Posts

Showing posts from June 17, 2017

Serikali ya China kujenga shule ya usafirishaji nchini

Image
Dar es Salaam. Serikali ya China imesema kuwa ipo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania ya kujenga shule ya usafirishaji hapa nchini. Akizungumza leo (Jumamosi) katika hafla ya kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini iliyoandaliwa na taasisi ya Confucius, Balozi wa China nchini, Dk Lu Youging amesema wakimaliza mazungumzo hayo wataanza ujenzi mara moja. Amesema lengo la ujenzi wa shule hiyo ni kuwaongezea ujuzi wahitimu na wale wasiokuwa wahitimu wa vyuo vikuu. Amesema kwa mujibu wa ripoti ya uwekezaji wa China hapa nchini ni kiasi cha dola bilioni saba huku kampuni zaidi ya 1,000 zikifanya shughuli zake na kutoa ajira 1,200 kwa Watanzania. Kwa upande wake, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo amezipongeza kampuni za China kwa kuisaidia Serikali kupambana na changamoto ya ukosefu wa ajira. “Wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini wasiichukulie fursa hii kimzaha bali waifanyie kazi kuhakikisha wanakuwa na weledi ...

OKWI RASMI SIMBA, KUZIBA NAFASI YA AJIBU.

Image
Wakati mshambuliaji Ibrahim Ajib akiwa anaelekea Jangwani, klabu ya Simba inaonekana kutokuwa na shida juu ya hilo kwasababu tayari ipo njiani kumvalisha Emannuel Okwi Jezi 25 msimu ujao. Okwi ambaye ameshaitumikia Simba kwa vipindi viwili tofauti, ametua Bongo jana usiku na leo mchana nilipata nafasi ya kuzungumza na amethibitisha kwamba yupo katika mazungumzo ya mwisho ya kujiunga na Simba. “Ni kweli nipo kwenye mazungumzo ya mwisho na Simba, naamini tutakubaliana kila jambo na nitasaini kuichezea tena Simba.” – alisema Okwi. Source: Shaffihdauda

MSANII ESTER APANGIWA MJENGO NA MWANAUME

Image
MSANII  wa filamu za Kibongo, Ester Kiama anadaiwa kupangishiwa mjengo na mwanaume ambaye ni mume wa mtu aliyemhamisha ku­toka Kijitonyama alikokuwa anaishi na kumwamishia Mbezi Beach. Chanzo makini kilieleza kuwa kwa sasa Ester anaishi kwenye nyumba nzima yenye hadhi tofauti na alikokuwa akiishi mwanzo ambapo amelipiwa kodi ya mwaka mzima na mwanaume huyo. Risasi Jumamosi  lilimtafuta Ester ili kujibu tuhuma hizo na alipopatikana alikiri kuhamia Mbezi Beach kwenye nyumba ny­ingine nzima lakini ali­pinga suala la kupang­ishiwa na mwanaume. “Ninaishi Mbezi Beach kwa sasa amba­ko nimehamia hivi kari­buni, habari za kwamba nimelipiwa kodi na mwanaume ni uongo, nimejilipia mwenyewe,” alisema Ester.

Serikali kujenga Ikulu ndogo makao makuu ya mkoa Songwe.

Image
Serikali imetoa shilingi billion 4.7 kwa wakala wa majengo nchini tba ili kuanza rasmi ujenzi wa ikulu ndogo na ofisi za makao makuu ya mkoa wa songwe mradi unaoanza mara moja baada ya wananchi kujitolea eneo lenye ukubwa wa hekari 40 zilizopo katika mlima nselewa kata ya mlowo wilayani mbozi. Mkoa wa songwe una zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu kuanzishwa kwake lakini kwa kipindi chote hicho viongozi wa ngazi ya mkoa akiwemo mkuu wa mkoa wamekuwa wakifanya kazi kwa kujibana kutokana na kutokuwa na ofisi hali ambayo bi chiku galawa mkuu wa mkoa songwe amesema ilikuwa haitoi nafasi nzuri katika utendaji kazi ulio bora. Aidha bi galawa amesema ujenzi huo utatosheleza kupatikana kwa ofisi za idara mbalimbali ngazi ya mkoa, nyumba ya mkuu wa mkoa na katibu tawala wake pamoja na ikulu ndogo na kwamba eneo hilo halina fidia kwa wananchi. Mtendaji mkuu wa wakala wa majengo tba elius  mwakalinga amesema bajeti ya mradi ni sh. Billion 4.7, ambapo awamu ya kwanza itatum...

Rais Baldwin Lonsdale afariki ghafla kufuatia mshutuko wa moyo

Image
Rais wa Vanuatu Baldwin Lonsdale amefariki kutokana na mshutuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 67. Bwana Lonsdale, ambaye ni kasisi wa kianglikana, amekuwa kiongozi wa kisiwa hicho cha Pacific tangu Septemba mwaka 2014. Gazeti la Daily Post nchini Vanuatu, lilisema kuwa alifariki ghafla kwenye mji mkuu Port Vila, muda mfupi baada ya usiku wa maane siku ya Jumamosi. Akiwa rais Bwana Lonsdale aliongoza ujenzi mpya wa maeneo ya kisiwa hicho kufuatia uharibifu uliosababishwa na kimbunga Pam, kilichosababisha watu 75,000 kukosa makao mwezi Machi mwaka 2015. Mwezi Oktoba mwaka huo huo aliapa kupambana na ufisadi nchini Vanuatu, baada ya sakata iliyomhusisha makamu wake. Makamu wake alijiondolea mashtaka pamoja na wabunge wengine 13 wakati Bwana Lonsdale alikuwa nje ya nchi, hatua ambayo aliifuta wakati alirejea nchini.

Ishu ya Mchele wa Plastiki Bongo, Kiwanda Kinachodaiwa Kutengeneza Chavamiwa

Image
D AR ES SALAAM: Katika wiki za hivi karibuni, kumekuwa na uvumi una­osambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, juu ya kuwepo kwa mchele wa plastiki, unaodaiwa kuingizwa nchini na wafanyabiashara wasio waaminifu, unaouzwa katika vibanda vya akina mama n’tilie.   Kinu chenye malighafi ya kutengeneza plastiki hizo. Baada ya uvumi huo kuleta hofu kubwa kwa wananchi, hasa kufuatia video mitandaoni kuonyesha wali uli­opikwa ukiliwa na hata kiwanda kina­chodaiwa kuwepo nchini kinachoten­geneza mchele huo, Risasi Jumamosi liliamua kuufanyia kazi uvumi huo ili kujua mbivu na mbichi ya sakata hilo. Malighafi zinazotumika kutengeneza plastiki hizo hapo kiwandani. Risasi Jumamosi liliambiwa kuwa mchele huo unauzwa katika baadhi ya masoko ya jijini Dar es Salaam yakita­jwa kuwa ni pamoja na yale ya Bugu­runi, Mwananyamala, Makumbusho na Afrikasana. Kikosi kazi kilisambazwa katika masoko hayo na kufanya uchunguzi wake ikiwa ni pamoja na kuzungumza na baadhi y...