MAHUSIANO
Tabia Ya Kuzoeana inavyoweza kuathiri Maisha yako ya kimahusiano
Kuzoeana baina ya wanandoa ni jambo zuri, kwa maana ya kila mmoja kumfahamu mwenzake, lakini kuzoeana huku kunaweza kuzalisha dharau hususani kwa upande wa mwanamke kwa kutojali usafi wake, mavazi anayovaa, chakula anchopika, nidhamu ya nyumba na mpangilio kwa ujumla.Matatizo mengi ndani ya nyumba yanaweza kusababishwa na moja au baadhi ya tabia hizo, ambazo huenda ikawa hazitokani na dharau, bali kuzoeana, kwa mfano, siku za mwanzo wa ndoa mwanamke huwa anajali sana usafi wa mwili wake, umaridadi wa nguo anazovaa, usafi wa nyumba na nidhamu ya hali ya juu, upishi wa chakula unaozingatia vionjo na ubunifu, mapokezi yenye bashasha na wakati mwingine hata kumkumbatia mumewe arudipo kutoka kazini.
Lakini baada ya kuzoeana yote hayo hubadilika, mwanamke huhisi kuwa hana jipya la kumuonyesha mumewe, hujiona wameishakuwa watu wazima sasa, na mara nyingi utakuta mwanamke huyu anashinda na sare (uniform) moja kuanzia asubuhi hadi anapopanda kitandani usiku, mambo ya Hinna, nguo za fashion, salon, manukato, kujipamba na dhahabu huyafanya pale anapotoka kwenda harusini na sio nyumbani. Huku ndio kuzoena, na tafsiri sahihi ni kudharau.
Hivyo ili kulinda kibarua cha chako cha mahusiano ni vyema ukajifunza kila wakati kutofanya vitu ambavyo vimekuwa havijayajengi mahusiano yako.
Ahsante kwa kuendelea kuwa msomaji wetu, kwa maoni na ushauri usisite kukutumia ujumbe kwa njia ya email
.........................................................................................................
Zari Athibitisha Kuwa Hajarudiana na Diamond
MPENZI wa zamani wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kupitia akaunti yake ya Snapchat amethibitisha taarifa kuwa yeye na Diamond hawajarudiana bali wameelewana kwa ajili ya kulea watoto wao.Tangu wiki iliyopita kulikuwa na tetesi zilizodai kuwa Diamond na Zari wamerudiana baada ya wawili hao kuonekana pamoja nchini South Africa na watoto wao.
Zari amefungukia tetesi hizo na kusema yeye na Diamond hawajarudiana kuwa wapenzi bali wameamua kuelewana kwa ajili ya kulea watoto wao.
Zari amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Snapchat ambapo aliandika:
Tetesi za Diamond na Zari kurudiana zilianza baada ya wawili hao kukutana nchini South Africa baada ya kutoanana kwa miezi minne baada ya kuachana.
....................................................................................................
Mke wa P Funk: Napambana na Kajala
MKE WA prodyuza maarufu Bongo, Paul Matthysse ‘P Funk’, Samira amefunguka kuwa licha ya kukutana na mitihani mingi ndani ya ndoa yake lakini kamwe hatokubali kuondoka nyumbani kwake na kumuachia nyumba muigizaji Kajala Masanja ambaye ni mzazi mwenziye na mume wake, kama alivyokuwa amepanga awali na atapambana naye.Akizungumza kwa uchungu sana, Samira alisema kila uchwao anakutana na kashfa nyingi zinazomhusisha mumewe na Kajala lakini ameaua kukomaa na ndoa yake.
“Yaani mateso ninayokutana nayo kwenye ndoa yangu ni Mungu pekee ndio anajua tena kwenye hali hii ya ujauzito niliyo nayo, awali nilipanga niondoke nimuachie nyumba lakini nimeona nikomae hadi kieleweke,” alisema Samira.
Mara nyingi Kajala alipokuwa akiulizwa kuhusiana na kuingilia ndoa hii ya mzazi mwenzie amekuwa akikana mara na kusema kuwa kuwa P Funk ni baba wa mtoto wake na si vinginevyo ingawa video mbalimbali zinavuja zikiashiria ni wapenzi.
Stori: Mwandishi Wetu
.....................................................................................................
Mbinu Za Kumfurahisha Mpenzi Wako Muwapo Faragha
TENDO la ndoa (kwa wanandoa) si tu linatumika kuboresha uhusiano kati ya mume na mke bali pia ni dawa inayoweza kuutibu mwili, akili na hisia. Hata hivyo, lazima liwe ni tendo lililokamilika, kwa maana lazima mwanaume na mwanamke wote walifurahie na kuridhika.Tendo hili lisipofanyika kwa ukamilifu wake, hubadilika na kuwa kero kubwa na janga kwa wanandoa. Kama ambavyo nimekuwa nikieleza mara kwa mara, sidhani kama yupo mtu ambaye hataki kumfurahisha mwenzi wake wawapo faragha.
Tatizo ni kwamba wengi hawana maarifa ya nini cha kufanya awapo faragha na mwenzi wake, na matokeo yake wamekuwa wakijiendea wanavyoweza, kama kutembea kwenye giza totoro usiku wa manane.
Hakuna mahali ambapo unaweza kufundishwa namna ya kumfurahisha mumeo au mkeo, angalau kidogo wazee wetu enzi zao walikuwa wanapelekwa jandoni na unyagoni, siku hizi unakuja kujifunzia ndani ya ndoa, yaani kama ni mechi ya mpira wa miguu basi unajifunzia kutuliza mpira na kupiga danadana uwanjani wakati wa mechi ambayo ni lazima ushinde.
M f a n o mwepesi ambao huwa napenda kuutumia ni kwamba kila mtu anaweza kuwa anatamani kupiga gitaa na kuzalisha muziki mzuri, lakini hebu jiulize, kama hujawahi kujifunza kupiga gitaa na ukaelewa, ukipewa gitaa sasa hivi unaweza kupiga na kutoa muziki mzuri? Jibu ni HAPANA.
Mapenzi ni sanaa, lazima ukubali kujifunza na kuyatafuta maarifa mahali popote yalipo ili uwe bora, huyo uliyenaye unaweza kuwa unafanya kila kitu kwa ajili yake, unajitahidi kumuonyesha upendo wa hali ya juu lakini kama hujui nini cha kufanya muwapo faragha ili afurahi, ni sawa na kazi bure. Ni kwa msingi huo ndiyo maana nikaamua tujadiliane mada hii kama inavyojieleza hapo juu.
MAANDALIZI YA KIHISIA
Jambo la kwanza ambalo unatakiwa kulifahamu, ni kwamba ili mume au mke afurahie tendo muwapo faragha, lazima awe ametulia kihisia. Haiwezekani mmetoka kukwazana kuhusu jambo fulani, hamjapata suluhu na kila mmoja ana hasira halafu ndiyo mnaingia uwanjani, hamuwezi kufurahia tendo kwa mtindo huo na hii inawahusu wote.
Maandalizi mazuri ya tendo yanaanzia katika maelewano, mpokee vizuri kwa maneno yaliyojaa bashasha, kwa sauti ya upole, mbembeleze, mpetipeti na msifie! Ukiikamilisha kwa ukamilifu hatua hii ya kwanza na ya muhimu, basi utakuwa tayari umeshamuingiza kwenye safari ya kuelekea kufurahia tendo.
Mnapokuwa eneo la tukio, hutakiwi kuwa na papara! Lazima kwanza na wewe akili yako uitulize na badala ya kukimbilia kuingia mchezoni na kuanza kupiga mbizi kama mtu anayejifunza kuogelea, unatakiwa kwanza kutumia muda wa kutosha kupasha misuli moto.
Muda unaoshauriwa kitaalamu, ni angalau dakika thelathini
ndani ya muda huu mfanyie yale mambo yatakayoamsha hisia zake za ndani, viungo vya mwili wako kama mikono, vidole, mdomo, masikio vinaweza kuzalisha hisia nzuri sana kama utakuwa unajua nini unatakiwa kufanya kwa wakati gani.
Narudia tena, epuka kuwa na papara za kukimbilia uwanjani, maandalizi ni muhimu sana kwani yatamuandaa mwenzi wako kimwili na kihisia. Ukiwa na uhakika kwamba maandalizi yamefanyika kwa ukamilifu, sasa unaruhusiwa kuendelea na hatua kubwa na ya muhimu inayofuatia.
Katika hatua hii ambayo kimsingi ndiyo inayowaunganisha, pia unatakiwa kuwa na uelewa juu ya nini cha kufanya na kwa mtindo gani, siyo unaingia kwa papara kama unakimbizwa, hapana. Hapa pia unatakiwa kujifunza zaidi ili kuhakikisha unaibuka mshindi kwa kumfikisha mwenzi wako kwenye kilele cha safari yake ya huba.
Kwa leo tuishie hapa, tutaendelea wiki ijayo sehemu ya pili.
...................................................................................
Aina 10 ya Wanawake Wanaopendwa na Wanaume
WENYE MSIMAMO
Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.
WAPENDA USAWA
Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50.
WANAOJUA MAPENZI
Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa kutosheleza katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani.
MARAFIKI
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani.
WA WAZI
Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo.
WANAOJITEGEMEA
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina naomba vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja.
WASIO NA PRESHA
Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi.
MARIDADI
Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje. Lakini pia ni welewa wa mazingira, si wasamba. Wanapendeza kwa muonekano.
WANAORIDHIKA
Wanawake ambao hulidhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.
WA MMOJA
Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo wanahitajika sana. “Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.
Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.
WAPENDA USAWA
Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50.
WANAOJUA MAPENZI
Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa kutosheleza katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani.
MARAFIKI
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani.
WA WAZI
Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo na uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo.
WANAOJITEGEMEA
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina naomba vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja.
WASIO NA PRESHA
Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi.
MARIDADI
Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje. Lakini pia ni welewa wa mazingira, si wasamba. Wanapendeza kwa muonekano.
WANAORIDHIKA
Wanawake ambao hulidhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.
WA MMOJA
Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo wanahitajika sana. “Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.
Hivi Ndivyo Vitu Hatari Vinavyoweza Kuharibu Na Kuvunja Ndoa Ya Wapendanao Katika Familia
WAPENZI
wanagombana, ndoa zinavunjika na familia nyingi zipo kwenye msoto kwa
sababu ya ubinafsi. Tunazungumza mengi lakini ukweli ni kwamba endapo
kila mmoja atafanikiwa kuushinda ubinafasi, upendo utashamiri kila kona.
Ubinafsi una matawi mengi. Mtu anaposaliti, maana yake ametekwa na tamaa binafsi. Anashindwa kutambua kwamba yeye ni mpenzi wa mtu, kwa hiyo anatakiwa kulinda penzi la mwenzake. Hajui kama anachokifanya ni dhuluma ya hali ya juu.
Ukweli ni kwamba unapoanzisha uhusiano na mtu, maana yake umeamua kumchagua yeye ndiye amiliki penzi lako. Kwa hiyo ukienda kulitoa kwa mwingine, huo ni ubinafsi. Umeingiwa na umimi kwa kuona kwamba unatoa rasilimali za ndani ya mwili wako mwenyewe.
