Posts

Showing posts from January 12, 2014

HIVI NDIVYO VYAKULA 10 AMBAVYO MWANAUME ANATAKIWA KULA ILI KUONGEZA UWEZO WAKATI WA TENDO LA NDOA.

Image
  CHAZA NA PWEZA Aina hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa. POMEGRANATE Ni aina fulani ya matunda mekundu yanayofananana na apple. Haya yatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa. Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume na kuacha idadi ya wanawake wanaokabiliwa na tatizo hilo kwa mujibu wa uchunguzi kubaki na asilimia 13. Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo mio

Mtoto wa Whitney Houston kaolewa na Kaka yake

Image
  Stori inaamplfy kwamba mtoto wa mwimbaji staa Marehemu Whitney houston, Bobbi Kristina amevunja mapendekezo ya familia yake ya kutoolewa na kijana ambae ni kama kaka yake, mshkaji ambae alilelewa toka mdogo na Whitney na wao wote kuishi nyumba moja. Pamoja na kushupaliwa kutoolewa, Bobbi ambae ana umri wa miaka 20 amethibitisha kuolewa na boyfriend huyu aitwae Nick Gordon ambae wamekua mapenzini kwa miaka kadhaa ambapo sasa hivi kama wanajipanga kuja na show yao ya TV. U

ANGALIA PICHA RAIS DK. SHEIN ALIVYOTUNUKU VYETI

Image
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na kamati ya Nishani alipowasili katika uwanja wa Ikulu Mjini Unguja katika sherehe za kutunuku Nishani ya Mapinduzi kwa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Wastaafu,Viongozi walioasisi,kuenzi na kudumisha Mapinduzi,pamoja na Viongozi mbali mbali wenye sifa za Kipekee na wenye Sifa Maalum,katika shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisimama pamoja na Viongozi,Wananchi pamoja na Wakuu wa vikosi vya Ulinzi wakati wimbo wa Taifa Ukipigwa katika sherehe za kunuku Nishani ya Mapinduzi,katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtunuku Nishani ya Mapinduzi Rais Mstaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,katika hafla kutunuku Nishani iliyofanyika viwanja vya Ikulu M

‘Mijimama’ inavyoingiza waosha kucha, miguu katika hatari ya kuambukizwa VVU

Image
Biashara hii inazidi kukua huku pia huduma zinazotolewa zikizidi kuongezeka kila kukicha, ambapo mara nyingi wanaotengeneza kucha, hujihusisha na usuguaji wa miguu, uchoraji wa tattoo ukandaji wa mwili (massage)na nyingine zinazofana na hizo.  Kwa ufupi Eneo alilotaka nimchore ndilo lilianza kunipa wasiwasi, lakini kwa sababu ya pesa nikapiga moyo konde Kazi hiyo huchangia kwa kiasi kikubwa pia kuwaweka vijana katika hatari ya kupata maradhi ya ngozi hasa fangasi kutokana na wengi wao kutotumia vifaa vya kujikinga. Utengenezaji wa kucha na uoshaji miguu ni biashara inayokuwa kwa kasi hasa maeneo ya mijini ambapo wanawake wengi wanahusudu na kujihusisha na masuala ya urembo. Biashara hii inazidi kukua huku pia huduma zinazotolewa zikizidi kuongezeka kila kukicha, ambapo mara nyingi wanaotengeneza kucha, hujihusisha na usuguaji wa miguu, uchoraji wa

Rais wa Comoro Awasili Zanzibar Kuhudhuria Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi

Image
   Rais wa Jamhuri ya Comoro Mheshimiwa DR. Ikililou Dhoinine akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar na Kupokea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.   Rais wa Jamhuri ya Comoro Mheshimiwa Dr. Ikililou Dhoinine akisalimiana na baadhi ya wana jumuiya ya Wakfi ya Wangazija hapa Zanzibar waliofika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar Kumpokea.   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Comoro Mheshimiwa DR. Ikililou Dhoinine  kwenye chumba cha watu mashuhuri(VIP)hapo uwanja wa ndege wa Zanzibar. Picha na Hassan Issa-Ofisi ya   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Image
:   Kwa kipindi kirefu sasa vijana ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) tumeshuhudia na kusikia kauli na vitendo vya baadhi ya wanachama wa CCM vinavyoashilia ukiukwaji wa makusudi wa maadili, miiko na kanuni za Chama. CCM katika uhai wake wa miaka 37 baada ya kuunganisha TANU na ASP, imeendelea kukua na kushamiri kutokana na misingi imara ya kikatiba tuliyojiwekea tangu mwaka 1977, ambayo wana CCM wote kwa utashi na hiari tumeienzi na kuifuata. Asiyetaka, ni ruksa kuondoka na kutuachia chama chetu. Ni kwa njia hii tumeweza kuimarisha mshikamano ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kutuwezesha kushinda katika chaguzi mbali mbali, hivyo kuendelea kutoa uongozi katika ngazi zote za utawala nchini.  Hivyo basi, kitendo chochote kile chenye mwelekeo wa kubomoa mshikamano ndani ya Chama, ni kitendo cha kutudhoofisha, hivyo kutuengua katika uongozi wa nchi. HILI KWA VIJANA WA CCM, HALIKUBALIKI! Tunasema hivyo kwa sababu kuanzia mwaka huu tunaingia kwenye mchakato wa chaguzi m