Posts

Showing posts from October 14, 2017

Dida: Sijawahi Kuhongwa Chochote Na Mwanaume

Image
Khadija Shaibu ‘Dida’. MTANGAZAJI wa redio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amefunguka kuwa katika maisha yake hajawahi kuhongwa chochote na mwanaume, mafanikio yake utafutaji kwa sababu hapendi kupewa wala kujibweteka anapambana na ataendelea kupambana kwani anaamini mwanaume hawezi kumfanya awe na maendeleo. na kujikuta hawana thamani tena, jamani pambaneni mbona inawezekana wanawake kufanikiwa bila kuwatumia wanaume na miili yetu!” alisema Dida.

Nape Apigilia Msumari Kauli ya Msekwa Kuhusu Ukomo wa Madaraka kwa Rais

Image
Nape Nnauye. MBUNGE wa jimbo la Mtama, Mh Nape Nnauye amepigilia msumari kauli iliyotolewa na Spika wa zamani wa Bunge, Pius Msekwa kuhusu miaka ya uongozi na kusema misimamo hiyo ndiyo misimamo ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwalimu Julius Nyerere. Nape Nnauye ameweka video ya Pius Msekwa akielezea juu ya ukomo wa kiongozi madarakani na kusema chama hicho kilishafikiria miaka ya nyuma kuongeza miaka kutoka 10 na kuendelea lakini waliona miaka kumi inatosha kwa mtu kuongoza na kusisitiza ikiwa miaka 15 ikatokea mkapata kiongozi mbaya miaka hiyo itakuwa ni mingi sana. “Miaka 15 mkipata kiongozi mbaya ni mingi sana, nashauri ibaki miaka 10 kama kiongozi ni mbaya angalau tumvumilie kwa miaka 10 tu halafu basi ndivyo hoja ya miaka 10 ilivyopita si kama hiyo mingine hatukufikiri ilifikiriwa ndiyo maana naposikia kuna Mbunge mmoja anataka kupendekeza twende kwenye miaka saba kwa vipindi viwili ninataka kumjulisha kwamba hili si wazo jipya tulishafikiri na lilik