Posts

Showing posts from November 5, 2016

Listi Ya Wasanii Watakao Kinukisha Jukwaa La Fiesta, Dar leo

Image
Staa kutoka Nigeria, Yemi Alade. Mkali wa ngoma ya Wash, Where, Dulo kutoka Nigeria, Tekno Miles. Staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba. Msanii wa Bongo Fleva, Darassa. Maua Sama. Jux. Baraka The Prince . Shilole. Roma. Vanessa Mdee . Raymond. Sholo Mwamba . Snura . Man Fongo . Fiesta 2016 kwa kishindo cha Tigo leo viwanja vya Leaders manispaa ya kinondoni jijini Dar es salaam, jukwaa litashereheshwa na orodha ifuatayo kwa wasanii kutoka hapa nyumbani. Ni pamoja na Alikiba, Baraka The Prince, Barnaba, Bell 9, Billnas, Chege, Christian Bella, Darassa, Dogo Janja, Fid-Q, Hamadai, Jay Moe, Juma Nature, Jux, Lord Eyez, Man Fongo, Maua Sama, Mr Blue, Msami, Nandy, Raymond, Roma, Shilole, Sholo Mwamba, Snura, Stamina, Vanessa Mdee, Weusi na Young Dee. Jukwaa pia litashereheshwa na wasanii kutoka nje ya Tanzania, ni pamoja na Jose Chameleon kutoka Uganda, Tekno Miles na Yemi Alade kutoka Nigeria. Fiesta 2016 Imooooo! Kwa tiketi

MWANAMKE ALIYEKAA SIKU NZIMA KWENYE JENEZA ILI KUPATA UZOEFU WA KIFO

Image
Imetokea nchini Brazil na Mwanamke  anayeitwa Vera Lucia da Silva na umri wake ni miaka 44 ambapo aliamua kukaa kwenye jeneza siku nzima ili apate uzoefu wa mazingira ya kifo ili siku akifa asiwe mgeni na Jeneza. Vera aliamua kukaa kwenye jeneza huku familia yake ikifanya vitu vinayofanywa kwenye msiba ili aone inakuaje ambapo baada ya kutoka humo alisema ilikua siku nzuri zaidi kwenye maisha yake yote. Sherehe hiyo ya kujifunza maisha ya kwenye Jeneza ambayo ilifanyika Jumatano ya November 2 2016 ni sherehe ambayo ilifanyika kwenye eneo la makaburi.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMEONGOZA MATEMBEZI YA HISANI KWA AJILI YA KUSOMESHA WAUGUZI WAKUNGA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi ya viungo kabla ya kuanza kwa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi ya viungo pamoja na umati uliojitokeza kabla ya kuanza kwa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiongoza Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga ambapo alitembea kwa kilometa 4.3 kuanzia viwanja vya Green Ground na kupitia barabara ya Toure na kurejea na barabara ya Msasani ,Oysterbay jijini Dar es Salaam wengine pichani ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Umm

Polisi Dar Yaeleza kwa Nini Hawajamkamata Tundu Lissu

Image
DAR ES SALAAM: Jana, Novemba 4, 2016 iliripotiwa kwenye vyombo vya habari kwamba Mbunge na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu anatakiwa kukamatwa kwa amri ya Mahakama baada ya kutotimiza masharti ya Mahakama kwa kutohudhuria kwenye kesi yake inayomkabili Kisutu, Dar. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kwa Kamishna wake Simon Sirro imesema sababu za kwanini Tundu Lissu hajakamatwa mpaka sasa ni kutokana na Polisi kutopokea hati yoyote kutoka Mahakamani Kisutu inayoagiza kukamatwa kwa Tundu Lissu lakini ikiwafikia tu watafanya hivyo.

Hatimaye Bunge Lapitisha Mswada Sheria ya Huduma za Habari

Image
Hatimaye mchana huu wabunge wamepitisha bungeni muswada wa sheria ya huduma za habari wa mwaka 2016 uliojadiliwa kwa siku mbili. Mswada huo uliwasilishwa bungeni jana mjini Dodoma na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kisha wabunge wakaanza kuujadili. Picha na Edwin Mjwahuzi