Tende, Maji Zinavyofaa Wakati wa Mfungo wa Ramadhani
V YAKULA vinavyofaa kuliwa wakati huu wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni vingi, leo tutaanza kuchambua kimoja baada ya kingine, Mbali na Waislamu, uchambuzi huu unawafaa pia wale ambao siyo Waislamu. Chakula kilichozoeleka zaidi kwa futari ni tende. Baada ya kushinda kutwa nzima na Swaumu, kiwango cha sukari ya mwili hupungua na hivyo, kuhitaji kujazilizwa tena. Aina ya kwanza ya sukari itumikayo mwilini na hasahasa ubongoni ni glukosi. Mshuko wa sukari walioupata wale ambao hawakula au kunywa kwa kipindi kirefu, unaweza kusababisha ulegevu wa mwili. Pindi sukari inapoliwa kwa njia ya chakula au kinywaji, viwango vya glukosi ya mwili hujisawazisha vyenyewe na kumfanya mtu aliyefunga asijihisi kuchoka sana na huwa na nuru zaidi ya macho. Ingawaje tende, mara nyingi, si chakula kinachopendelewa sana na watu wenye njaa, lakini ndicho chakula kisicho na mafuta, na ni chanzo madhubuti cha sukari. Nusu ya sukari zitolewazo na tende ni kwa aj...