Kwa nini ukimfumania mwenzi wako panachimbika? Ni kwa sababu alichokitoa kwa mtu mwingine ni chako, kwa maana hiyo amekutendea dhuluma. Ndiyo maana ukawa na jeuri ya kupigana kwa sababu haki yako imetumika ndivyo sivyo.
Hivyo basi, usaliti ni ubinafsi. Umeingiwa na jeuri kwamba unacho ndani ya mwili wako, kwa hiyo unaweza kukitumia bila kumshirikisha mwenzi wako. Hiyo ni tabia mbaya mno. Kabla ya kusaliti, fikiria
Kama inauma, ni kwa nini umtende mwenzako? Je, umemuona yeye hana moyo? Anza leo kukemea ubinafsi. Popote pale utakapoona unachukua nafasi, upinge kwa sababu ni adui mkubwa mno kwenye mapenzi. Siku zote usiseme “nipo”, sema “tupo”.
Unapozunguka, usiwaze “upo”, unatakiwa kuwaza “mpo”. Hii itakusaidia kulinda siti ya mwenzako kila utakapokwenda. Hakikisha nafasi ya mwenzi wako haichafuliwi au kutolewa mkopo. Kama ilivyo kwenye soka, wachezaji huchezea timu nyingine kwa mkopo ndivyo na mapenzi ya sasa yalivyo.
Ni kweli mtu ana mpenzi wake lakini anavyojieleza anatoa
picha kwa muulizaji kuona kwamba aliyepo si muhimu sana. Hii husababisha muulizaji aombe kukaa na baadaye hukaribishwa. Wengi walikaribishwa kwa mkopo, mwisho wakawa wamiliki wa jumla.
Kwa nini umwambie huyo mtu kwamba anaweza kukaa, wakati unajua siti ina mmiliki wake halali? Kwa porojo za kitoto, eti mnaambiana mfanye siri. Kinachosikitisha ni kwamba ukisikia na mwenzako naye kagawa siti yako kwa mwingine, macho yatakutoka kwa hasira.
Si wakati wa kuchukia unapotendwa, bali unatakiwa uache
ubinafsi. Haliitwi penzi bila kuwepo watu wawili. Lazima uhakikishe unalinda la mwenzako ili na lako lilindwe. Somo la mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, linafundisha kuacha ubinafsi. Mfikirie mwingine.
Kama ambavyo ubinafsi unavyowatesa wananchi pale kiongozi mwenye dhamana kiserikali anaposhindwa kutimiza majukumu yake na kuamua kushughulikia shida zake binafsi, huku akitumia rasilimali za umma, ni kirusi hatari kila upande.
Baba anapoamua kufuja fedha wakati anajifahamu anayo familia inayomtegemea, huo ni ubinafsi. Anafikiria kutumbua yeye binafsi, wakati anatakiwa kujenga msingi wa familia. Anashindwa kujua kwamba fedha anazotafuta si zake peke yake.
Kama anaona anatakiwa kutumia fedha zake peke yake, basi hapaswi kujipa mzigo wa kumiliki familia. Mtu anapokuwa baba au mama, uamuzi wake unatakiwa uwe kwa ajili ya wengi. Kumaliza mshahara kwenye kumbi za starehe ni ukatili kwa familia hususan mtoto ambaye hautakavyoumia pindi utakaposalitiwa. Usijidanganye kwamba unajimiliki mwenyewe. Wewe unamilikiwa na familia yako, kwa hiyo una deni na wajibu mkubwa kwa wale wanaohusika. Kabla ya kwenda nyumba ya kulala wageni na huyo unayemtamani, fikiria kwamba unamilikiwa.
Baba au mama, anapokwenda hoteli na mpenzi wa nje. Akakubali kuvua nguo na kufanya mapenzi. Ajitambue kuwa anachezea maisha ya watu wengine. Kuna maradhi, kwa hiyo unatakiwa uwe na afya njema ili wanaokumiliki waendelee kupata huduma yako.
Unafahamu kwamba mapenzi yanaua. Unaelewa kuwa unaposhindwa kuwa mtulivu nyumbani, unaiba muda wa familia yako. Kumbe sasa, fedha siyo zako ila ni za familia. Unaweza kupata picha kwamba viungo ni vyako lakini penzi si lako. Ukilitoa ni wizi, ni dhuluma iliyopitiliza. ZAIDI
kukuomba umlete duniani.
Ubinafsi una matawi mengi. Mtu anaposaliti, maana yake ametekwa na tamaa binafsi. Anashindwa kutambua kwamba yeye ni mpenzi wa mtu, kwa hiyo anatakiwa kulinda penzi la mwenzake. Hajui kama anachokifanya ni dhuluma ya hali ya juu.
Ukweli ni kwamba unapoanzisha uhusiano na mtu, maana yake umeamua kumchagua yeye ndiye amiliki penzi lako. Kwa hiyo ukienda kulitoa kwa mwingine, huo ni ubinafsi. Umeingiwa na umimi kwa kuona kwamba unatoa rasilimali za ndani ya mwili wako mwenyewe.
Kwa nini ukimfumania mwenzi wako panachimbika? Ni kwa sababu alichokitoa kwa mtu mwingine ni chako, kwa maana hiyo amekutendea dhuluma. Ndiyo maana ukawa na jeuri ya kupigana kwa sababu haki yako imetumika ndivyo sivyo.
Hivyo basi, usaliti ni ubinafsi. Umeingiwa na jeuri kwamba unacho ndani ya mwili wako, kwa hiyo unaweza kukitumia bila kumshirikisha mwenzi wako. Hiyo ni tabia mbaya mno. Kabla ya kusaliti, fikiria
Kama inauma, ni kwa nini umtende mwenzako? Je, umemuona yeye hana moyo? Anza leo kukemea ubinafsi. Popote pale utakapoona unachukua nafasi, upinge kwa sababu ni adui mkubwa mno kwenye mapenzi. Siku zote usiseme “nipo”, sema “tupo”.
Unapozunguka, usiwaze “upo”, unatakiwa kuwaza “mpo”. Hii itakusaidia kulinda siti ya mwenzako kila utakapokwenda. Hakikisha nafasi ya mwenzi wako haichafuliwi au kutolewa mkopo. Kama ilivyo kwenye soka, wachezaji huchezea timu nyingine kwa mkopo ndivyo na mapenzi ya sasa yalivyo.
Ni kweli mtu ana mpenzi wake lakini anavyojieleza anatoa
picha kwa muulizaji kuona kwamba aliyepo si muhimu sana. Hii husababisha muulizaji aombe kukaa na baadaye hukaribishwa. Wengi walikaribishwa kwa mkopo, mwisho wakawa wamiliki wa jumla.
Kwa nini umwambie huyo mtu kwamba anaweza kukaa, wakati unajua siti ina mmiliki wake halali? Kwa porojo za kitoto, eti mnaambiana mfanye siri. Kinachosikitisha ni kwamba ukisikia na mwenzako naye kagawa siti yako kwa mwingine, macho yatakutoka kwa hasira.
Si wakati wa kuchukia unapotendwa, bali unatakiwa uache
ubinafsi. Haliitwi penzi bila kuwepo watu wawili. Lazima uhakikishe unalinda la mwenzako ili na lako lilindwe. Somo la mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, linafundisha kuacha ubinafsi. Mfikirie mwingine.
Kama ambavyo ubinafsi unavyowatesa wananchi pale kiongozi mwenye dhamana kiserikali anaposhindwa kutimiza majukumu yake na kuamua kushughulikia shida zake binafsi, huku akitumia rasilimali za umma, ni kirusi hatari kila upande.
Baba anapoamua kufuja fedha wakati anajifahamu anayo familia inayomtegemea, huo ni ubinafsi. Anafikiria kutumbua yeye binafsi, wakati anatakiwa kujenga msingi wa familia. Anashindwa kujua kwamba fedha anazotafuta si zake peke yake.
Kama anaona anatakiwa kutumia fedha zake peke yake, basi hapaswi kujipa mzigo wa kumiliki familia. Mtu anapokuwa baba au mama, uamuzi wake unatakiwa uwe kwa ajili ya wengi. Kumaliza mshahara kwenye kumbi za starehe ni ukatili kwa familia hususan mtoto ambaye hautakavyoumia pindi utakaposalitiwa. Usijidanganye kwamba unajimiliki mwenyewe. Wewe unamilikiwa na familia yako, kwa hiyo una deni na wajibu mkubwa kwa wale wanaohusika. Kabla ya kwenda nyumba ya kulala wageni na huyo unayemtamani, fikiria kwamba unamilikiwa.
Baba au mama, anapokwenda hoteli na mpenzi wa nje. Akakubali kuvua nguo na kufanya mapenzi. Ajitambue kuwa anachezea maisha ya watu wengine. Kuna maradhi, kwa hiyo unatakiwa uwe na afya njema ili wanaokumiliki waendelee kupata huduma yako.
Unafahamu kwamba mapenzi yanaua. Unaelewa kuwa unaposhindwa kuwa mtulivu nyumbani, unaiba muda wa familia yako. Kumbe sasa, fedha siyo zako ila ni za familia. Unaweza kupata picha kwamba viungo ni vyako lakini penzi si lako. Ukilitoa ni wizi, ni dhuluma iliyopitiliza. ZAIDI
kukuomba umlete duniani.
.................................................................................................................................................................
Sababu kubwa za watu kuchepuka katika mahusiano ya kimapenzi ni hii
Niliwahi kusema ya kwamba ya kwamba “mchepuko ni dili feki” wengi wakabishana sana, na leo naomba kurudia kusema ya kwamba mchepuko ni dili feki kwa sababu michepuko ndio chanzo cha mifarakano ya ndoa zilizo nyingi ulimwenguni kote hii ni kwa mujibu wa utafiti usio rasmi lakini ndio ukweli wenyewe. Na miongoni mwa sababu inayopelekea kutokea kwa michepuko ni:
Penzi kupoa au kufa
Penzi linapopoa au hata linapokufa huwa inaonyesha wazi kabisa dalili zote za awali. Kwenye kupoa mhusika anaweza kuanza kujihisi ndani ya moyo wake kutompenda mwenzake kama alivyokuwa akimpenda awali. Inawezekana mwenzake hajagundua kuanzia mwanzoni kwamba penzi la mpenzi wake limepoa ila kama hali ya kupoa huku itaendelea lazima itagundulika.
Baadhi ya vitu dhahiri vitakavyoweza kukufanya ufahamu kwamba penzi la mwenzako limepoa au kufa nikwamba kuna mambo ambayo uliyazoea kuyaona yakifanywa kawaida hautayaona tena. Kuna vitu vilikuwa vikifanywa pasipo kukumbushana sasa utalazimika kuviomba ili ufanyiwe, utaona kila kitu kinakuwa kigumu kumhusu mwenzako na hata uongeaji au kujibu kwake kunakuwa na walakini.
Kwenye tendo la ndoa nako maranyingi ndiko kwenye kuonyesha taa nyekundu mapema, ule ushiriki, furaha na bashasha zilizokuwapo awali mkiwa kwenye tendo hauzioni tena, tendo la ndoa linafanywa kama jukumu la kawaida na mara nyingine hata hamu ya kushiriki haipo. Hapa ndipo mmoja hukinai hiyo hali ya kulazimishana tendo la ndoa, au kupeana kwa masharti au kunyimwa au hata mmoja kupoteza hamasa ya kulifanya tendo hilo na mtu asiyekuwa na hisia naye.
