MSIBA WA MASOGANGE WAZIMA NDOA YA ABDU KIBA
MSIBA wa aliyekuwa video queen mkali Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ aliyefariki Ijumaa iliyopita, umezima tukio kubwa la kufunga ndoa la msanii wa Bongo Fleva, Abdul Kiba ambaye alioa jana alfajiri. Abdul Kiba ambaye amefunga ndoa siku tatu tu baada ya kaka yake, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ aliyemuoa Amina Khaleef huko Mombasa nchini Kenya. Msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake ya Jeraha alifunga ndoa hiyo jijini Dar, jana kwenye Msikiti wa Kichangani, Magomeni ambapo alimuoa mchumba wake wa muda mrefu, Luwada Hassan. Habari zilizolifikia Ijumaa Wikienda jana zilieleza kuwa, huenda Ali Kiba na Abdul Kiba wakafanya sherehe ya pamoja ya harusi Aprili 29, mwaka huu kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar ili kufurahi na watu wao wa karibu kufuatia zoezi la wao kufunga ndoa. Taarifa zilieleza kuwa, baada ya Ali Kiba na Abdul Kiba kuoa, dada yao, Zabibu Kiba, naye anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na beki za zamani wa Timu ya Simba ambaye kwa sasa an...