Posts

Showing posts from June 1, 2016

Mume, Mke Wachinjwa Kinyama.

Image
Majeneza yenye miili ya marehemu hao. Na Gregory Nyankaira, RISASI MCHANGANYIKO MARA: Hali mbaya! Wanandoa Said Somba (48) na Kadogo Ehijo (47), wakazi wa Kitongoji cha Rugala, Kijiji cha Mazami, Kata ya Bukabwa wilayani Butiama mkoani hapa wameuawa kwa kuchinjwa shingo na watu wasiojulikana, Risasi Jumatano lina kila kitu. Marehemu Somba (kushoto) na marehemu Kadogo kulia. Diwani wa Kata ya Bukabwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Rugala, Jonas Maswe aliliambia gazeti hili kuwa, tukio hilo lilijiri usiku wa Mei 25, mwaka huu ambapo watu hao wakiwa na mapanga walivamia nyumbani kwa Somba akiwa amelala na mkewe na kuwachinja. Baadhi ya watoto wa marehemu wakilia juu ya jeneza la baba yao Alisema wakati wanachinjwa, wanandoa hao hawakupiga kelele na baada ya ukatili huo  wauaji hao waliifunika miili yao kitandani kisha wakatokomea kusikojulikana.  Alisema mauaji hayo yalifanyika kimyakimya kwani hata  watoto wa marehemu waliokuwa wame...

Je, Wajua! Maganda ya chungwa tiba kwa ugonjwa wa Mba kichwani

Image
  Watu wengi wanasumbuliwa na ugonjwa wa mba kichwani, awali nilishawahi kuandika kuhusu tiba nyingine, lakini ninaongeza na hii ili kuwasaidia. Mara nyingi mba huwa wanatokea nyakati za baridi kwani kichwa huwa ni kikavu sana kama unasumbuliwa na hilo tatizo unatakiwa kuwa makini na mafuta unayotumia na kuhakikisha unatumia mafuta kila unapoosha nywele zako. Jinsi ya kufanya Chukua chungwa limenye upate maganda yake baada ya hapo chukua limao likamue kisha uweke kwenye Brenda usage upate mchanganyiko mmoja. Matumizi Osha nywele zako kwanza zitakate na baada ya hapo zikaushe kisha paka mchanganyiko wako kwenye ngozi acha kwa muda wa dakika 20-25 kisha osha kwa kutumia shampuu unayotumia ambayo unaamini ni nzuri. Tumia tiba hii kwa wiki mara tatu utaona jinsi utakavyokomesha moja kwa moja tatizo la mba kichwani.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMWAKILISHA RAIS DKT JOHN MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA AFRIKA, NCHINI PAPUA NEW GUINEA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Papua New Guinea Mhe. Peter O Neil Alipowasili Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Papua New Guinea leo Mei 31,2016 kwa ajili ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific (ACP) unaojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama, kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe walipokutana Katika kituo cha Mikutano cha kimataifa ACC mjini Papua New Guinea leo Mei 31,2016 kwa ajili ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa siku mbili kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific (ACP) unaojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama...

Hatimaye Siwema wa Nay Atoka Gerezani!

Image
Mzazi mwenzake Nay wa Mitego, Siwema Edson. Na Gladness Mallya, RISASI MCHANGANYIKO HABARI njema! Mzazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson aliyehukumiwa miaka miwili jela kwa kosa la kutishia kwa njia ya mtandao, hatimaye ametoka jela. Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko , Nay wa Mitego alisema katika harakati za kushughulikia ili mzazi mwenzake huyo atoke alifanikiwa kupata mawakili wawili ambao mpaka Jumamosi iliyopita walifanikisha zoezi la Siwema kutoka na sasa atatumikia kifungo cha nje. Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mzazi mwenzake,  Siwema Edson Nay wa Mitego alisema alilazimika kupambana kwa nguvu zote si kwa sababu anataka kuwa naye isipokuwa kama mzazi hakujisikia vizuri kuona mama wa mwanaye yuko jela wakati yeye anao uwezo wa kufanya kitu kwa ajili ya kumsaidia. “Kulikuwa kuna njia mbili za kufanya, kukata rufaa au kubadilishiwa kifungo, mawakili wangu waliniambia niwaachie wao watam...