Huo unakuwa mwanzo wa mmoja au wote kutoka nje ya mahusiano au ndoa. Penzi ni kama moto, ukiwashwa pasipo kuchochewa hupoa au hata kuzima kabisa. Wengi wanapoingia kwenye ndoa wanadhani mkishaoana basi mambo yanajiseti yenyewe tu, mapenzi yanajichanulia yenyewe tu, la hasha! Lazima kuwepo na jitihada za dhati za wanandoa kuhakikisha wanachochea penzi lao, kulilinda na kulipalilia ili liendelee kumea, kunawiri na kuzaaa matunda.
hivyo kupoa kwa penzi husababisha michepuko, hivyo ili uweze kuepuka jambo hili ni vyema ukaepuka visababishi vya ambavyo nimekwusha vieleza hapo awali.............................................................................................................
Kama unataka kudumu katika mahusiano yako Epuka kumwambia mpenzi wako maneno haya.
Endapo umekwisha ingia katika mahusiano au unatarajia kuingia katika mahusiano ya kimapenzi, yapo mambo yanyofaa ambayo junaweza kumwambia mpenzi wako naye akafurahi, lakini yapo mambo ambayo kimsingi hupaswi kabisa kumwambia mpenzi wako. Kwani endapo utaamua kumwambia utatengeneza njia ambayo itawafanya mahusiono yenu yafe mara moja.
Maneno yafuatayo ni hatari kwa kuwa yanaleta madhara makubwa moyoni mwa mlengwa na ni vyema kuzuia kuyatamka kwa namna yoyote ile.
Maneno Mabaya Ambayo Hutakiwi Kusema Kwa Mwenza Wako:
1. Nakuchukia
Chuki ni kitu kikubwa sana,kwa kweli huwezi kuishi na mtu ambaye unamchukia. Hutakiwi kumtamkia mwenza wako neno hili. Unaweza kuchukia tabia yake lakini si yeye mwenyewe. Njia nzuri ni kusema kuwa “Nachukia au sipendi tabia yako ya kuchelewa kurudi nyumbani” au maneno yanayofanana na hayo.
2. Maneno ya Matusi
Maneno kama “mjinga” au “mpumbavu” yasitumike kwa mwenza wako hata kama yana ukweli ndani yake. Japo ujinga ni kutofahamu kitu fulani lakini neno hili linaleta majeraha kama likitoka kwa mwenza. Hasa kama linatoka wakati wa ugomvi au kutofautiana.
Useseme maneno mabaya yanayomshusha mweza wako mfano kuhusu mwonekano mbaya wa mwenza wako kama “sura mbaya”,”Mnene kama nguruwe” n.k
3. Kumfananisha Tabia Mbaya mwezi wako na Wazazi Wake.
“Tabia zako kama mama yako”, au “..kama baba yako” maneno yanayomfananisha mwenza wako na wazazi au familia anakotoka yanachokoza sana na huweka vidonga kwa muda mrefu moyoni na yaepukwe.
4. Acha! Nitafanya Mwenyewe
Katika mahusiano kusaidiana ni jambo la kawaida na muhimu,maneno mabaya ya namna hii yanamvunja moyo mweza wako kutaka kufanya jambo kwako siku nyingine na linaleta utengano na kuvunjika kwa upendo.
5. Maneno Mabaya ya Kukatisha Tamaa
“Hutaweza” ,”Hutafanikiwa” n.k yanavunja moyo kwa mwenza wako na kurudisha nyuma maendeleo.
Ni muhimu kwa wenza kupeana moyo na kusaidiana ili wote muende mbele kwa pamoja. Umoja ni nguvu.
Hivyo nikusihi ya kwamba kama kweli unataka kudumu katika mahusiano ya ndoa acha mara moja kumwambia maneno hayo, bali unatakiwa kumfariji kwa maneno mazuri yenye kuleta upendo wa kweli na kujenga hamasa ya kudumu milele.
...........................................................................................................
Jinsi ya Kukabiliana na Tatizo la Kukosa Hisia za Tendo la Ndoa
TATIZO hili huwatokea wanaume na wanawake. Ni tatizo linaloathiri hali ya kisaikolojia na kimwili. Hamu na hisia za tendo la ndoa kitaalamu huitwa Libido au Sex drive, ndivyo humsukuma binadamu ashiriki tendo hili. Libido au sex drive hutofautiana kiwango kati ya mtu na mtu. Wapo wanaume wenye kiwango kikubwa na wapo wenye kiwango kidogo na wenye kiwango cha wastani.Hali hii hivyohivyo ipo kwa wanawake. Mwanaume mwenye kiwango kidogo cha libido au sex drive huhisi amepungukiwa nguvu za kiume, kumbe yupo vizuri ila tatizo ni kwamba hana hamu na hisia. Mtu mwenye kiwango cha juu cha libido na sex drive, awe mwanaume au mwanamke huwa hawatulii na hawatosheki, huhangaika huku na kule. Kama ni mwanaume hutamani kila mwanamke anayemuona na kama ni mwanamke hivyohivyo, haangalii kila mwanaume humuona anafaa.
Ingawa ongezeko wengi huliona zuri kuliko mapungufu, lakini ongezeko la libido au sex drive huleta madhara ya kupata magonjwa ya kuambukiza, migogoro ya kimapenzi na hata kuvunjika kwa mahusiano. Mapungufu yake pia huumiza kwani mwanaume hawezi kushiriki tendo la ndoa na mwanamke hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa ujumla, hisia na hamu ya tendo la ndoa huongozwa na mifumo ya kibaolojia, kisaikolojia na kijamii.
Kibaolojia tunahusisha zaidi vichocheo au homoni, aina nyingine za kemikali zipatikanazo mwilini ziitwazo Neurotransmitters, hasa vichocheo vya Testosterone na Dopamine ambavyo vina kazi kubwa katika utengamano wa libido mwilini mwa binadamu. Matatizo ya kijamii yanayoathiri hamu na hisia za tendo la ndoa ni majukumu ya kikazi na kifamilia, matatizo ya kisaikolojia ni yote yanayokusibu na kuumiza akili yako, mfano hali ya kujikataa mwenyewe na kukata tamaa, msongo wa mawazo, haya yote huathiri hamu ya tendo la ndoa.
Hisia au sex drive vinaweza kuathiriwa na uwepo wa magonjwa makali kama kisukari, magonjwa ya moyo, maumivu ya mwili, kansa, HIV, matumizi ya dawa kwa muda mrefu na baadhi ya madawa kama ya moyo, kansa, TB na mengineyo. Hali ya maisha na mahusiano kama sio mazuri pia huathiri kuwa vizuri katika hamu na hisia za tendo la ndoa. Umri huathiri hamu na hisia hasa katika kipindi cha balehe, mara nyingi hamu na hisia za kushiriki ngono huongezeka miongoni mwa vijana wengi.
Mtu yeyote awe mwanamke au mwanaume mwenye hamu na hisia kubwa za kushiriki ngono kitaalamu huitwa Hypersexuality na yule mwenye kiwango kidogo tunaita Hyposexuality. Huwa inatokea mtu akawa na hamu sana ya kuhitaji kushiriki ngono, lakini mazingira hayamruhusu au sheria fulanifulani zinambana kutokana na misingi au taratibu mbalimbali, mfano za kidini au kijamii au kimaadili, basi endapo itatokea atashindwa kujidhibiti au kudhibitiwa na akaipata fursa hiyo, basi huanza kushiriki kwa fujo bila kuangalia anayemfuatilia na kushiriki naye ni mtu wa aina gani, kwa hiyo wakati mwingine mtu anaweza kujikuta amedumbukia katika dimbwi la ngono bila kujijua alianza vipi kumbe ni kushindwa kudhibiti hali ya hisia zake na hamu. Itaendelea toleo lijalo
Haja na utashi wa kushiriki tendo la kujamiiana, au sexual desire miongoni mwa binadamu husaidia kuimarisha maelewano mazuri endapo wawili hao watakuwa na mawasiliano mazuri.
TUPIA MAONI YAKO HAPA
................................................................................
Vyakula 7 vizuri kwa kuongeza nguvu za kiume
Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana
na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na
mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo
linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na
kufanya mazoezi.
Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa makali kama
viagra au vilevi vikali. Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha kwa
muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda
mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia
vyakula vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na
kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia "booster". Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako.
Sababu za kukosa nguvu za kiume
Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi wake. Mwili wako una
maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au mawada, unachotakiwa
kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema, utakuwa bora kama chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili kulinda heshima yako nyumbani?
Vitu vinavyoweza kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume ni kama:
- Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
- Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone
- Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini
Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume
Leo napenda tuangalie vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha nguvu za
kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda
mahusiano na ndoa.
1. Blueberry
Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi
hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini.
Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia
mzunguko mzuri wa damu mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za
kiume.
Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber)
ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla
hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu
husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.
2. Mtini (Figs)
Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni
kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi
cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa
hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.
3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)
Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za kiume.
Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya
mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi
hupelekea hamu na nguvu zaidi.
Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume,
udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.
4. Karanga
Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na
kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa
damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.
5. Vitunguu saumu
Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa
damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume
ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.
6. Ndizi
Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo
kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na
nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo
cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).
7. Chocolate
Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid.
Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa
wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati
wa mapenzi.
Vyakula ni bora kuliko madawa makali
Mie
binafsi nashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo yako yote
ya kiafya. Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona kuna
tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa. Kutumia
madawa makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa kufanya
kazi kama inavyotakiwa. Ni vizuri kama utamuona daktari kama ukiona
hakuna kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.
Mara
nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko, lakini
matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo hutibua
mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako. Mie nashauri uangalie
jinsi unavyokula, nenda kapime vizuri. Kama jogoo ameshindwa kupanda
mtungi, ruksa kuangalia njia mbadala.
Ni
vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa usiku
kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya
ziada ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na
kunyong’onyea. Hii husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri
wako katika kufanya shughuli nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi,
kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi wakati wewe ndio unajiroga, kuwa
makini.
Kama
ilivyo ada kwenye mambo mengi ya kiafya, hakuna muarobaini. Ni vizuri
ukajaribu kubadilisha chakula unachokula, fanya mazoezi mara kwa mara
ili kupata mwili wenye nguvu. Kama utakuwa na swali, weka maoni hapo
chini nasi tutakujibu bila kusika hukusu njia zaidi za kutatua tatizo la
nguvu za kiume.
........................................................................................................
Mambo 6 yakuzingatia katika ndoa
1. kucheka pamoja
Kicheko ni mlango wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia pamoja, na hapa mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu, kama waweza kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya katika vyote. Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu. Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea. Kama utaanza kujizoeza hivi ukiwa nyumbani, taratibu utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine kokote.
2. Jifunzeni kutiana moyo
Kila mmoja awe msaada na tegemeo kwa mwenzake. Jifunze kumtia moyo na kumwezesha mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au apendavyo. Onyesha heshima katika vitu hivyo pia. Kila upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu. Mjenge mwenzako mbele yawengine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye. Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo. Zaidi tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini na kutunyanyua na sisi pia.
