MTOTO WA MIAKA 12 AFUNGUKA ALIVYOFUNDISHWA UCHAWI
Mtoto (kulia jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 12 anayemtuhumu baba yake kumfundisha uchawi. MTOTO mmoja mkazi wa Kimara Salanga, jijini Dar es Salaam (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 12 hivi karibuni aliibuka na kutoa madai mazito, akimtuhumu baba yake mkubwa kuwa alimfundisha uchawi, Ijumaa lina mkasa kamili. Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, mtoto huyo alisema alianza kufundishwa tabia hiyo mbaya na baba yake mkubwa wakati huo akiwa na umri wa miaka mitano jijini Mbeya, kwa kumwelekeza namna ya kuroga na kuua watu. Katika mojawapo ya matukio makubwa aliyodai kuwahi kuyafanya ni pamoja na kutengeneza ajali ya boti iliyotokea Nungwi mapema mwaka huu ambapo yeye na wenzake walitumwa na baba yake huyo kutega mambo yao huku wengine wakipanda kwenye chombo hicho ili kuongeza uzito uliosababisha boti hiyo kuzama na kuua watu kibao. “Tuligandisha maji na kuweka sindano ambazo zilitoboa na baada ya watu kufa tulic...