Posts

Showing posts from September 20, 2017

Rais Magufuli Azindua Barabara Mererani Mkoa Wa Manyara Leo

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa kwa furaha na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera alipowasili kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia maelfu ya wananchi alipowasili Mererani kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa Mererani wakati wa kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe M

Miili ya Ndugu 13 Waliofariki kwa Ajali Uganda Ilivyoagwa Dar (Pichaz)

Image
Wanajeshi wa JWTZ wakibeba miili ya marehemu hao kupeleka eneo maalum kwa ajili ya kuaga. SIMANZI, vivlio na majozni imetawala wakati wa kuaga miili ya Watanzania 13 ambao ni ndugu wa familia moja waliofariki kwenye ajali mbaya ya gari iliyotokea nchini Uganda hivi karibuni. Waziri Angella Kairuki akiteta jambo na Betty Kamya ambaye ni mwakilishi wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni. Miili ya wanafamilia hao imeagwa leo Septemba 20, 2017 katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi ya Lugalo jijini Dar es Salaam na baadaye kusafirishwa kuelekea Arusha, Kilimanjaro na Mpwapwa kwa ajili ya mazishi. Waombolezaji wakati wa shughuli ya kuaga marehemu. Katika ibada hiyo ya kuwaaga marehemu, viongozi mbalimbali wa serikali walikuwepo wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala), Angela Kairuki, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles John Mwijage, Waziri Maalum wa Kusimamia Jiji la Kampala, Betty Kamya kutoka Uganda aliyemwakilisha Rais wa nch

Serikali Yatangaza Nafasi za Ajira kwa Walimu wa Shule za Msingi

Image

RAIS MAGUFULI ALIAGIZA JESHI LA WANANCHI KUJENGA UKUTA ENEO LA TANZANITE

Image
              Rais John Magufuli. RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameliagiza Jeshi la Wananchi (JWTZ)kushirikiana na Suma JKT kujenga ukuta eneo lenye madini ya Tanzanite wilayani Simanjiro mkoani Manyara. Magufuli ametoa agizo hilo leo Jumatano, Septemba 20, 2017 akiwa ziarani mkoani Manyara alipowahutubia wananchi wa Simanjiro akizindua Barabara ya Lami kutoka Kia hadi Mererani. Nchi hii ni tajiri, tulipewa madini na Mungu ambayo hayapatikani nchi yoyote, lakini hayatusaidii sisi na tunapata shida. Kwa nini tupewe Tanzanite, tena Simanjiro pekee halafu wanachi wapate shida za maji na barabara? Kwa nini tuibiwe? Kwani Mungu alifanya makosa kutupa hayo madini? Haiwezekani, tuanze kubadilika sasa. “Tatizo letu sio vyama, bali ni vipi tunatumia rasilimali zetu. Tanzanite ingekuwa nchi nyingine, hapa pangekuwa kama Ulaya. Ipo siku Tanzanite haitakuwepo, tutaachiwa mashimo tu! Hakuna haja ya kumung’unya maneno, Tanzani