3. Jifunzeni kupenda kugusana
Nguvu ya mguso wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote. Lazima mjifunze kujenga tabia ya kugusana mara mpatapo nafasi sio tu mnapokuwa mmelala. Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono mkiongea au mkitembea, kukumbatia bega, kugusa au kuchezea nyewele za mwenzako na njia nyingine zozote za kuonyesha ukaribu kimwili. Wengi wetu huweza kufanya haya kidogo tunapokuwa peke yetu na kamwe sio mbele ya watu, Je, ni aibu? au nidhamu mbaya? au dhambi?
Kugusana ndio mwanzo wakuamsha hisia za kuhitajiana, (hembu jiulize kisirisiri, lini umegusana na mwenzako nje ya chumbani). Kumgusa umpendaye hukuzuia kutowaza au kutovutiwa kumgusa yeyote katika ulimwengu uliojaa wengi waliopweke wanaotamani kuguswa.
Mguso huu wa upendo haumaanishi mguso wa tendo la ndoa, ingawa pia ni vema kujifunza kuijenga lugha ya mguso wa tendo la ndoa katika mahusiano yenu.
4. Zungumzeni hisia zenu
Kati ya vikwazo vikubwa katika ustawi wa mahusiano mengi hususani ya wanandoa ni kutokuwepo kwa majadiliano. Lazima wapenzi wajifunze kuzungumza kuhusu hisia zao. Kama vile maisha yasivyo na ukamilifu, mahusiano na hata ndoa pia hazina ukamilifu. Mpenzi wako hayuko kamili na wala wewe pia sio mkamilifu. Jifunze kuzungumza na umpendaye jinsi unavyojisikia na nini kinachokusumbua. Kuendela tu na migogoro isiyosuluhishwa husababisha moyo kuwa baridi juu ya mwenzako, jiwekeeni muda kila wiki ninyi wawili kutoka ili kuzungumza mambo yenu. Mwambie umpendae yapi yanayojiri kila siku na zipi changamoto zako, mkiweza kujifunza kuwekeza katika muda wa kuwa pamoja taratibu hata muda wenu wa maongezi ya simu utaongezeka.
5. Samehe na kubali kusamehewa
Kamwe tusiache maumivu na machungu yatawale mahusiano yetu. Lazima tujifunze kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia. Kutofautiana katika mahusiano kupo sana, na lazima tuwape tuwapendao nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yetu. Kila hisia za mmoja wetu zinaumuhimu. Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako akuambie yanayo muumiza na msameheane.
6. Linda muonekano wa mpenzi wako
Mara nyingi hatari hii hutokea tunapokuwa katika mizunguko ya huku na huko. Ukaribu na mpenzi wako hauendelezwi tu bali pia unalindwa, pia muonekano wetu lazima ume halisi na sio feki. Vile tunavyoviona katika tamthilia na filamu sio ukaribu ulio halisi. Kama tunataka tuonekane sawa na vile tunavyowaona wengine wanavyopendana basi tunakosea na kujizuia kuwa na mtazamo bora katika mahusiano yetu. Ukianza kupata ukaribu wa kweli baina yako na mwenzako utapoteza hisia ya kuhitaji ukaribu huo na mwingine yeyote, na badala yake utaanza kuulinda ukaribu mlionao.
Lengo liwe kuvitafuta vile vyote mpenzi wako alivyonavyo ambavyo hukuza ukaribu wenu. Mwenzako awe ndio mtu wa muhimu kuliko wote katika maisha yako.
Kicheko ni mlango wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia pamoja, na hapa mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu, kama waweza kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya katika vyote. Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu. Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea. Kama utaanza kujizoeza hivi ukiwa nyumbani, taratibu utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine kokote.
2. Jifunzeni kutiana moyo
Kila mmoja awe msaada na tegemeo kwa mwenzake. Jifunze kumtia moyo na kumwezesha mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au apendavyo. Onyesha heshima katika vitu hivyo pia. Kila upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu. Mjenge mwenzako mbele yawengine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye. Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo. Zaidi tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini na kutunyanyua na sisi pia.
3. Jifunzeni kupenda kugusana
Nguvu ya mguso wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote. Lazima mjifunze kujenga tabia ya kugusana mara mpatapo nafasi sio tu mnapokuwa mmelala. Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono mkiongea au mkitembea, kukumbatia bega, kugusa au kuchezea nyewele za mwenzako na njia nyingine zozote za kuonyesha ukaribu kimwili. Wengi wetu huweza kufanya haya kidogo tunapokuwa peke yetu na kamwe sio mbele ya watu, Je, ni aibu? au nidhamu mbaya? au dhambi?
Kugusana ndio mwanzo wakuamsha hisia za kuhitajiana, (hembu jiulize kisirisiri, lini umegusana na mwenzako nje ya chumbani). Kumgusa umpendaye hukuzuia kutowaza au kutovutiwa kumgusa yeyote katika ulimwengu uliojaa wengi waliopweke wanaotamani kuguswa.
Mguso huu wa upendo haumaanishi mguso wa tendo la ndoa, ingawa pia ni vema kujifunza kuijenga lugha ya mguso wa tendo la ndoa katika mahusiano yenu.
4. Zungumzeni hisia zenu
Kati ya vikwazo vikubwa katika ustawi wa mahusiano mengi hususani ya wanandoa ni kutokuwepo kwa majadiliano. Lazima wapenzi wajifunze kuzungumza kuhusu hisia zao. Kama vile maisha yasivyo na ukamilifu, mahusiano na hata ndoa pia hazina ukamilifu. Mpenzi wako hayuko kamili na wala wewe pia sio mkamilifu. Jifunze kuzungumza na umpendaye jinsi unavyojisikia na nini kinachokusumbua. Kuendela tu na migogoro isiyosuluhishwa husababisha moyo kuwa baridi juu ya mwenzako, jiwekeeni muda kila wiki ninyi wawili kutoka ili kuzungumza mambo yenu. Mwambie umpendae yapi yanayojiri kila siku na zipi changamoto zako, mkiweza kujifunza kuwekeza katika muda wa kuwa pamoja taratibu hata muda wenu wa maongezi ya simu utaongezeka.
5. Samehe na kubali kusamehewa
Kamwe tusiache maumivu na machungu yatawale mahusiano yetu. Lazima tujifunze kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia. Kutofautiana katika mahusiano kupo sana, na lazima tuwape tuwapendao nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yetu. Kila hisia za mmoja wetu zinaumuhimu. Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako akuambie yanayo muumiza na msameheane.
6. Linda muonekano wa mpenzi wako
Mara nyingi hatari hii hutokea tunapokuwa katika mizunguko ya huku na huko. Ukaribu na mpenzi wako hauendelezwi tu bali pia unalindwa, pia muonekano wetu lazima ume halisi na sio feki. Vile tunavyoviona katika tamthilia na filamu sio ukaribu ulio halisi. Kama tunataka tuonekane sawa na vile tunavyowaona wengine wanavyopendana basi tunakosea na kujizuia kuwa na mtazamo bora katika mahusiano yetu. Ukianza kupata ukaribu wa kweli baina yako na mwenzako utapoteza hisia ya kuhitaji ukaribu huo na mwingine yeyote, na badala yake utaanza kuulinda ukaribu mlionao.
Lengo liwe kuvitafuta vile vyote mpenzi wako alivyonavyo ambavyo hukuza ukaribu wenu. Mwenzako awe ndio mtu wa muhimu kuliko wote katika maisha yako.
.........................................................................................................
Mpenzi Wako Hakuridhishi? Mfungukie Bwana!
KWANZA nimshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema. Pia nikukaribishe msomaji wangu katika jamvi lako ulipendalo la UIimwengu wa Mahaba.
Leo nimemua kuzungumzia suala ambalo wapenzi wengi limekuwa likiwatesa hasa wanawake.
Kufikia kilele cha Mlima Kilimanjaro au kufika mshindo, kuridhishana mnapokuwa faragha, penzi ni tamu kama ukimpata anayeyajua mapenzi, kisha mkaridhiana, mkaelewana hakika mtayafurahia mapenzi yenu.
Wanaume wengi huweza kufurahia tendo la ndoa wanapokuwa na wenza wao, kuliko wanawake, wanaume wanaweza kufikia mshindo kwa haraka zaidi kuliko wanawake.
Wakati idadi kubwa ya wanaume ikiongoza kwa kufikia mshindo, wanawake wengi zaidi hushindwa kufurahia tendo hilo na kuishia hewanihewani.
Kama nilivyosema awali, mapenzi ni kuridhiana, kuelewana, kukubaliana sasa inapotokea mko faragha halafu mmoja wapo anafurahia na mwingine anaishia kunukia shombo ya mchezo si sawa.
Na mbaya zaidi anayeishia kugugumia kwa maumivu anachukuliwa poa, eti alishazoea. Hili ni tatizo tena kubwa ambalo linaweza kusabisha usaliti katika uhusiano wenu.
Tatizo hili linaweza kukufanya uanze kuwaza namna ya kuchepuka ili kutafuta tamu ya penzi au wewe mwanaume unaweza kuwa chanzo cha mwenza wako kuchepuka.
Pamoja na kuwa wanawake wengi, hawajui raha ya mapenzi, bado akili za wengi zimetawaliwa na nidhamu ya woga wanapokuwa faragha.
Ni nadra sana kwa mwanamke ambaye hajafurahia penzi la mwenza wake kumuambia ukweli mpenzi wake kuwa hajaridhika kwa sababu zifuatazo:
ATAONEKANA NI MALAYA
Baadhi ya wanawake wanashindwa kuwaambia ukweli wapenzi wao pindi ambapo hawafurahii tendo la ndoa kwa kuhisi anaweza kuonekana ni malaya aliyekubuhu au ni mwanamke anaye-penda sana ngono kuliko kitu kingine.
Kwa mantiki hiyo, mwanamke huamua kupotezea na kubaki akigugumia kwenye mtima wake. Jambo ambalo ni hatari kwa uhusiano wake.
ANAONEKANA HANA ADABU
Wanawake wengine huona tu aibu kuzungumzia suala la faragha na mwenza wake kwa kuamini kuwa halipaswi kuzungumzwa. Anaona ni bora kufa na tai yake shingoni kuliko kusema ukweli.
Wewe mwanamke unayeona aibu kuzungumza na mwenza wako kuhusu kinachokusibu hasa mnapokuwa faragha unakosea kwa kuwa inawezekana mwenza wako hajagundua tatizo
hilo, yeye anahisi ni kidume cha mbegu kwa sababu anakufurahisha kumbe ukweli hujawahi kufurahia.
UKOROFI WA MWANAUME
Wakati mwingine mwanamke anaweza kuhofia kumwambia mwanaume kwa sababu ya tabia au ukorofi alionao.
Pengine huwa hasikilizi ushauri na maoni yake hivyo anaona hata jambo hilo akikuambia itakuwa yaleyale tu.
Kwa tabia hiyo ya kujiona yeye ni kila kitu bila kumpa nafasi mwenza wake, hukosa mambo mengi na mwisho wake hukaribisha michepuko kwenye penzi au ndoa.
Pamoja na mambo yote niliyoyazungumza hapo awali, fika sehemu mwanaume au mwanamke jiulize hivi kwa nini ukubali kuteseka na penzi wakati mpenzi wako unaye?
Kwa nini ufikirie kuchepuka wakati unaweza kuzungumza na mpenzi wako na akawa bora zaidi?
