SIMBA SC YAWAONYA YANGA KWA KUANZA UJENZI WA UWANJA BUNJU, ZANA ZATUA RASMI!
Hivi ndivyo mambo yalivyo huko Bunju. Picha hii ni kwa hisani ya Blog ya Bin Zubeiry. Na Baraka Mpenja, Dar es salaam WAKATI mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Simba unaotarajia kufanyika juni 29 mwaka huu ukizidi kushika kasi hasa baada ya mgombea aliyeenguliwa kuwania Urais Michael Richard Wambura kurejeshwa, taarifa njema kwa mashabiki wa klabu hiyo ni kwamba mkakati wa ujenzi wa uwanja umechukua sura mpya leo hii. Mtandao huu unafanya jitihada za kuwatafuta viongozi wa Simba ili kujua zoezi hilo linaendeleaje huko Bunju. Hata hivyo, Msemaji wa Simba sc, Asha Muhaji ameuambia mtandao huu kuwa hajapewa taarifa rasmi na uongozi kuhusu zoezi hilo. Muhaji amesema linapotokea jambo katika klabu hiyo anapewa taarifa, hivyo ameahidi kufikia baadaye atakuwa na taarifa zaidi. “Mimi bado sijapewa taarifa kamili, labda tuwasiliane baadaye ili tujue”. Amesema Muhaji. Uongozi wa Simba amepeleka magari yanayomwaga vifaa na kusafisha eneo la uwanja wao ...