WEMA SEPETU ADAIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA
Skendo ya mastaa mbalimbali Bongo kutajwa katika biashara na usafirishaji wa madawa ya kulevya ‘unga’ linazidi kuchukua sura mpya ambapo tayari majina ya wasanii wawili wakubwa, Wema Isaac Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ yametajwa huku kinachowaponza kikijulikana. Habari zinadai kuwa mastaa hao wameanza kujutia tambo zao za kutangaza utajiri walionao hivyo kuibua maswali kuwa huenda wana uhusiano na wafanyabiashara wa dawa za kulevya ikiaminika ndiyo njia ya haraka ya utajiri. WEMA Inadaiwa kuwa kitendo cha Wema kutangaza kununua nyumba, magari ya kifahari na kutapanya fedha ndiko kulikomponza na sasa anatajwa na wengi vinywani mwao juu ya kuhusika katika biashara hiyo haramu. Kuna madai kuwa bosi huyo wa Endless Fame Productions amehojiwa juu ya suala hilo lakini meneja wake, Martin Kadinda alikanusha uvumi huo. DIAMOND Wiki iliyopita, Diamond aligeuka gumzo baada ya kuripotiwa akihusishwa na biashara hiyo huku ikidaiwa kuwa kinachomponza ni u...