............................................................................................................
Tabia Ndogondogo Zinavyoweza Kuvunja Penzi Ndoa!
LEO kwenye safu yetu hii tutaangalia tabia ndogondogo ambazo zinafanywa na wanandoa au wapenzi lakini wengi wao hawajui kuwa zinachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu uhusiano au kuvunja ndoa.
Kila kukicha napata ujumbe kutoka kwa wanandoa ambao hulalamika kuwa hawawaelewi wenza wao kwani wamebadilika lakini malalamiko mengi yanaelekezwa kwenye tabia hizi ambazo nitakueleza hapa na kama zinakuhusu, kabla ndoa yako haijapinduka unatakiwa kuzifanyia kazi.
Tabia hizo unaweza kuzipitia moja baada ya nyingine, yawezekana ukawa huna zote lakini ukawa na moja au mbili ambazo zinakuhusu. Fuatilia hapa chini;
Kukosa muda wa kubadilishana mawazo na mwenza wako
Wanandoa wengi au wapenzi hawana muda wa kupumzika na wapenzi wao na kubadilishana mawazo. Hii ni kutokana na maisha ya sasa yanavyoenda. Tatizo hili au tabia hii inaweza kukusababishia mwenza wako kukukosa na kuona kuwa hana muda na wewe. Kwa maana hiyo inaweza kusababisha yeye kuvunjika moyo na kuizoea tabia ambayo kimahusiano inafifisha mapenzi.
Usishangae, hilo unaweza kuliona dogo lakini linaweza kuvunja ndoa au kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara kwa sababu tu mume au mpenzi hana muda na mkewe.
Kusema uongo, kuvunja ahadi
Hakuna anayependa kudanganywa hasa pale ambapo hapastahili lakini pia hakuna ambaye anapenda kuahidiwa kitu kisha asitimiziwe. Baadhi ya tulio kwenye uhusiano tunapenda kudanganya sana, kitu ambacho unaweza kukidharau lakini mwenza wako kikamuumiza sana.
Lakini pia hili la kuahidi halafu unapotezea. Kumbuka uliyenaye ni mtu mzima, ukimwambia nikirudi safari nitakuletea zawadi halafu unarudi mikono mitupu bila kuwa na maelezo lazima mwenza wako atakuona unamchukulia kama mtoto. Vijitabia hivi ni vyema ukaviweka pembeni.
Kuonesha kutokumuamini
Kuwa na wasiwasi na mwenza wako kila wakati ni tabia mbaya ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kuivunja ndoa, ni sawa tu na kutokumuamini unayeishi naye. Jenga imani hata kama unatilia shaka jambo f’lani, lifanyie kazi kwa makini na usimuoneshe umpendaye kuwa una mashaka naye mara kwa mara.
Hulalamiki, kila analokufanyia poa tu
Kama mwenza wako hakulalamikii kwa jambo baya unalomfanyia au unalomnyima ni rahisi kujisikia vibaya. Unapokuwa unajaribu kumwambia mpenzi wako kuhusu jambo ambalo amekuumiza na limekuchanganya ni vema ili uweze kukupa furaha.
Ni vizuri kama atafahamu unahitaji nini na unataka nini lakini usipolalamika atakushangaa kwani moja kwa moja atahisi huna upendo naye. Wanandoa wengi huhisi wanapendwa kama watalalamikiwa jambo, hasa wanandoa wanawake wao wakilalamikiwa na waume zao huamini wanapendwa.
Kupuuza tendo la ndoa
Mara nyingi wapendanao penzi hujengwa na tendo la ndoa hasa pande zote zikishiriki ipasavyo. Sasa ikitokea wewe ni mtu ambaye una tabia ya kupenda kupuuza tendo hilo hasa anapokuhitaji mpenzi au mumeo/ mkeo, unamkatisha tamaa mwenza wako. Kumbuka kuwa uhusiano bila ya tendo utaenda pabaya.
Kuwa bize mara kwa mara na mambo yako au maisha yanayokufanya uwe na sababu ya kukosa muda wa kutosha wa kucheza na mwenza wako ni tatizo, kumbuka tendo ni muhimu kuliko chochote.
Wakati wote unatanguliza kazi yako
Kuwa na kazi kwa ajili ya kuwaendeleza kimaisha ni muhimu hasa kwa maisha ya sasa lakini linapokuja suala la uhusiano au ndoa ukiendekeza kazi wakati wote unaweza kujikuta ukivunja ndoa au uhusiano kwa jumla.
Kutumia pesa bila hekima
Pesa ni kitu muhimu sana kwa maisha ya binadamu lakini isipotumiwa kwa umakini inaweza kuleta balaa.
Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unakuwa na matumizi mazuri ya pesa hata kama mnazo nyingi.
................................................................................
YAFAHAMU MAMBO YANAYOWADATISHA WANAWAKE KWA WANAUME..WEWE UMO?
HAKUNA aliyeaibika wakati akijaribu kufanya jambo kwa faida yake. Siku zote kufanya jaribio ni mwanzo wa kuelekea kwenye ufanisi mzuri wa jambo husika.
Rafiki zangu, ni vema nawe ukajiwekea utaratibu wa kujaribu kufanya mambo ambayo unadhani huyawezi, lakini yakileta matokeo chanya yatakuwa na faida kubwa kwako.
Kujaribu kupo katika mambo mengine mengi ya kawaida – ya kibinadamu. Katika mambo mbalimbali ya kila siku. Ukianza na kupata matokeo mazuri, unakuwa mshindi na bila shaka unakuwa umefanikiwa.
Hali ni tofauti katika suala la mapenzi, huku hakuna kujaribu – ni kuamua tu! Hata hivyo, wakati unaamua mambo yako yanayohusu mapenzi ni lazima kichwani mwako utambue kuwa unafanya kitu kwa ajili yako na mtu mwingine (mpenzi wako).
Hapo ndipo kazi inapokuja. Kwa maneno mengine, wakati ukijifikiria wewe katika ulimwengu wa mapenzi, unatakiwa pia kumfikiria mpenzi wako.
Kwa bahati mbaya, katika eneo hili, wanaume wengi huwa hawafikirii sana namna ya kuwafurahisha wenzi wao. Wanahisi ni suala linalowahusu wanawake pekee. Ni kosa.
Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.
Hapa katika Love Moment, nimekuandalia mambo ambayo wanawake wengi wanavutiwa zaidi kutoka kwa wanaume.
Je, wewe ukoje? Una sifa hizo? Hebu twende pamoja katika mada hii ambayo bila shaka itakutoa matongotongo.
USAFI BINAFSI
Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda sana usafi. Ni aghalabu sana kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au ua la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi.
Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi chumbani.
Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele.
KUJIAMINI
Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini – mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia. Siyo anayebabaika.
Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia manukato mapya. Mathalani unakuwa naye katika mtoko, angependa kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.
Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwenye kujiamini na mawazo yasiyo na matege wala makengeza!
KUJITETEA
Kipengele hiki hakina tofauti kubwa sana na kilichopita, lakini hapa ni kwenye upande wa kujitetea zaidi. Wakati unapodai haki yako mbele ya mwanamke wako, suala la kujitetea linapewa nafasi kubwa sana.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi.
Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia haki ya mwanamke wako. Nisieleweke vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni yule ambaye ana nguvu – anafanya mazoezi na ambaye yupo tayari kwa lolote!
Inapowezekana, uwe na uwezo wa ‘kuzichapa’ ikiwa mtakutana na vibaka au watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.
Mwanaume aliye ‘fiti’ ni chaguo la wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu hana nafasi.
KUJALI
Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali. Wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi wako kwa kila hali.
Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai.
UKARIBU
Kati ya vitu vinavyowapa mshawasha mkubwa wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku.
Ni vizuri kuwasiliana naye mchana, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi.
Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako. Hebu tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa.
................................................................................
SEHEMU NNE (4) ZA MWILI USIZOPASWA KUMSHIKA MKEO Nyakati Hizi 18+
Ingawa kuna mtazamo uliojengeka katika jamii kuwa ukishamuoa mwanamke na mkawa mwili mmoja basi una kila haki ya kumshika sehemu yoyote uipendayo hasa wakati unahitaji kufanya nae tendo la ndoa.Lakini utafiti na uzoefu uliokusanywa na wataalam wa mahusiano na ndoa waliofanya mahojiano na wanawake kama kuna sehemu wazisopenda kuguswa na waume zao na nyakati husika, umetoa picha na mtazamo ambao wanaume wanapaswa kuufahamu mapema kabla hawajaingia katika hatari ya kuwa kero au kuwakwaza wake zao.
Kama tunavyofahamu, wanawake ni viumbe wenya mlango mmoja wa ziada wa fahamu kuwapita wanaume. Hii nitaizungumzia siku nyingine. Lakini mlango huu wa ziada ndio huwapa hisia ya ziada pamoja na kuwafanya kujali sana vitu ambavyo mwanaume hasa mwenye haja ya kufanya tendo anaweza asizingatie sana anataka kukidhi haja yake.
Ukifuatilia sehemu hizi za mwili wa mwanamke nitakazozitaja na nyakati zake, utabaini kuwa ni rahisi sana kufahamu kwani mwanamke katika nyakati hizo anaweza kuonesha kusita sana wakati anataka kuguswa.
1. Chuchu wakati miili yao inaendelea na shughuli nyingine za ndani
Idadi kubwa ya wanawake huwa hawapendi kuguswa na wanaume chuchu zao wakati wananyonyesha au wakati wako katika hedhi. Hiki ni kipindi ambacho kama mwanamke ananyonyesha na mwanaume anataka kumgusa sehemu hiyo basi maziwa yanaweza kutoka kwa kasi na kumfanya ajisikie hayuko ‘confortable’ kuendelea na zoezi la kushiriki tendo.
2. Kwapani wanapokuwa wanatoka jasho kabla ya kuoga
Wanaume wengine huwa na hisia za matamanio zaidi wanapoyaona makwapa ya wake zao. Hii ni hali ya kisaikolojia inayojengeka kwa baadhi japo sio wengi. Kuna wanaume wakiona kwapa la mwanamke basi matamanio yao huongezeka mara dufu. Lakini wanawake wengi wameeleza wazi kuwa hujisikia vibaya na kukosa amani pale wanaume zao wanajaribu kuwashika kwapani wakati ambapo wametokwa jasho.
3. Sehemu za siri kabla ya kuoga
Hili ni eneo ambalo wanawake wengi wameonesha kulalamikia waume zao. Kwa mazoea wanaume wengi huwa kama wanawabaka wake zao bila kufahamu, hasa pale wanapotoka safari zao wakiwa na matamanio. Lakini wanawake wengi wameeleza wazi kuwa hupoteza hali ya kuwa ‘comfortable’ pale wanapoguswa na wanaume zao sehemu za siri wakati bado hawajaoga.
Wanaume wengi hujikuta wakishiriki tendo la ndoa na wake zao ghafla baada ya kukamilisha kazi kadhaa za ndani wakati wanawaangalia. Wanaume wanaweza kuwa wanafurahia zaidi tendo hilo lakini wanawake pamoja na kwamba hufurahia pia lakini mlango wao wa ziada wa fahamu huwafanya kukosa amani kwa kiasi fulani wakati wa tendo ukilinganisha na nyakati ambazo wanajiamini ni wasafi.
