Posts

Showing posts from May 4, 2017

Faida za kutumia juisi ya miwa katika kuimarisha afya zetu

Image
Bila shaka unaifahamu juisi ya miwa, watu wengi tumekuwa tunakunywa na wengine tukiwa tunaibeza pia, hii ni kwasababu tumekuwa hatujui faida zitokanazo na unywaji wa huisi hiyo. Leo nataka nikupashe japo kwa uchacje faida za kunywa juisi ya miwa katika afya zetu. Kunafaida nyingi za juisi ya miwa. Baadhi ya faida hizo ni kama zifuatazo; 1. Juisi ya miwa inauwezo mkubwa wa kuipatia miili nguvu kwa haraka na kukata kiu ya maji.  Hii ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari "sucrose" ambayo kazi yake kuu ni kutengeneza nguvu mwilini. Kwahiyo wakati mwingine ukiwa na nguvu au uchovu, badala ya kunywa vinywaji vya viwandani tafuta juisi ya miwa. 2.  Husaidia figo kufanya kazi vizuri. Juisi ya miwa inasaidia kuongeza kiwango cha protein mwilini na ku-imarisha ufanyaji kazi wa figo. Juisi a miwa iliyochanganywa na maji ya Nazi husaidia kupunguza maumivu hasa yanayosababishwa  na mawe yaliyopo kwenye figo. 3. Hupunguza uwezrkano wa kupata ugonjwa wa kansa. Ju

MFAHAMU JOHN STEPHEN ,MTANZANIA MAARUFU ULIMWENGUNI KULIKO HAPA TANZANIA

Image
John Steven Akhwari ni mwanariadha mstaafu. Alizaliwa mwaka 1938 kule Mbulu- Mkoani Manyara. Aliiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Olimpic mwaka 1968 nchini Mexico, katika mashindano ya riadha ya kilomita 42. Washiriki walikuwa 75, lakini waliomaliza shindano ni 57 pekee, huku John Steven Akhwari akimaliza wa mwisho kabisa. Kwa nini alimaliza wa mwisho?   Baada ya mbio kuanza, walipofika kilomita ya 19, mshiriki mojawapo alimparamia, kumsukuma na kuanguka vibaya mno. Aliumia begani, na goti la mguu wa kulia lilitenguka. Gari la huduma ya kwanza lilimfikia na kumpa matibabu, akaweza kusimama tena na kuendelea na riadha. Umaarufu wake duniani. Watu waliomhudumia walimlazimisha kuaihirisha shindano na apande kwenye gari lakini alikataa katakata. Aliendelea na riadha huku akichechemea. Alifanikiwa kumaliza kilomita zote 42, jioni ya saa 1 kwa saa za Mexico. Watu wachache waliokuwa wamebakia uwanjani walimshangilia sana. Mwishoni kabisa, waandishi wa habari

Kiama kingine cha Majina wenye vyeti feki J’tano

Image
WAKATI watumishi wa umma 9,932 wakiwa wamebainika kuwa na vyeti feki mpaka sasa, idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka Jumatano ijayo, siku ambayo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi itatangaza majina zaidi. Ijumaa iliyopita, serikali ilitangaza kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa vyeti vya kuhitimu kidato cha nne, sita na ualimu kwa watumishi wa Sekretarieti za Mikoa, Tawala za Mikoa, Wakala wa Serikali, Taasisi za umma na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk. Laurean Ndumbaro, alisema uhakiki wa vyeti unaendelea kwa watumishi wa wizara zilizosalia na taasisi mbalimbali. Alisema uhakiki huo wa awamu ya pili na ambao utafuatiwa na awamu ya tatu, unatarajiwa kukamilika Jumatano. Alisema baada ya matokeo ya uhakiki huo kuwekwa hadharani, uamuzi wa serikali utatolewa. “Maamuzi ya watumishi 9,932 waliobainika kuwa na vyeti vya kugushi ili

WAZIRI LUKUVI AMTUMBUA AFISA MIPANGO MIJI LINDI

Image
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsimamisha kazi  Ndugu Castory Manase Nkuli Afisa Mipango Miji wa Lindi kuhusu tuhuma za kumilikisha ardhi kinyume cha sheria. Na. Hassan Mabuye & Muhammad Salim Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameamuru kusimamishwa kazi Afisa Mipango Miji wa Lindi Ndugu Castory Manase Nkuli baada ya kunyang`anya ardhi ya vijiji vya Ruvu na Mchinga hekari 4000 na kumilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate kinyume cha sheria ya Ardhi. Mhe. Lukuvi aligundua hayo baada ya kuona utaratibu wa umilikishaji wa ardhi haukufuatwa  na badala yake kuonekana kuwa na mianya ya rushwa kwa kuwa ardhi hiyo imehamishwa kutoka ardhi ya kijiji hadi kumilikishwa kwa kampuni ya Azimio ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais. Aidha, Afisa Mipango Miji huyo aligundulika kuwa na kosa la kughushi kwa kujifanya ni Afisa ardhi baada ya kuandika barua na kuisai

JB RAY NA RICH WAFUNGUKA MAZITO KUHUSU TUHUMA ZA KUHONGWA VIWANJA NA PESA

Image
Baada ya kuwepo kwa madai kuwa mastaa wa filamu Bongo, Jacob Steven (JB), Single Mtambalike (Rich) na Vincent Kigosi (Ray) walihongwa fedha na viwanja ili ‘kuinjinia’ maandamano ya hivi karibuni kupinga sinema za nje, mastaa hao wamebanwa na hatimaye kufungukia ishu hiyo inayowatafuna, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili. Chanzo kilicho karibu na tasnia hiyo kililiambia Risasi Mchanganyiko kuwa kampuni moja ya usambazaji filamu (jina kapuni kwa sasa), iliwapa fedha baadhi ya waigizaji ili wafanye maandamano ya kuziondoa sokoni filamu hizo za nje, zinazodaiwa kukingiwa kifua na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba. Inadaiwa kuwa baada ya kampuni hiyo ya usambazaji ‘kupenyeza sumu hiyo’ waigizaji hao walikwenda kwa kigogo mmoja wa kisiasa na kumshawishi kuwaunga mkono, ambaye naye alikubali na kuwaomba waigizaji hao kufanya kila wawezalo, kumtoa kwenye kiti chake, Simon Mwakifwamba, kwani ana ukaribu na hasimu wake wa siasa. “Kuna watu w

Hali ya Mbunge wa Chadema Tarime si Shwari

Image
Hali ya Mbunge wa Tarime Vijijini Mh. John Heche imebadilika usiku wa kuiamkia leo na amekimbizwa hospitalini Dodoma.  Huenda akahamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Tumuombee comrade Heche na pole sana kwa familia na wabunge wenzake.