WATU WANNE MBARONI AKIWEMO M/KITI WA KIJIJI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YAKIHUSISHA IMANI ZA KISHIRIKINA MKOANI DODOMA
Watu watatu wameuawa Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma katika matukio mawili tofauti yanayohusisha imani za kishirikina. Akizungumzia matukio Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema tukio la kwanza limetokea tarehe 01/03/2015 majira ya saa 01:00hrs katika kitongoji cha Golani, kijiji cha Masinyeti, kata ya Iduo, tarafa ya Mlali Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la SAIDIA S/O CHAKUTWANGA mwenye miaka 80, kabila Mkaguru, Mkulima Mganga wa kienyeji aliuawa na watu waliojichukulia sheria mkononi kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kutobolewa macho. Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina wakimtuhumu marehemu kuwa anazuia mvua kunyesha katika eneo hilo. Pia Kamanda MISIME amesema katika tukio lingine limetokea tarehe 01/03/2015 majira ya saa 02:00hrs katika kitongoji cha Majengo, kijiji cha Ihanda, K...