Posts

Showing posts from August 10, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AANZA ZIARA YAKE MKOANI MWANZA.

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza.    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kuwasili akitokea Chato mkoani Geita. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wanakwaya wa UWT Kisima cha maji Chumvi mara baada ya kuhutubia wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza.     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwalimu Mstaafu wa Shule ya Sekondari Sengerema Wilson Fumbuka Mbanga ambaye walifundisha naye shule hiyo tokea mwaka 1982-1985 mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara Sengerema Mkoani Mwanza.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kumaliza kuwa

WANACHAMA NA MASHABIKI WA YANGA WAMSHAMBULIA MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA BAADA YA KUANDIKA MANENO HAYA MTANDAONI

Image
Kitendo cha wanachama wa klabu ya Young Africans kumruhusu mwenyekiti wao, Yusuph Manji kuikodi klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 10 kinaendelea kuwagusa watu wengi na mmoja wapo ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye amefikia hatua ya kuandika ujumbe katika mitandao ya kijamii. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makonda ameandika “Unataka kujuwa kwa nini Tanzania ni masikini pamoja na UTAJIRI MKUBWA WA MALIASILI tulizonazo? Soma Mkataba wa Yanga wanaosaini LEO” Baada ya kuweka picha hiyo wadau mbalimbali wa soka nchini wamekua wakianzika maoni yao katika ujumbe wa Makonda, wengine wakimtaka asizungumze mambo ya Young Africans, na wengine wakimtaka afanye kazi za serikali na aache kujihusisha na soka na mashabiki wa klabu hiyo nguli hapa nchini. Awali Makonda aliweka picha ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na kusema kuwa alikuwa na maswali 87 kwa kiongozi huyo wa Yanga lakini baada ya kutizama mahojiano aliyofanyiwa, aligundua kwamba kiongozi

Hukumu Kesi Ya Babu Tale Bofya Hapa!

Image
ILE kesi inayomkabili Meneja wa Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Babu Tale ya kusambaza na kuuza DVD za mawaidha ya Shehe Hamis Mbonde bila ridhaa yake imeahirishwa tena na Mahakama Kuu ya Kanda ya Dar es Salaam hadi Agosti 24, mwaka ambapo hukumu itatolewa. Akizungumza mbele ya mawakili na wahusika wa pande zote mbili leo asubuhi, Msajili wa Mahakama, Kayonza alianza kwa kutupilia mbali hoja ya mawakili wa upande wa Babu Tale, Robert Mkoba na Augustino Aluta iliyoomba kupewa muda zaidi kwa sababu ya mmoja kati ya mawakili wao (Paul Mgaya) ana udhuru na kwamba yupo jijini Arusha kwa semina. “Mawakili mnaosikiliza kesi hii kwa upande wa Tale mpo watano, siwezi kuruhusu tena kuahirishwa kwa kesi hii kisa mmoja hayupo. Agosti 24 itakuwa siku ya hukumu na kutekelezwa ambacho kipo na niwaombe wote muwepo,” alisema Kayonza. Awali kesi hiyo ilitakiwa itolewe hukumu Agosti 1 lakini kutokana na Mgaya kuumwa ilibidi kuahirishwa hadi leo (Agosti 10). Wakili wa

REAL MADRID NA SEVILLA WALIVYOTOANA JASHO KWENYE MCHEZO WA UEFA SUPER CUP USIKU WA KUAMKIA LEO

Image
Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos akishangilia huku akinyanyua kombe na wenzake baada ya kutwaa ubingwa wa Uefa Super Cup baada ya kushinda 3-2 dhidi ya Sevilla huko Norway  Beki wa Real Madrid Dani Carvajal akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la tatu na ushindi dhidi ya Sevilla kwenye mchezo wa Uefa Super Cup. Sergio Ramos akiifungia Real Madrid goli la kusawazisha kwa kichwa na kufanya matokeo kuwa 2-2 dhidi ya Sevilla kwenye mchezo wa Uefa Super Cup, kabla ya kuibuka na ushindi ndani ya dakika 120.  Konoplyanka, ambaye hakuwa kwenye kiwango bora kwenye Michuano ya Euro 2016 na Ukraine, akifunga mkwaju wa penati na kuipa Sevila uongozi wa mabao 2-1.