SHUHUDIA DK. MAGUFULI ALIVYORUDISHA FOMU ZA URAIS NEC LEO
Mgombea urais kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damiani Lubuva, wakati alipowasili ofisi hizo. …Akiwa na mgombea mwenza, Samiah Hassan Suluhu. Viongozi wa CCM waliomsindikiza mgombea wao wa urais. Lubuva (kulia) akizungumza jambo wakati wa kurudisha fomu hizo. Magufuli akionyesha fomu wakati wa kurudisha. Mgombea urais kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari baada ya kurudisha fomu. Wanahabari wakiwa kazini katika hafla hiyo. Magufuli akitoka ofisi za NEC baada ya kukamilisha zoezi hilo. MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli, leo amerudisha fomu ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). NEC iliwataka wagombea wote wa urais kupitia vyama vyote vya siasa kurudisha fomu leo Agosti 21 baada ya kuzunguka mikoa ya Tanzania kutafuta wadhamini, ambapo vyama vyote hivyo viwili vimeonekana kukidhi vigezo na kurudisha fomu hizo. (PICHA: DENIS MTIM...