Hii Ndiyo Sababu ya Wanafunzi 7802 UDOM Kurudishwa Nyumbani

Image
JUMUIYA ya Wanataaluma ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) imesema kilichotokea si walimu kugoma kufundisha programu ya Stashahada Maalumu ya Elimu, Sayansi, Hisabati na Tehama, bali tatizo ni kutoelewana na Menejimenti ya chuo kutokana na mazingira mabovu ya uendeshaji wa programu hiyo chuoni hapo. Aidha, imelaani kitendo cha wanafunzi 7,802 wa Programu Maalumu ya Ualimu wa Msingi na Sekondari, waliorudishwa nyumbani bila kupewa muda wa kutosha kujiandaa kwa kuzingatia umri wao na mazingira waliyokuwa wanaishi, hali inayofanya wazagae mitaani huku wakiwa hawana pa kwenda. Hayo yako kwenye tamko lililotolewa jana na Katibu wa jumuiya hiyo, Lameck Thomas, ambalo lilieleza kuwa lawama zimekuwa zikitupwa kwa walimu kutokana na taarifa hizo kutolewa na upande mmoja, ambao ni Menejimenti ya chuo kwenda serikalini bila kuwepo na taarifa yoyote kutoka kwa walimu kupitia jumuiya yao. Thomas alisema si kweli kama walimu waligoma kufundisha lakini tatizo kubwa ni kutoel...

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI KATIKA HAFLA YA UTOAJI WA TUZO ZA RAIS KWA WAZALISHAJI BORA WA VIWANDA KWA MWAKA 2015.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na washindi mbalimbali waliopata tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa viwanda kwa mwaka 2015.    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo mpya ya Tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa Viwanda    PMAYA  The President’s Manufacure of the Year    pamoja na Mwenyekiti wa Wenyeviwanda Tanzania CTI Dkt. Samwel Nyantahe katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wadau mbalimbali wa CTI na kutoka Sekta ya Viwanda nchini kabla ya kutoa Tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2015 katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Leodgar Tenga mara baada ya ku...

SERIKALI KUANZISHA BENKI YA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI.

Image
Na Lilian Lundo-MAELEZO. Serikali ya awamu ta Tano imedhamiria kuifanya sekta ya Viwanda nchini kuchangia pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka asilimia 7.3 ya sasa. Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli amesema kuwa jambo hilo linawezekana hasa kwa kuzingatia nchi yetu ina rasilimali zinazohitajika katika kujenga uchumi wa viwanda.“Nafahamu kwamba tunakila aina ya rasilimali inayowezesha uwepo wa viwanda hapa nchini ikiwemo umeme wa kutosha pamoja na malighafi zake na kwa maana hiyo serikali ya awamu ya tano imepanga kuifanya sekta ya viwanda kuchangia pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka 7.3 ya sasa”. Alisema Rais Magufuli. Aidha Dkt. Magufuli aliwatoa wasiwasi wadau hao kuhusu uwepo wa soko la uhakika kwa bidhaa zitakazozalishwa kwani Tanzania im...

BOSI WA ZAMANI WA TRA KITILYA NA WENZAKE WAZIDI KUSOTA MAHAKAMA YA RUFAA

Image
Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya akienda kupanda gari litakalompeleka rumande. Sioi Sumari akiwa na askari wa magereza. Shose Sinare naye akiongozana na askari magereza kuelekea kwenye gari lililompeleka rumande. Baadhi ya mawakili na wananchi wakitoka mahakamani. LEO katika Mahakama ya Rufaa Tanzania, jijini Dar es Salaam Kamishna Mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake  waliokuwa wafanyakazi wa Benki ya Stanbic Tanzania, Sioi Sumari na Shose Sinare walifikishwa mahakamani hapo kusikiliza rufaa iliyokatwa na upande wa Jamhuri. Jamhuri imekata rufaa kupinga kufutwa shitaka namba 8 linalowakabili wote kwa pamoja la utakatishaji fedha linalowakabili. Hata hivyo, mahakama hiyo itapanga tarehe ya kusikilizwa shauri hilo siku itakayotangazwa. Washitakiwa hao wanakabiliwa na shitaka la kula njama na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kinyume na sheria na walifikishwa mahakamani kwa m...