Mbunge Chadema Avuliwa Ubunge
Aliyekuwa Mbunge wa Longido, Mhe. ONESMO NANGOLE. Kesi iliyokuwa inaunguruma kuanzia tarehe 29.02.2016 katika Mahakama Kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii. Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea Ubunge wa CCM, Jimbo la Longido, Dk. KIRUSWA alifikisha mahakamani shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi dhidi ya Mbunge wa Longido, Mhe. ONESMO NANGOLE. Akisoma hukumu hiyo, Jaji MWAGESI alisema kwamba mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa na Wakili Dk. Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka. Katika shauri hilo, dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikuwa ni; 1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa Mhe. Onesmo Nangole 2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mhe. Nangole 3.Kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura 4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje. 5.Kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matok...