HIZI NDIO TAARIFA ZENYE UHAKIKA KUHUSU ALIYEKUWA MPENZI WAKE LULU MICHAEL
Mitandao ya kijamii kuanzia kwenye Whatsapp mpaka twitter, Facebook na Instagram siku hizi imekua na nguvu kubwa na ndio maana hata taarifa zinaenea kwa kiasi kikubwa sana siku hizi bila kungoja Magazeti, Radio au TV. Najua kama unafatilia habari zinazoendelea mjini utakua umekutana na voicenote au taarifa ya kifo cha huyu ndugu yetu inaweza kuwa imekufikia lakini sio kwa usahihi, au chanzo cha kifo kinaweza kuwa kimepotoshwa. Sasa familia ya Marehemu Lusekelo Samson Mwandenga ( Secky ) imekanusha taarifa zinazoendelea kusambazwa kupitia voice note na kwenye mitandao kuhusu chanzo cha kifo chake na kwamba alikwenda kwenye birthday, "ukweli ni kwamba aliumizwa na kiti cha kioo akiwa kambeba mtoto wake nyumbani kwake, akapelekwa hospitali na baadae akafariki akiwa Hospitali, hakuna kingine zaidi ya hapo". Secky alikua rafiki wa watu wote wakiwemo wasanii wengi wa bongofleva na hata bongomovie pia ndio maana msiba huu umewagusa kutokana ...