Mwalimu atiwa mbaroni kwa kumuua mtoto wa miezi 7
Mwalimu wa sekondari Stephen Wachira Wangara mwenye umri wa miaka 43, amefikishwa Mahakamani kwa kosa la kumuua mtoto wake wa miezi 7 kwa kumchinja na panga nchini Kenya. Mashahidi watano wa tukio hilo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Jimbo la Kirinyaga, Maina Muriuki wamemweleza Jaji Lucy Gitari wa Mahakama Kuu ya Kerugoya, jinsi mtuhumiwa alivyoua mtoto wake, Maina ameieleza Mahakama kuwa mwili wa mtoto huyo ulikuwa umewekwa ndani ya gunia ukiwa na damu, nje ya nyumba ya Wangara na pembeni ya mwili huo kuliwa na panga ambalo lilitumiwa kumuua mtoto huyo. Shahidi mwingine Joseph Muriithi amesema wakati wa tukio hilo alikuwa shambani kwa Wangara akifanya kibarua na alimwona mtuhumiwa akiwa na madoa ya damu na muda mfupi baadaye alisikia kelele kutoka kwenye nyumba ya mwalimu huyo. Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi March 1, 2018, ambapo itasikilizwa tena. Wangara ambaye ni mtuhumiwa ni baba mwenye watoto wawili na mwalimu katika shule ...