MAHAKAMA YAMSAKA PADRI ANAYEKABILIWA NA KESI YA KUMLAWITI MTOTO
Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, limeshindwa kusikiliza rufaa iliyokatwa na upande wa Jamhuri kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomwachia huru Padri wa Kanisa Katoliki, Sixtus Kimaro aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kumlawiti mtoto wa miaka 17. Rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa hivi karibuni lakini hata hivyo padri huyo pamoja na wakili wake hawakufika mahakamani. Upande wa Jamhuri una hoja saba katika rufani hiyo.Kabla ya kuachiwa huru baada ya kukata rufaa, Padri Kimaro alihukumiwa kifungo cha miaka 35 jela na kulipa faini ya Sh milioni mbili kwa mtoto baada ya kupatikana na hatia. Kutokana na kushindwa kwa jopo hilo kusikiliza rufani hiyo wiki iliyopita, kwa kutotokea mahakamani hapo padri huyo wala wakili wake, jopo limeagiza upande wa Jamhuri kutoa taarifa ya mwito kuwa anahitajika mahakamani hapo kupitia vyombo vya habari. Hatua ya kuamriwa kutumika vyombo vya habari kunatokana na wakili wa Serikali, Salum Malick kudai kuwa amep...