Posts

Showing posts from January 30, 2017

BREAKING NEWZZ:MWENYEKITI WA CCM MBEYA ANUSURIKA KUUAWA

Image
Mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini, Efrahim Mwaitenda mwenye umri wa miaka 60 amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mgongoni na mtu au watu wasiofahamika. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29.01.2017 majira ya saa 05:45 usiku katika kitongoji cha Ilopa, Kijiji cha Mahenge, Kata ya Makwale, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Amesema tukio hilo limetokea wakati akiwa amelala kitandani nyumbani kwake Ntembela ambapo mbinu iliyotumika ilikuwa ni  kukata wavu wa dirisha na kumjeruhi kwa kutumia silaha za kienyeji zinazotumia risasi za gololi. Mwenyekiti huyo amefikishwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na hali yake inaendelea vizuri. Lukula amewaambia waandishi wa habari kuwa nia ya shambulizi hilo ilikuwa ni kutaka kuumua na kwamba juhudi za kuwatafuta na kuwakamata wahusika zinaendelea

FARU FAUSTA WA NGORONGORO,ATIMIZA MIAKA 54 AISHI CHINI YA ULINZI WA KIJESHI

Image
Ndio faru mzee duniani,sasa haoni Ngorongoro yampa ulinzi wa kijeshi FARU Fausta ndio anayesadikiwa kuwa na umri mkubwa kuliko Faru wote duniani,mwaka huu amefikisha umri wa miaka 54.Faru Fausta yupo katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,lakini kutokana na uzee wake huo,sasa anakabiliwa na tatizo la macho la kutoona. Kufuatia hatua hiyo,uongozi wa Ngorongoro sasa umemuweka katika makazi maalum ndani ya hifadhi hiyo.Hatua ya mamlaka kuchukua hatua ya kumpa ulinzi maalum Faru Fausta inahofia kushambuliwa na wanyama wengine wakali na hususani fisi na Simba. Hivi sasa gharama inayotumika kumlinda Faru Fausta ni kubwa,hivyo uongozi wa Mamlaka umeishauri wizara kuchukua hatua juu ya Faru Fausta