga marufuku zuio la Polisi, leo limetupiliwa mbali. Mbowe alifungua kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2016, baada ya hivi karibuni Jeshi la Polisi  kupiga marufuku mikutano ya hadhara kwa madai kwamba, hali ya usalama nchini si salama. Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, Kilimanjaro katika shauri hilo, aliwashtaki Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa madai wanahusika kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Mbowe ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, walitangaza kufanya oparesheni iliopewa jina ‘Okoa Demokrasia nchini’ iliyokuwa na lengo la kuishtaki serikali kwa wananchi kwa kile alichodai, kuendesha nchi bila kufuata katiba ya nchi. Hata hivyo, baada ya kupigwa marufuku kwa maandamano, Mbowe alifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania K...

Mdosi mbaroni kwa ujambazi Moshi

Image
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Wilbroard Mtafungwa. Issa Mnally na Richard Bukos, UWAZI DAR ES SALAAM: Watu watatu akiwemo mmoja mwenye asili ya Kiasia ‘Mdosi,’ wametiwa mbaroni na polisi Moshi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za ujambazi, Uwazi limeezwa. Akizungumza na waandishi wetu kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Wilbroard Mtafungwa alisema kuwa watuhumiwa hao wanashikiliwa na jeshi hilo baada ya kukamatwa kutokana na ushirikiano wa polisi na raia wema. Akielezea jinsi polisi walivyowanasa watuhumiwa hao, Kamanda Mtafungwa alisema kuwa walimkamata kwanza mmoja Fredil Guston maarufu kwa jina la Chedieli ambaye ni mkazi wa Majengo, Moshi. Aidha, alisema Chedieli aliwataja wenzake ambao ni Frank Nkya maarufu kwa jina la Chabufa na Frank Mbesanyo Domani ‘Ausho’ mkazi wa Pasua na walipopekuliwa walikutwa na vitu kadhaa vya wizi. “Sasa hawa wakamtaja bosi wao ambaye ni kiongozi wao mkuu wa...

Majibu ya Hoja za Wabunge Yaliyotolewa Jana na Waziri wa Fedha

Image
JUNI 20, 2016 DODOMA UTANGULIZI Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kukushukuru wewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuendesha vizuri majadiliano kuhusu Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa 2015 na Mpango wa Maendeleo wa 2016/17 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2016/17, niliyowasilisha tarehe 8 Juni, 2016. Mheshimiwa Spika, Kipekee, ninampongeza sana Mhe. Naibu Spika kwa umahiri na weledi wa hali ya juu alioonesha katika kusimamia Kanuni za Bunge wakati wote wa kikao hiki cha Bunge la bajeti. Hakika viwango vyake ni vya kimataifa. Japokuwa Mhe. Joseph Kakunda, mwanafunzi wangu Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam alichomekea sehemu fulani akidai kwamba mimi ni bahiri, (nadhani alimaanisha bahiri wa kutoa maksi za upendeleo!), nataka niliambie Bunge lako tukufu kwamba kwa viwango ambavyo Mhe. Naibu Spika alivyoonesha humu ndani, hakika ningempa maksi za haki asilimia 100 kama walivyofanya maprofesa...