Posts

Showing posts from November 13, 2016

Fanya hivi ili kuweka mvuto wa maandishi kwenye WhatsAppYako.

Image
WATU wengi husumbuka sana wanapoandika ujumbe kwenye mtandao wa WhatsApp kutokana na hali kwamba herufi huwa na uzito sawa wa rangi katika hali ya kawaida, aidha, mtindo wake huwa mmoja. Je, wajua unaweza kukoleza rangi ya herufi na kuzifanya nzito (bold), ukaziweka kwa mlazo (italiki) na pia ukaweka mstari unaozikata herufi kati, kwa Kiingereza strikethrough? Unachohitaji kufanya kwanza kabisa ni kuwa na toleo la karibuni zaidi la app ya WhatsApp kwenye simu yako. Kuweka bold Ili kukoza rangi kwenye herufi (kufanya bold), unahitajika kutanguliza neno lako na alama ya nyota na kisha kuhitimisha na alama ya hiyo hiyo nyota. Kwa mfano, ukiandika *bold* itatokea ikiwa bold Kuweka italiki Ili kufanya herufi zako kuwa za mlazo au kuwa za italiki, unahitajika kutanguliza na mstari sakafu (underscore) na kuhitimisha na alama iyo hiyo. Ukiandika _italics_ itatokea ikiwa italics Kuweka strikethrough Ukitaka kuweka alama ya kukata kati kwenye herufi zako, u

Hii ndiyo familia ya Donald Trump

Image
Barron Trump Ndiye mwana wa pekee wa Rais mteule wa Marekani, Donald Trump na mke wake wa sasa, Melania. Ingawa alijitokeza katika mikutano kadha ya kampeni, kijana huyo wa miaka 10 hakuwa akionyeshwa mara kwa mara hadharani. Anapendelea kucheza gofu na baba yake, pia ana uwezo mkubwa wa kuzungumza Kislovenia kwa ufasaha. Melania Trump Ni mwanamitindo wa zamani, mzaliwa wa Slovenia, aliolewa na Donald Trump Januari 2005. Alijitokeza na kumtetea mumewe, baada ya kanda ya video kutolewa wakati wa kampeni na kumuonesha akijitapa kuhusu kuwadhalilisha kimapenzi wanawake. Julai 2016, aligonga vichwa vya habari baada ya kutoa hotuba katika mkutano mkuu wa kitaifa wa chama cha Republican, baada ya Trump kuidhinishwa kuwania urais, ambapo alituhumiwa kuchukua maneno mengi kutoka katika hotuba iliyotolewa na Michelle Obama mwaka 2008. Alipoulizwa na CNN Oktoba ni jambo gani angetaka kubadilisha kwa mumewe, alijibu: “Kuandika

Clinton Aitupia Lawama FBI kwa Kushindwa Urais

Image
Aliyekuwa mgombea urais nchini Marekani kupitia Chama cha Democratic, Hillary Clinton, amesema kushindwa kwake ghafla katika uchaguzi uliopita, kulichangiwa sana na hatua ya Mkurugenzi wa Shirika la Kijesusi la Marekani FBI, James Comey kutangaza uchunguzi mpya wa sakata la barua pepe dhidi yake siku chache kabla ya uchaguzi kufanyika. Bi. Clinton aliyepata kura za wajumbe 228 huku mpinzani wake Donald Trump akishinda kwa kura za wajumbe 290 amewaambia wafadhili wa chama chake kuwa hatua ya Comey ilisambaratisha kampeini zake licha ya uchunguzi huo kutomkuta na hatia.

KUTANA NA MWANAMKE WA AJABU,ANAZUNGUSHA MWILI KAMA KAMBA,ANAKULA KWA MIGUU,ANATEMBEA KWA MIKONO

Image
 Kwa jina unaweza muita Leilani Franco(Backbend)  ana uraia wa nchi mbili (Uingereza / Philippines) alisafiri katika nafasi umbali wa 20m  katika muda wadk  10.05  katika  tamasha la Royal Hall mjini London Uingereza, tarehe 11 Machi 2013.   Backbend binadamu ambaye ana uwezo wa kutembealea mikono na miguu kwa umbali mrefu.  Pia kama inavyodhaniwa kwa kawaida Mtu anaweza tumia mikono kwa kulia chakula na kufanya shughuli nyingine,  lakini kwa mwanamke huyu imekuwa ni tofauti kabisa, Mwanamke huyu ana uwezo wa kutumia miguu yake  katika shughuli zake binafsi kama Kula na kadhalika.....  Hatimaye, Leilani pia anashikilia rekodi ya Dunia kutokana na uwezo wake katika kuuzungusha  Mwili wake.

MZ Yakanusha Taarifa za Kifo cha Balozi Omar Ramadhan Mapuri

Image
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inapenda kukanusha taarifa kutoka kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Balozi Omar Ramadhan Mapuri (pichani) amefariki dunia. Taarifa rasmi ya serikali ni kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata chembe ya ukweli, Kamishna Balozi Mapuri yupo hai na afya yake iko vizuri. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokwenda kumjulia hali Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mh. Omar Ramadhan Mapuri katika Hospitali ya Rufaa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.  Mheshimiwa Balozi Omar Ramadhan Mapuri ambaye kwa sasa ni Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipata matibabu na baada ya kupata huduma kutoka kwa madaktari, Mheshimiwa Balozi Mapuri aliruhusiwa kurejea nyumbani siku ya Jumamosi Novemba 12 baada ya afya yake kuimarika. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed