Rais Uhuru Kenyatta Aruhusu Maandamano ya Wanaopinga Ushindi Wake
Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake, William Ruto. Rais Uhuru Kenyatta huenda akaingia katika vitabu vya kumbukumbu na historia kwa marais wa Afrika kwa kuamua kuruhusu maandamano ya amani kupinga ushindi wake alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8. Kenyatta amewataka polisi kujizuia kutumia nguvu kubwa na badala yake wawape ulinzi wakati wa maandamano hayo ya amani na yanayoruhusiwa kisheria kwa watu ambao hawafurahii matokeo ya uchaguzi uliopita. Rais Kenyatta alisema hayo jana alipokuwa akitoa ujumbe kwa wagombea walioshindwa katika uchaguzi huo uliofanyika Jumanne iliyopita. Kenyatta alisema hayo akiwa Jengo la Harambee alikokwenda kukutana na Kamati ya Maandalizi ya Hafla ya kuapishwa kwake. Katika ujumbe huo uliomlenga zaidi Raila Odinga aliyekuwa mgombea urais kupitia muungano wa Nasa, Kenyatta aliwataka wagombea wote ambao hawakuridhishwa na matokeo ya uchaguzi wachukue hatua zilizobainishwa na Katiba ili kupata wanachotaka. “Marafiki