4. Nywele zao dakika chache baada ya kutoka saloon kujiremba
Ingawa unaamini kuwa mkeo alienda saloon kujiremba kwa ajili ya kukuvutia wewe, usithubutu kutaka kuzivuruga nywele zake dakika chache baada ya kutoka kwa mtaalam wa kutengeneza nywele, hata kama pesa aliyotumia ulimpa wewe.
Hiki ni kama kituko hivi, lakini ndio ukweli. Wanawake hutumia muda mrefu sana kwenye vibanda au saloon za gharama kwa ajili ya kujiremba ili waongeze mvuto. Lakini, hugeuka kuwa walinzi wa vichwa vyao angalau kwa saa kadhaa. Msifie uwezavyo, lakini nywele zake usizivuruge mapema mtaharibiana ‘mood’.
Haya ni kati ya mambo machache ambayo wanaume huyaona madogo sana na kufuatilia yale wanayoamini ni makubwa zaidi. Lakini mambo haya ni kati ya machache yanayokwangua taratibu kuta za hisia za mwanamke kwa mmewe.
............................................................................
Kumteka Mwanamke Mwenye Mapenzi ya Kweli ni Rahisi
NINA afya njema kwasababu yupo anayepigania afya na uzima wangu, lazima nikubali kuwa uwezo wa kuandika makala haya si akili wala nguvu zangu, ni Mungu mwenyewe ndiye anayesimamia haya yote.
Hii ni sababu inayonifanya kila wakati nimshukuru Yeye, maana ni mwema na fadhili zake ni za milele.
Ndugu zangu, ninapozungumza juu ya mapenzi ya dhati namaanisha yale yanayotoka moyoni mwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Hapa mapenzi ya ulaghai hayahusiki, namaanisha mapenzi ya dhati kutoka katikati ya moyo wa mtu kwenda kwa mwingine.
Mapenzi hayo hukamilika baada ya wawili hao kuwa na hisia sawa za mapenzi. Amini kama upo katika uhusiano na mpenzi ambaye hakupendi, yaani wewe peke yako ndiyo unayempenda, wewe ni mtumwa wa mapenzi!
Kama ndivyo, kwanini uwe mtumwa? Msomaji wangu huna sababu ya kuingia katika uhusiano tata, ambao mwisho wa siku utaishia kulia huku wa kukubebembeza akikosekana.
Hebu sasa tugeukie hatua muhimu nilizoandaa kwa ajili ya kukuweka sawa katika mada hii muhimu katika uhusiano wa kimapenzi.
NI KWELI UMEMPENDA?
Suala la mapenzi huhusisha moyo zaidi, moyo wako ndiyo mwamuzi wa mwisho katika hilo, hata siku moja usikubali kulazimisha moyo wako kwa mtu ambaye hujaridhia. Achana na imani kwamba ukimkataa kijana fulani basi bahati inaweza kukupita, nani amekudanganya?
Suala la kuolewa halina bahati, Mungu mwenyewe ndiye mpangaji wa hili, unadhani hakuna mwingine ambaye anaweza kukupenda kwa mapenzi ya dhati na penzi hilo likawa kwa pande zote mbili tofauti na ilivyo sasa? Inawezekana, huna sababu ya kulazimisha penzi kwa mtu ambaye hakupendi.
Mapenzi ni nguzo katika maisha yetu, kama ukifanikiwa kumpata mpenzi ambaye atakupenda na wewe ukampenda ni wazi kuwa maisha yako yatakuwa yenye furaha na hakika utafurahia sana maisha yako na huyo mwandani wako.
Mapenzi yapo hivyo na kama ukijaribu kuyabadilisha utaumia mwenyewe. Wakati mwingine unaweza ukapendwa na mpenzi ambaye hujampenda, unadhani kuna ulazima wa wewe kulazimisha kumpenda?
Moyo wako umeshazungumza na wewe, umekuweka wazi kuwa hauna mapenzi ya dhati kwa mtu huyo, kwanini ujilazimishe?
Tatizo hili mara nyingi huwa kwa wanawake zaidi. Anatokea mwanaume anampenda sana, anapomtongoza anajikuta kuwa hampendi, anachokifanya ni kumwambia kuwa atamjibu baadaye! Lengo la kumwambia hivyo ni kwa ajili ya kujipanga na kufikiria! Mapenzi hayafikiriwi ndugu zangu.
Kama mtu unampenda, unapomuona tu siku ya kwanza, moyo wako hutetemeka juu yake na hutamani uambiwe kitu fulani na huyo aliyeuteka moyo wako ghafla.
Hii inamaana kuwa atakapokuambia kuwa anakupenda, huwezi kusubiri zaidi, hutakuwa na kitu cha kusubiri, ni nafasi uliyokuwa ukiisubiria kwa hamu sana, na hazima utamkaribisha!
HUWEZI KUJIFUNZA KUPENDA
Baadhi ya wasichana, akitongozwa na mwanaume ambaye anaona wazi kuwa hampendi, lakini akawa na mali au uwezo mkubwa kifedha, huamua kumkubali kwa lengo la kupata vitu vya mwanaume huyo.
Hufanya hivyo akijidanganya kuwa atajifunza kupenda akiwa ndani ya uhusiano na mwanaume huyo. Baada ya wazo hili kuingia akilini, huwa hana muda wa kusubiri zaidi, anakubali na wakati mwingine huweza kuingia katika ndoa.
Wataalamu wa uhusiano huita ndoa hizo ‘Ndoa za kichwa-kichwa’, usikubali kuingia katika ndoa ya aina hii hata siku moja. Mwisho wa siku utajikuta ukilia. Kamwe huwezi kujifunza kupenda.
MADHARA YA KULAZIMISHA PENZI
Yapo mengi, lakini kubwa ni lile la kutokutosheka na mpenzi uliyenaye. Anaweza akakupa kila kitu lakini ukakosa penzi la dhati, ambalo ndiyo msingi wa maisha. Unajua kama kuna mtu anakupenda na wewe unampenda, unajihisi furaha na amani siku zote.
Hayo ndiyo mapenzi ya kweli bwana, siku zote hujisikia mwepesi na huru kwa mwenzako. Madhara makubwa zaidi ni pale utakapojikuta ukiingia katia uhusiano na mwanaume mwingine kwa ajili ya kusaka penzi la dhati! Unajua kitakachotokea?
Kama hutaleta magonjwa ndani basi siku moja utafumaniwa, siku lazima utafukuzwa nyumbani kwa mwanaume huyo, na kama ana hasira, anaweza kukua, kumuua aliyekufumania naye au kujiua yeye mwenyewe kukwepa fedheha.
Hapo utauficha wapi uso wako? Fikiria kwa makini…
FIKIA MAAMUZI
Kamwe usijaribu kuingia katika mkumbo huu, mkumbo wa kujifunza kupenda, ni jambo gumu ambalo huweza likaharibu maisha yako kabisa. Jambo ambalo linaloweza kukusababisha ukajuta kuzaliwa.
Kuwa makini, maamuzi yahusuyo mapenzi ni lazima yafanywe kwa umakini wa hali ya juu sana. Unapofanya uamuzi juu ya mapenzi, unakuwa unapanga mustakabali wa maisha yako yajayo. Fanya maamuzi sahihi juu ya maisha yako.
................................................................,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,................................................................
7 Tips to Make a Guy Fall in Love With You
1.Be confident.
Being sure of yourself and your actions is an incredibly attractive
trait. As humans, we long to be with someone who can be confident in
their decisions, in their future, and therefore your future together.
You are resilient and strong – don’t ever doubt yourself! Inner
confidence is sexy and it shows even when you are not trying to push it
forward. Always being confident is a tremendous asset – don’t be timid
about exhibiting max confidence!
2.Learn how to listen.
Every healthy relationship is based on communication and finding true
love will be based on it too. You must be genuinely interested in the
person you would like to pursue – get to know them, where they are
coming from what makes them tick. Be still for a few minutes and just
listen.
3. Look into his soul.
They say that “the eyes are the mirrors to our souls” for a reason. Eye
contact is crucial in any communication especially when you are just
trying to get to know someone. Our mouths can say whatever we want but
our eyes rarely lie. Look at him, study his face, smile, and most
importantly have a blast!
4.Be approachable.
So many women all over the world are dying to find love yet can get very defensive and tighten up and don’t let anyone get too close. A guy needs to know that he can ask you things and you won’t look down on him. Be easy-going and open, engage in conversation, and share your inner thoughts! Relax, he is just a person.
5.Respect his masculinity.
We live in a day and age when we treat everyone equally (at least we try). As the independent woman that you strive to be, it is easy to overlook this. A man wants to feel like a man and be appreciated for his abilities. When he wants to walk you home after your date ‘to keep you safe’ – don’t get mad but rather use this opportunity to spend more time with him!
6.Captivate him.
We all like to believe that we have enchanting personalities. In most cases we do but we push them down because we don’t want to be different. If you want to attract someone – you have to entice him with your charm. Share your thoughts and your passions – show him your last DIY project! Mesmerize him with you.
7.Be YOU.
Speaking of you: don’t forget that you are awesome. And if you are reading this you are already open to new possibilities. Don’t ever hide behind a mask – show your true colors! You always get caught in a lie when you try to conceal something. Be yourself and stay true to who you are. Being calm, open, and humble are the most attractive things in a girl.
...........................................................................................
SABABU 4 ZA WANAWAKE WAJAWAZITO KUFANYA MAPENZI KARIBU KILA SIKU
Baadhi ya wanawake wamekuwa wakiona ujauzito kama mzigo,walioubeba na baadhi wakiona kama zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenye miili yao.
Kubeba ujauzito sio jambo dogo,kukibeba kiumbe tumboni kwa miezi tisa kunaweza kuleta msongo wa mawazo.Zipo njia mbalimbali zinazoweza kumpunguzia mwanamke mjamzito msongo wa mawazo.S.ex katika kipindi cha ujauzito ni best S.ex ambayo huwezi kuipata katika kipindi kingine cha maisha na inasiadia kuimarisha misuli katika njia za uzazi hata baada ya kujifungua.
1.Husaidia presha kushuka.
S.ex katika kipindi cha ujauzito inasidia kushusha presha ya damu.Oxytocin, love homoni inayozalishwa kwa wingi mtu akifanya mapenzi inasaidia kupunguza kama sio kuondoa kabisa msongo wa mawazo na kuhakikisha presha iko katika hali ya kawaida ya mwili.
2.Husaidia mjamzito kupata usingizi mnono.
Mjamzito anakumbwa na mambo mbalimbali yanayoweza kumnyima usingizi kama maumivu kwa mbali kwenye uti wa mgongo,kukojoa mara kwa mara,masaa ya kulala kupungua/kuonekana mafupi fetus anavyozidi kukua katika mfuko wa uzazi.S.ex katika kipindi cha ujauzito kunamsaidia mwanamke kufika kileleni na hivyo kupata usingizi mnono kwani huisi kupungukiwa na mzigo(anarelax).
3.Inasaidia mwanamke kuwa karibu zaidi na mumewe kwenye kipindi hiki.
