Sakata la Mauaji Msikitini Mwanza: Kundi la Kigaidi la ISIS lahusishwa
YADAIWA ni kisasi baada ya Polisi kuwakamata wanaharakati wa IS saa 24 kabla. "baada ya swala kumalizika, watu hao waliingia na kuwaamuru kulala chini huku wakitoa bendera nyeusi na maandishi ya meupe ya Kiarabu kisha kumtaka Imamu wa msikiti kujitokeza mbele, bendera hiyo ni kama ile inayotumiwa na kundi la kigaidi la IS" "Imamu alipojitokeza huku tukiwa tumelala chini, watu hao walisikika wakisema 'Kwa nini mnaswali wakati wenzetu wamekamatwa na polisi, wengine wanapigana 'jihad'...hali hiyo ilitushtua zaidi baada ya Imamu kuanza kuchinjwa kwa panga," "Ghafla wakatuamuru kulala kifudifudi na kudai wao ni IS wamekuja kufanya kazi yao, kisha wakaanza kutushambulia na kujeruhi. Mwenzangu niliyekuwa naye pembeni alikatwa panga na kuangukia juu yangu, hali hiyo ilinifanya nionekane kama nimekufa," Habari za uhakika ambazo Nipashe imezipata zinasema. Imam huyo na wafuasi wake, waliuwawa na kundi la watu wanane waliokuwa na bu...