Taarifa za ndani ya familia… Diamond ‘mchafu’
Diamond Platnumz Imelda Mtema na Musa Mateja Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amejikuta akiwatibua baadhi ya ndugu zake huku wengine wakimuita mchafu kutokana na kitendo cha kumpachika mimba mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’ kisha kuwepo madai kuwa ‘amewajaza’ pia mamodo Hamisa Hassan ‘Mobeto’ na Irene Hilary ‘Lynn’. Mmoja wa ndugu wa karibu wa Diamond aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, familia imeshtushwa na madai kuwa kijana wao huyo mbali na kwamba Zari a.k.a Mama Tiffah ni mjamzito, amewapa mimba tena Mobeto na Lynn. Zari. ILIKUWAJE? Miezi kadhaa nyuma, yaliibuka madai kuwa Zari ni mjamzito lakini Diamond amekuwa mgumu kulizungumzia hilo licha ya hivi karibuni mazazi mwenziye huyo kutundika picha akionesha kitumbo chake kilichodhihirisha kuwa ndani yake kuna kiumbe. Lynn LYNN NAYE Huku mashabiki wa Zari ‘Team Zari’ wakionesha furaha ya staa wao ‘kumshika’ mwanamuziki huyo kwa kumbebea ujauzito mwingine, zikaibuka taa...