Bond kati ya mume na mke inaendela kuwepo kwani wanaweza kuendelea kufanya mapenzi kwenye kipindi hiki cha ujauzito.Wanawake katika hiki kipindi wanakuwa na hali isiyo ya kawaida na mara nyingi huwa na hasira wanatakiwa kuangaliwa kwa umakini.Oxytocin inamfanya mwanamke awe anajali,na kuamini kuwa mpenzi wake anamjali.
4.Kupunguza maumivu
Homoni kama oestrogen,prolactin na progesterone zinasaidia damu kupita kwa wingi katika maeneo ya nyonga,na hata kwenye uke uongeza hisia na utelezi.
.................................................................................
MREMBO Jack Wolper Amtema Rasmi Mwanamuziki Harmonize
Akizungumza na mwandishi wetu jana, Wolper alikiri kwamba, yeye na Harmonize, mapenzi yao yamekwisha kabisa.
“Yah! Ni kweli, nimeamua tu kuachana naye. Unajua katika uhusiano kuna kugombana, tumekoseana na kusameheana mara nyingi, sasa tumeamua kila mtu aendelee na maisha yake. Kwangu ni fursa nzuri kwani nitakuwa na amani ya moyo. Maisha yatasonga na nitajikipu ‘bize’ na kazi zangu. “Siwezi kujutia uamuzi huu na moyo wangu umeshazoea, kanikuta nikiwa Wolper na tumeachana nikiwa Wolper labda kama angekuwa amenikuta Fatuma na kunifanya kuwa Wolper.
“Harmonize nimedumu naye kwenye mapenzi kwa mwaka mmoja tu. Nilimkosea, akanikosea kanikosea tena, siwezi kuongelea kitu halisi alichonikosea lakini jua hilo.
“Wakati tukiwa kwenye uhusiano wetu hatujawahi kuchiti (kusaliti) au inawezekana tulichiti na tukasameheana ila kwangu ni rahisi kusamehe kwa kuchiti kuliko kukusamehe kwenye kosa dogo ambalo wewe unaliona ni la kawaida lakini kwangu nikahisi kama unanishusha thamani, na ninapoingia kwenye uhusiano huwa nasema vitu ambavyo sivipendi kukosewa, na nikiona unakosea mara kwa mara najua hiyo ndiyo tabia yako,” alisema Wolper na kuongeza:
“Hata sikumbuki mara ya mwisho niliongea naye lini ila neno lake la mwisho kwangu lilikuwa ni samahani ambalo sijalikubali.” Juhudi za kumpata Harmonize zinaendelea baada ya jana kutokupatikana hewani.
...............................................................................
KAJALA MASANJA ENDELEA KUITESA MIDUME YENYE UCHU
Kajala
Masanja ni mmoja wa waigizaji wenye muonekano Mzuri katika Tasnia ya
Bongo Movie na pia mwenye kipaji kikubwa katika uigizaji wa filam
mbalimbali. Ameweza kuwana filamu nzuri na zenye kufuata maadili hali
iliyomfanya kujizolea mashabiki wa Lika mbalimbali nchini na Nje ya
Nchi.Leo hii nimekuletea Picha zake Tano Kali katika Muonekano tofauti
tofauti. Zicheki hapo Chini. Usisahau kuniachia Maoni yako hapo chini.
Ufanyeje unapompenda aliyependwa?
KWANZA
nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ameniwezesha kuandika haya
tena wiki hii tukiwa wazima. Lakini pia tumshukuru kwa kutuletea kitu
kinachoitwa mapenzi.
Mpenzi msomaji wangu, kupenda hakuna
macho! Moyo ukishapenda hausikii la kuambiwa. Katika hili ndiyo maana
unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa demu ambaye hawaendani kabisa
lakini moyo wake ndiyo umeshapenda.
Ilishawahi kutokea msichana akampenda
kijana mmoja ambaye ni fukara kupita maelezo. Yeye akawa ndiyo
anamhudumia kwa kila kitu. Akamfanyia mpango wa ajira na mwisho wake
wakafunga ndoa.
Sasa hivi wanaishi maisha ya furaha na
amani. Wamegeuka mfano wa kuigwa kwa jinsi wanavyo-pendana lakini huko
nyuma msichana huyo alikuwa akichekwa kwa kutoa penzi kwa mwanaume asiye
na mbele wala nyuma.
Hayo ndiyo mapenzi jamani!
Lakini pia katika kufurukuta kumtafuta
mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume unaweza kujikuta unaangukia kwa
demu ambaye tayari ana mpenzi wake yaani ameshapendwa. Moyo wako
unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana
mtu wake, unafanyaje?
Utapambana kuhakikisha unapata kile
ambacho moyo wako umekipenda au utakubaliana na ukweli kwamba huwezi
kuwa naye kwa kuwa ana mtu wake? Inapofikia hatua hiyo unaweza kujikuta
upo njia panda hasa pale ambapo huyo mwenye mtu wake naye anaonesha kuwa
na chembechembe za mapenzi kwako.
Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kukabiliana na hali hii.
Chunguza
Tumia muda wako mwingi kuchunguza juu ya
uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye
‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo
uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye future
naye.
Usitafute uadui
Baada ya kuchunguza, ukibaini kwamba
uhusiano wao hauko ‘siriasi’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na
likaufurahisha moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na
wanaelekea kuoana, usitafute uadui bure, kaa pembeni.
Una nafasi kwake?
Sawa umetokea kumpenda msichana aliye na
mtu wake, umeshawahi kujiuliza kama una nafasi ndani ya moyo wake?
Anaonesha dalili fulani za kukupenda kama unavyompenda na ni mtu
anayeonesha kukumisi anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi
kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi.
Ni rahisi kubadili uamuzi wake?
Unadhani huyo uliyetokea kumpenda
anaweza kubadili maamuzi ya kumuacha huyo aliyenaye kama kweli hawana
future? Utagundua hilo kwa kuongea naye na kumsikia kama anaweza kufanya
maamuzi hayo ili awe na wewe.
Pingana na moyo wako
Ifike wakati upingane na moyo wako.
Unajua moyo wako kukuambia kuwa unataka kuwa na uhusiano na demu ambaye
tayari ana mpenzi wake wakati mwingine utakuwa unakupotosha.
Kwa hiyo ukiona vipi, pingana nao. Acha
kumng’ang’ania msichana mwenye mpenzi wake licha ya ukweli kwamba,
huenda wewe ndiye mwenye nafasi ya kuwa mume wake na siyo huyo aliye
naye.
Urafiki ni poa?
Umempenda sana na hauko tayari kumkosa
katika maisha yako lakini imetokea kwamba tayari yuko na mtu na umebaini
huna nafasi kwake kabisa? Usiumie, omba angalau urafiki. Siyo urafiki
wa kivile sana ila angalau pale unapotaka kusikia sauti yake kwa
kumsalimia tu, upate nafasi hiyo.
Usiumie, yupo mwingine
Haina haja ya kujitafutia vidonda vya
tumbo bure kwa kuwa tu umebaini uliyetokea kumpenda tayari ana mtu.
Chukulia ni hali ya kawaida, mademu wazuri ambao wanaishi singo wapo
kibao huko mtaani ni suala la wewe kutulia tu. Amini yupo mwingine
ambaye atayafanya maisha yako yawe ya furaha.
Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba,
unapotokea kumpenda mtu fulani, pambana kuhakikisha unampata kwa sababu
ukimkosa maisha yako yanaweza kuwa gizani. Ila pale utakapoona uwezekano
wa kuwa naye haupo, usilazimishe ndugu yangu. Kumbuka haya ni maisha
tu!
.............................................................................
Kwa nini mapenzi yakupe huzuni kila siku?
Jumamosi iliyopita, nikiwa
katika pilikapilika za kila siku, nilipokea simu kutoka kwa mtu
aliyejitambulisha kwa jina moja la Nancy. Kwa jinsi sauti yake
ilivyokuwa ikisikika, ilionesha dhahiri kwamba analia, nikashangaa kwa
nini analia na kinachomliza ni nini?
Aliomba kukutana na mimi siku hiyohiyo
akieleza kwamba ana matatizo mazito na anahitaji ushauri kutoka kwangu.
Japokuwa nilimweleza kwamba siku hiyo nilikuwa na ratiba ngumu tupange
siku nyingine, aliendelea kusisitiza huku akilia, nikawa sina cha
kufanya zaidi ya kukubali ombi lake.
Saa nane za mchana, tayari nilikuwa
nikitazamana uso kwa uso na Nancy, alionesha kuwa binti mzuri, mpole na
anayejitambua lakini bado alikuwa analia. Macho yake yalikuwa yamevimba,
uso wote ulibadilika na kuwa mwekundu, maskini! Alitia huruma.
Haikuwa kazi nyepesi kumtuliza, hatimaye nilifanikiwa kumfanya atulie
kwa sababu asingeweza kunieleza
kinachomsumbua kama angeendelea kuwa kwenye hali ile. Baada ya kutulia,
nancy alinieleza kilichomtokea na kusababisha awe kwenye hali hiyo.
Alichonieleza ndiyo hasa kimenifanya leo nije na mada hii kwa sababu
naamini wapo wengi wanaoteseka kama Nancy, pengine hata zaidi lakini
hawana pa’ kusemea.
Alinieleza mambo mengi lakini kwa
kifupi, alikuwa kwenye matatizo makubwa na mpenzi wake ambaye aliniomba
nisimtaje jina, waliyedumu naye kwa zaidi ya miaka mitatu kwenye
uhusiano wao.
Nilichojifunza kutoka kwa msichana huyo
ni kwamba alikuwa na huzuni kubwa ndani ya moyo wake, kila kitu
kilipoteza maana, alichokuwa anatamani kwa muda huo, ilikuwa ni
kuyakatisha maisha yake ili akapumzike! Uwezo wa moyo wake kuhimili
mateso ulikuwa umefikia mwisho na alichoona kinafaa ilikuwa ni
kuyakatisha maisha yake.
Alinieleza kwamba kwa kipindi chote
alichoishi na mwenzi wake, furaha ilikuwa kitu adimu sana maishani
mwake, akanihakikishia kwamba hata mwili wake ulikuwa umepungua sana kwa
sababu hakuwa akila vizuri wala kupumzika, chanzo cha yote ikiwa ni
mapenzi! Bila mwenyewe kujijua, matatizo ya kimapenzi yalikuwa
yamemuingiza kwenye huzuni kali ambayo kitaalamu huitwa Depression.
Kwa wanaoelewa kuhusu Depression,
wengine huita msongo wa mawazo ingawa siyo tafsiri yake sahihi,
watakubaliana na mimi kwamba unapokukumba, unaweza kuugua maradhi ambayo
hospitali vipimo vyote vitashindwa kuonesha unaumwa nini.
Kabla ya kuendelea mbele, ningependa
kila mmoja ajichunguze kwa makini kwenye maisha yake ya kila siku, ya
kawaida na yale ya kimapenzi.
Je, muda mwingi unajihisi kuwa na huzuni
moyoni mwako? Unahisi unatamani kulia hata bila sababu? Unahisi mwili
wako uko tupu na huna matumaini kabisa kuhusu kesho?
Kuna muda unakasirika sana hata kwa
sababu ndogo? Unahisi kichwa kuchanganyikiwa? Unahisi kila kitu
kinakukera hata vile ambavyo awali vilikuwa vikikufurahisha? Kama
ulikuwa unapenda kusikiliza muziki, kutazama tamthiliya au vipindi
fulani kwenye runinga, hutaki tena?
