Posts

Showing posts from September 7, 2018

Breaking News: Baba Mzazi wa Profesa Jay Afariki Dunia

Image
       Profesa J. MBUNGE wa Mikumi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  Joseph Haule (Profesa Jay), amefiwa na baba yake mzazi leo akiwa katika Hospitali ya  St. Kizito,  Mikumi, ambapo alikuwa asafirishwe kwenda kupata matibabu zaidi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Prof. Jay amethibitisha kifo hicho katika mawasiliano aliyoyafanya kwa njia ya simu akiwa Dodoma.

Mashabiki watoa ya moyoni baada ya Diamond kumpost Irene Uwoya

Image
 Wiki hii wakati muimbaji Diamond Platnumz anahojiwa na Wasafi TV alifunguka mambo mbalimbali kuhusu maisha yake pamoja na kueleza kuwa kwa sasa hayupo kwenye mahusiano na mwanamke yeyote. Hatua hiyo ilikuja baada ya muimbaji huyo kumtuhumu Hamisa Mobetto ambaye ni mzazi mwenzake kwamba alienda kwa mganga ili airoge familia yake. Ijumaa hii muimbaji huyo ameibua hisia tofauti mtandaoni kwa mashibiki wake na wadau wa burudani baada ya kupost picha ya mke wa rapa Dogo Janja, Irene Uwoya bila kuandika ujumbe wowote. Kama unavyojua picha inazungumza zaidi ya maneno 1000 ambapo wadau wengi katika mitandao ya kijamii wamekuwa na maoni tofauti huku wengi wakihisi msanii huyo anatafuta kiki kupitia mrembo huyo. Angalia maoni ya mashabiki hao. masikini_jr Kuwa Star ili uwe na amani oa mwanamke mwenye sura ya babake kwasababu Mdogo wake dullysykes anapenda ku review mafile mazuri kama yote duh!!! Sasa janjaro kama nakuona 😂 😂 😂 saidsabin70 @evansmbesigwe h...

Linah afunguka kuhusu unene wake.

Image
Mwanadada Linah Sanga amefunguka na kusema kuwa swala la kuongezeka kwa mwili wake baada ya yeye kujifungua hakuathiri kazi zake kwa sababu anaweza kufanya kitu chochote jukwaani kuwafurahisha mashabiki wake, Hii inakuja baada ya moja ya picha yake ya wikiendi hii kusambaaa sana katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiwa kama amenenepa sana na kuwa anaweza kushindwa kufanya show nzuri kama zamani, Akiongea na  Clouds fm Linah anasema; "Mazoezi nafanya ya kawaida tu, naupenda sana mwili wangu, mimi naona kawaida tu kuongezeka kwangu hakujaniathiri chochote nafanya kazi zangu kama kawaida, napiga shoo jukwaani na najiona ni mwepesi kama kawaida, unajua kuwa watu wembaba lakini wazito, lakini mimi unene nilionao haunipi changamoto zozote ninapokuwa jukwaani nawaburudisha mashabiki wangu kama kawaida, halafu ujue kwamba mimi sio dansa mimi ni mwanamuziki naimba nitakavyo sio lazima niruke ruke"

Zari aandika waraka mzito

Image
 Mashabiki wengi wameupokea kwa furaha ujumbe wa Zari the Bosslady kwa kile wanachoamini ujumbe huo unamlenga Hamisa Mobetto. Zari The Bosslady ametumia ukurasa wake wa Instagram kueleza kuwa; 'Usimpe mtu yeyote nguvu ya kuchagua kati yako na mtu mwingine... kama hukubaliki, ondoka na usiangalie nyuma na wala usimweleze mtu. Situmi chochote zaidi ya upendo kwako , Sasa futa machozi na urekebishe,'. "Never give anyone the power to 'choose' between you and someone else. If they can't decide, decide for them. Walk it away and never look back. Go where your celebrated. Don't even explain i to anyone, your journey is yours. NOBODY has to understand it but YOU. Sending nothing but love you sis in TZ, Now wipe those tears and fix that. Ujumbe huo wa Zari unakuja ikiwa ni hivi karibuni Hamisa Mobetto ameingia kwenye shutuma nzito kwa kile kinachodaiwa kuwa alikuwa akipanga njama za kumloga Diamond Platnumz na familia yake. Zari the Bosslady...

Hiki ndio Kilichomkuta Mchina baada ya kumuita Rais Kenyatta nyani

Image
Mfanyabiashara raia wa China anaeishi nchini Kenya, Liu Jiaqi amekamatwa kufuatia kusambaa kwa video yake katika mitandao ya kijamii inayomuonesha akiwakashifu raia pamoja na Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta. Taarifa ya uhamiaji nchini Kenya imesema “Kibali chake cha kazi kimefutwa na atafukuzwa nchini kutokana na ubaguzi”. Video hiyo iliyosambaa katika katika mitandao ya kijamii inamuonesha mfanyabiashara huyo akirekodiwa na mfanyakazi wake huku akisema, “Kila mmoja, kila mkenya ni kama nyani, akiwamo Uhuru Kenyatta, hao wote”. Aliposhauriwa na mfanyakazi huyo kuwa arejee kwao China endapo hapendi kuendelea kuishi Kenya, alijibu, “Mimi si mkazi wa hapa, sipapendi hapa, watu wake ni kama nyani na sipendi kuongea nao, pananuka harufu mbaya, masikini na watu ni weusi, siwapendi. Kwanini hawako kama watu weupe, kama wamarekani ?”. Kwa mujibu wa msemaji wa ubalozi wa China nchini Kenya, Zhang Gang, video hiyo ilirekodiwa mwezi Juni na tayari alishachukuliwa hat...