Posts

Showing posts from September 5, 2017

Hashim Rungwe Ashikiliwa na Polisi Dar

Image
Hashim Rungwe Spunda. ALIYEKUWA mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Hashim Rungwe Spunda anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa siku nne sasa. Rungwe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chaumma) anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam akituhumiwa kughushi nyaraka. Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema leo Septemba 5 kuwa, Rungwe anashikiliwa kituoni hapo kwa siku nne. Hata hivyo, Kamanda Mambosasa hakutaka kuingia kwa undani kuhusu suala hilo akisema hana taarifa za kutosha.

DENTI ACHARANGA WATU VISU MTAANI!

Image
Paulo Ndensai akiuguza majeraha. MWANAFUNZI wa kidato cha pili katika shule moja ya sekondari Wilaya ya Kinondoni jijini, Samuel Wilson, Jumanne iliyopita, saa mbili usiku, alifunga mtaa maeneo ya Mwenge Mlalakuwa na kuwachoma visu watu kadhaa akiwemo Paulo Ndensai na Yasin Mohammed. Akisimulia kwa uchungu tukio hilo mmoja wa mashuhuda alisema mwanafunzi huyo alikuwa akimpiga kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Mohammed huku akimchoma kwa kisu alichoshika hali iliyowafanya wananchi waliokusanyika eneo hilo kukimbia kwa kuhofia usalama wao. Shuhuda huyo alisema denti huyo akiendelea kumshambulia Mohammed ambapo chanzo cha ugomvi huo hakijawekwa bayana, kaka yake Mohammed aitwae Paulo Ndensai alitokea na kwenda kumuokoa mdogo wake. “Katika harakati za kumuokoa mdogo wake, mtuhumiwa alimuacha aliyekuwa akimshambulia na kuhamishia varangati kwa kaka mtu ambapo alimchoma kwa kisu kichwani juu kidogo ya sikio la kushoto, kingine akamchoma kichwani juu, hali...

RAILA ODINGA AMWITA KIBA KENYA, ATUMIWA NDEGE BINAFSI

Image
Alikiba. DAR ES SALAAM: Upepo mwanana bado unaendelea kumpuliza, staa namba moja wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ baada ya mgombea anayewakilisha Muungano wa Vyama vya Upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Omolo Odinga, kudaiwa kumuita nchini humo. Kwa mujibu wa chanzo kisicho na chembe ya shaka, Kiba anayesumbua kwa sasa na wimbo wake wa Seduce Me, alipata mwaliko huo mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni saa chache mara baada ya Odinga kushinda kesi ya uchaguzi Katika Mahakama ya Juu aliyokuwa amemfungulia Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ambaye mambo yalimuwia mazito. Kenyatta alitangazwa mshindi wa nafasi ya urais na Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IBEC) katika uchaguzi uliofanyika nchini humo Agosti 8, mwaka huu ambapo Odinga alifungua kesi hiyo mahakamani. Baada ya mahakama kupitia hoja za pande zote, iliufuta uchaguzi huo kwa kueleza kuwa tume ya uchaguzi haikuzingatia uadilifu. ODINGA KICHEKO Mara baada ya hukumu hiyo kutolewa mahakaman...

BREAKING: Wabunge wa Upinzani watoka nje ya Bunge

Image
Wabunge wa Ukawa wasusia na kutoka nje shughuli ya kuapishwa kwa wabunge wa viti maalum 7 wa CUF. Wabunge hao ni wale waliopatikana baada ya Mwenyekiti wa Chama hicho Prof Lipumba kutangaza kuwavua uanachama Wabunge 8 wa chama waliokuwepo kwasababu mbalimbali ikiwemo ya maadili.

RIPOTI YA MAKINIKIA ALMASI, TANZANITE BUNGENI KESHO

Image
             WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, kesho anatarajiwa kukabidhiwa taarifa za kamati mbili zilizoundwa na Bunge katika Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 kuhusu na makinikia ya almasi na biashara ya madini ya tanzanite. Kwa mujibu wa taarifa za bunge hafla fupi ya makabidhiano hayo itafanyika katika viwanja vya bunge na viongozi wa kitaifa watakuwepo. Kabla ya Waziri Mkuu kukabidhiwa taarifa hizo, kamati hizo mbili zitakabidhi taarifa zake kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye naye atakabidhi kwa Waziri Mkuu. Taarifa hizo mbili zinazosubiriwa kwa makini hasa baada ya taarifa za kamati zilizoundwa na Rais John Magufuli kuibua makubwa katika makinikia kwenye makontena bandarini. Kamati hizo maalumu zote zilikuwa na idadi sawa ya wabunge ambao ni tisa na zililenga kushauri juu ya mfumo bora wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa biashara ya madini ya almasi na Tanzanite hapa nchini. Kamati iliyohusu almasi ikiongozwa na Mweny...