Usiku hupati usingizi vizuri kama zamani, muda wote unahisi mwili umechoka, unajihisi kuwa na hatia na muda wote unajilaumu?
Kama jibu ni ndiyo, basi tambua kwamba
na wewe ni miongoni mwa watu wanaosumbuliwa na huzuni kali ‘Depression’.
Hata hivyo, japokuwa wengi hawajui, migogoro ya mara kwa mara ya
kimapenzi, kuishi na mpenzi asiye mwaminifu, anayekushusha hadhi na
kukudhalilisha kwa namna mbalimbali na anayeutesa moyo wako ni chanzo
kikubwa sana cha Depression.
Kibaya zaidi, wengi huwa hawajui kwamba
wanasumbuliwa na tatizo hilo ndiyo maana matukio ya watu kujiua, kuwaua
au kuwajeruhi wengine, kusababisha madhara makubwa kwenye jamii au
kuugua maradhi yasiyopona, yanazidi kuongezeka kila kukicha.
Swali ambalo nataka msomaji wangu ujiulize, kwa nini kila siku mapenzi yakusababishie huzuni na matatizo?
Kwa leo nafasi haitoshi, wiki ijayo
nitaendelea kukusimulia kisa cha dada Nancy na kukupa mbinu za namna ya
kuondokana na huzuni inayosababishwa na mapenzi ili hatimaye na wewe
uyafurahie mapenzi kama wanavyoyafurahia wengine.
Tukutane wiki ijayo.
.............................................................................
Shoga: tui la nazi lazima lionjwe!
SHOGA
yangu u hali gani? Ni siku nyingine tena tulivu imefika na
tumekutana kwenye kona yetu hii inayowaelimisha wengi hususan wanawake
wenzangu japo wanaume nao siwaachi nyuma. Natumai na wewe ni mzima wa
afya na kama mgonjwa nakuombea kwa Mwenyezi Mungu atakutia nguvu.
Baada ya hayo tugeukie basi kwenye hiki
kilichonifanya niwaandikie, si mnakumbuka mara ya mwisho nilitoa somo la
chakula cha usiku hakifunikiwi!
Wengi mlinipigia simu na kunitumia
meseji jinsi mnavyowafanyia waume zenu. Inanipa raha sana kuona mada
imewaingia kisawasawa na kuyafanyia kazi shoga, mwanamke sharti ujue
kukipika chakula bwana!
Kiwe kitamu pia usimfunikie mume wako eti kwa kuhofia nzi au kupoa, kifunue ili akila ajihisi ameridhika, upo?
Shoga baada ya hayo, nimepata maswali
mengine mengi kutoka kwa nyie wasomaji wangu wengi mnaniuliza hivi tui
la nazi lina utamu gani? Wengine mnauliza kwani lazima lionjwe? Jamani
hata hili kweli la kuuliza au la kujiongeza mwenyewe? Umeshaandaa mboga
yako, nazi ukune mwenyewe, machicha ukamue mwenyewe eti kuonja unataka
usaidiwe. Tui la nazi sharti lionjwe shoga, usiwe zoba utaibiwa mjini,
ahii!
Wengine wanaishia kuonja machicha tu,
wanashindwa kumalizia kupata utamu wa tui lenyewe, wanashindwa kujua
hata tui la kwanza na la pili lipi tamu. Nikupashe tu shoga, wanaume wa
sasa ni wa kimjinimjini, wakizunguzungu tena wengine wakichinachina!
Chunga sana siku hizi kwani wanawake
wengine wanaweza kumnasa mwandani wako na wakamuandalia tui, balaa
itakuja kama tui hilo litakuwa zito kuliko unalopika wewe, mume akiona
hilo ni tamu anaweza kukuhama. Wengi wazembe wamewahi kukimbiwa na waume
au wapenzi wao kutokana na kupika tui jepesi na kutokuwa na ladha!
Unapoandaa tui la nazi yako jitahidi
liwe nzito na likolee kwelikweli na hata mume au mpenzi wako anapokuja
kula basi asiione lina matatizo au jepesi, mfanye awe analitamani kila
siku kwani usipofanya hivyo na wenzako nje wakamtengenezea na akakosea
kulila, ndiyo mwanzo wa kuhama kwenye jiko lako.
Uzuri wa mwanamke siyo sura tu bali hata
katika mapishi kwenye jiko lenye kiwanja cha sita kwa sita. Ukiwa
jikoni humo jitahidi kupika mboga, ukiamini kwamba ukitia tui, mumeo au
mchumba wako hatabanduka na kwenda kutafuta chakula sehemu nyingine.
Tumewahi kushuhudia wanawake wengi wakilalamika kuchukuliwa kwa waume
wao au wapenzi wao au wachumba wao na wanawake wengine kisa ni jinsi
wanavyowatayarishia tui na kila wakila wanaona ni hovyo tu.
Ubaya ni kwamba siku hizi wasichana
wengi hawafundwi kama zamani ambapo walikuwa wakikusanyika wanawake watu
wazima na kuwafundisha wasichana jinsi ya kutengeneza tui zito
litakalomfanya mume asihangaike na mboga za nje.
Siku hizi wasichana wanaona mambo hayo
kuwa ni ya kizamani na wala hawana haja ya kufuatilia kwa wanawake
waliowapita umri ambao wameona mengi, hivyo kubaki kuharibu tui na
kutotamanika. Ukiwa wa bush kwenye miti mikavu na vichaka unaachwa, sasa
kwa nini usijifunze hata kwa kuibia kwa wenzako?
Shoga, acha nikupe kaubuyu kadogo!
Wenzako wakipewa jembe kabla hawajaingia shambani wanaangalia kwanza
kama wataweza kulilimia, halijaharibika!
Wanalichukuwa na kuingia shambani,
wakimaliza kulima wanachukuwa nazi na kuanza kukuna, wanahakikisha
wanapata machicha ya kutosha, wanakamua hadi tui lile zito walione
likitoka! Wakionja huo utamu wake, mwanaume hatoki! Kwanza akafuate nini
huko nje?
Uzuri wa siku hizi tui la nazi hata
ukilila kwa chakula cha usiku tamu, chakula cha mchana tamu. Ukilila
kipindi cha baridi tamu, kipindi cha joto tamu. Ukilila kwa kufunika
chakula tamu, ukikifunua napo tamu.
Ukilila kwa kuimba nyimbo zote tamu, iwe Mchiriku au Taarab linakuwa tamu.
Shoga najua umenipata, basi yafanyie kazi niliyokuambia ili ndoa yako idumu.
Kwa leo sina mengi tuonane wiki ijayo! Kwa ushauri, nitumie meseji tu kwa namba yangu hapo juu nitajibu.
..................................................................................................
HAYA NDIO MADHARA YA KUNYONYA UKE WAKATI WA KUFANYA MAPENZI.... NA PIA WATAMBUE WANAWAKE MATAPELI KATIKA MAPENZI... KAMA WEWE NI MWANAUME HAKIKISHA UMESOMA
Kwanza kwa nini wasichana wengi mmekuwa matapeli wa mapenzi?
Utakuta msichana hajampenda jamaa lakini anataka pesa tu na anapretend
kama amekufa ameoza hii inajidhihirisha pale mnapokuwa kunako sita kwa
sita utaona msichana anapiga kelele za hatari mnaweza kuwa mpo Mwenge
lakini watu wa mbagala wanazisikia kelele hizo…. Kwa mwanaume asiejua
mambo anaweza kuhisi ndo amemtoa bikira mdada huyo kumbe wapi ni wizi
mtupu….mtoto anatengeneza tu mazingira ya kukutoa pesa… mkimaliza ukimpa
elfu 5 ya nauli anakwambia beib hela gani hii hivi hujaona jinsi
ulivoniumiza jamani nipe hata elfu 30 basi…. Kweli mapenzi kamari
Nanyi wanaume
waogopeni sana wasichana wenye tabia kama hizo maana hawana mapenzi ila
wapo kimaslahi zaidi!!!! Na pia watoto wa kiume epukeni kujitafutia
magonjwa makubwa kwa kuwanyonya hawa wasichana sehemu zao za siri
…. Usiige yale unayoyaona kwenye mikanda ya ngono ukahisi ni jambo zuri, kumbuka wale wanaoigiza mikanda ya xxx wapo kibiashara zaidi na sio kimapenzi……
…. Usiige yale unayoyaona kwenye mikanda ya ngono ukahisi ni jambo zuri, kumbuka wale wanaoigiza mikanda ya xxx wapo kibiashara zaidi na sio kimapenzi……
Kwanza hebu tafakari mambo matatu yafuatayo…..
1. wanawake wanaenda
breed kila mwezi…. Ila damu huwa ni chafu sana ndio maana hairuhusiwi
kulala nae wewe unapata wapi ujasiri wa kumnyonya!!!!
2.
Wanawake wengi wanatumia vipodozi na madawa mengi yenye athari wewe
unajiweka kundi gani kwa kuyalamba na kuyameza hivi unayapenda kweli
maisha yako na wanaokutegemea
3. Inawezekana
mwanamke huyo ndo mara yako ya kwanza kukutana nae hujui aliwahi kuwa na
nani huko nyuma wewe unakurupuka tuu na kutaka kuonesha ufundi wako…..
huenda alikuwa na jamaa mwenye magonjwa ya ngozi kama ukurutu,
malengelenge, fangasi na mengineyo….fikiria mara tatu kabla ya kuyaweka
rehani maisha yako kwa mambo ya kijinga!!!!
NJIA MBADALA NA NZURI NA PENZI LITAKUWA TAMU
Tumia njia zingine
kama kupapasana, kutekenyana sehemu mbalimbali kwa kucha na vidole … Na
pale muwapo ndani ya sita kwa sita msisitize mpenzi wako kukata viuno
taratibu ila kwa ufundi, mtekenye masikio yake taratibu kwa kucha
zako….. mtazame kimahaba, mtekenye na mpapase chini ya kitovu hadi
kwenye nywele za ikulu yake…. Usisugue haraka haraka kama unakimbizwa
fanya taratibu ila kwa ufundi……. Kwa hujui ufundi upoje usione aibu
nitumie sms inbox hapo na nitakusaidia……
Je, unapenda kesho niendelee na madhara ya kiss na kunyonya uume?
..............................................................................................................................
Mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius aliyekuwa nakabiliwa na
shtaka la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp leo amesomewa hukumu ya
kesi hiyo nchini Afrika Kusini.
Pistorius amehukumiwa kifungo cha miaka 6 gerezani kwa kukutwa nahatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi.
Pistorius alitenda kosa hilo Februari 13, 2013 ikiwa ni usiku wa kuamkia siku ya Valentine Day na inaelezwa alimpiga mpenzi wake risasi kwa madai alidhani ni mwizi aliyekuwa amejificha bafuni.
Pistorius amehukumiwa kifungo cha miaka 6 gerezani kwa kukutwa nahatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi.
Pistorius alitenda kosa hilo Februari 13, 2013 ikiwa ni usiku wa kuamkia siku ya Valentine Day na inaelezwa alimpiga mpenzi wake risasi kwa madai alidhani ni mwizi aliyekuwa amejificha bafuni.
Comments
Post a Comment