Posts

Showing posts from March 6, 2015

TASWIRA RAIS KIKWETE ALIPOZINDUA RASMI AZAM TV JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza rasmi kuzinduliwa kwa studio mpya za stesheni ya Azam TV Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015. Pamoja naye kwenye kilinge cha utangazaji ni mmiliki wa stesheni hiyo Bw. Saidi Salim Bakhressa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Mkurugenzi wa Azam TV Bw. Dunstan Tido Mhando wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakat...

NINI MAONI YAKO KUHUSU KAULI YA SINTAH JUU YA SHILOLE NA MZIWANDA?

Image
  “Jamani jamani mnaosema ooh umasikini mmbaya kwanini Shilole anamdhalilisha bwana yake, jamani kwani huyo ‘so calle’ Nuh or ‘whatever’ his name is kalazimishwa?? unajua siku hizi mapenzi yamemekuwa ‘free’ sana yaani ukiona mtu anakupa vitasa mara humuelewi yanini kun'ga'gania ‘as if’ umezaliwa naye, mtu uliyemjua ukubwani nae akupe shida ‘BIG NO i would rather stay single for the rest of my life’, kwanza sio adhabu kuwa ‘single’ kuliko kuwa katika ‘unhealthy relationship’ ...  Mnaomuonea huruma huyo ‘so called’ Mziwanda ni wanafiki mapenzi ya mtu mbili kama anapigwa vitasa na anatulia anajua mwenyewe alichokifanya na atulie, kuliko kusema ni umasikini kwani yeye ni kiwete? ina maana hawezi kutafuta kazi akapata mpaka awe msingi kiuno? ‘hell no’ muacheni apokee makonde, vitasa, nk,  vijana kama yeye wapo wengi tuu kazi ‘kujisexisha’ na kuwa msingi kiuno mjini ndio wanafanya taifa linadidimia kwa umasikini, vijana wenye nguvu wanatakiwa wafanye k...

WATU WANNE WAHUKUMIWA KIFO,MAUAJI ALBINO

Image
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mlemavu wa ngozi, Zawadi Magimbu (32) wakiwa ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Geita baada ya kuhukumiwa kunyongwa.  Kutoka kushoto ni Nasoro Charles, Singu Siantemi, Masaru Kahindi na Ndahanya Lumola. Picha na Jackline Masinde.  Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji Joacquine De-Mello wa Mahakama Kuu, ambaye alisema alisema Mahakama imeridhika pasi na shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka kwamba walihusika moja kwa moja na kifo hicho. Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Nassoro Charles mkazi wa Kijiji cha Beda mkoani Kagera, Masaru Kahindi mkazi wa Kijiji cha Nyamaruru, Ndahanya Lumola na Singu Nsiantemi wakazi wa Kijiji cha Kakoyoyo, Wilaya ya Bukombe. Jaji De-Mello alisema washtakiwa walifanya kosa hilo Machi 11, 2008 saa 1:00 usiku nyumbani kwa akina Zawadi wakati wakipata chakula cha usiku, walimkata kwa shoka na panga miguu yote na mkono wa kulia. Alisema Masaru Kahindi aliyekuwa jirani na Zawadi, ...

UKWELI KUHUSU MAREHEMU KEPTENI KOMBA NA MSANII LULU MICHAEL

Image
HATIMAYE siri ya madai kuwa Mheshimiwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Damian Komba na msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ni wapenzi, sasa mambo hadharani, Risasi Mchanganyiko linakupa ukweli. Mambo hayo ambayo yamekuwa katika vinywa vya watu na kuzagaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwa muda mrefu, yamewekwa kweupe na Mheshimiwa Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa la Tanzania One Theatre (TOT). LAIVU ITV Akizungumza katika Kipindi cha Shamsham za Pwani kinachoongozwa na Mtangazaji Hawa Hassan kupitia Runinga ya ITV Jumamosi iliyopita, Kepteni Komba alifunguka kuwa hajawahi kutembea na msanii huyo kama watu wanavyodai. HUYU HAPA KEPTENI KOMBA “Huwa ninawasaidia wasanii wa jinsi zote lakini watu wakiona nimemsadia msanii wa kike, wanavumisha kwamba nimemtafuna,” alisema Kepteni Komba. Alikiri kuwa alishawahi kumpa Lulu gari lake la kifahari pale msanii huyo alipokwenda na marehemu Steven Kanumba kumuomba kwa ajili ya kumpo...