HAWAENDANI LAKINI NDO HIVYO TENA,SOMA HAPA
Aunt Ezekiel na Moze Iyobo. NImtazamo wa wengi kuwa baadhi ya mastaa ambao wapo kwenye uhusiano hawaendani kabisa kutokana na muonekano wao, tabia zao na hata fani zao kuwa tofauti. Kuna mastaa wa Bongo na wa Mamtoni ambao mapenzi yao yalivyoanza yaliwashtua watu mbalimbali na wengine kudai hayafiki mbali huku wale wanaotazamiwa kuendana kwa kila kitu wakimwagana vibaya mfano, Diamond Platnumz na Wema Sepetu, Rihanna na Chris Brown na wengineo wengi. AUNT EZEKIEL NA MOSE IYOBO Aunt Ezekiel ambaye ni staa wa Bongo Muvi alidai ‘kudate’ na dansa wa Diamond Platnumz, Mose Iyobo, hiyo ilijulikana mwishoni mwa mwaka jana baada ya Aunt Ezekiel kudai kuwa mimba hiyo ni ya dansa huyo. Uhusiano huo uliwashtua mashabiki wengi wa staa huyo ambapo mpaka sasa hawakubaliani na uhusiano huo wakidai kuwa kuna mtu nyuma ya Mose ambaye ndiye muhusika wa mimba ya Aunt kwa kigezo kuwa Mose hana jeuri ya pesa ya kuweza kumuweka Aunt mjini. .NAY WA MITEGO NA SHAMSA FORD Huu ni moja tu ya mfano wa...