Msalaba wa ajabu wamshangaza mama Kanumba
Mama wa staa wa sinema za Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa akiwa makabulini. DAR ES SALAAM: Jambo limezua jambo! Baada ya hivi karibuni barua yenye ujumbe mzito kukutwa kaburini kwa aliyekuwa staa wa sinema za Bongo, marehemu Steven Kanumba, limezuka jipya ambapo kitu kilichopo kaburini kinachodaiwa ni msalaba (kilichozungushiwa duara pichani) kimemshangaza mama wa Kanumba, Flora Mtegoa. Kitu hicho cha chuma chenye umbo la pembe tatu katikati kikiwa na alama ya msalaba, kwa juu kuna picha ya Kanumba, chini kuna maandishi ya DJ na katikati maandishi ya RIP SCK kilizua gumzo hivi karibuni kwenye kumbukumbu ya marehemu kutimiza miaka 4 ambapo baadhi ya watu waliohudhuria Makaburi ya Kinondoni alikozikwa walipigwa butwaa. Baadhi yao walisema chuma hicho kilitengenezwa kwa mfano wa alama mojawapo ya imani ya Freemason ambayo baada ya kifo chake, kuna watu walihusisha kifo hicho na imani hiyo. Muonekano wa msalaba huo ukiwa juu ya kabuli la mare...