Posts

Showing posts from March 2, 2015

Soma Alichoongea MPOKI kuhusu msiba wa Kapteni John KOMBA.. #RIP John Komba

Image
Msanii wa Kundi la   Orijino Komedi ,   Mujuni Sylivery  aka   Mpoki   moja ya vitu ambavyo aliwahi kuvifanya katika kazi yake ya uchekeshaji ni pamoja na kuigiza sauti ya marehemu, Kapteni   John KOMBA   ambaye amefariki siku ya juzi February 28. Leo   Mpoki   amesikika kwenye Leo Tena @CloudsFM, alianza kuzungumzia namna alivyopokea taarifa za msiba huo; “ ..Mtu akishatoweka kwenye ulimwengu akifariki dunia inauma kwa sababu mtu unayempoteza leo huwezi kumpata tena.. lakini ukimpoteza mbuzi utaenda Vingunguti utamnunua na sherehe itaendelea.. Kitendo cha kufariki mtu yoyote hata kama hajulikani ni pengo kubwa tu ” “ Imeniathiri kwa kisanii kwa kuwa nilikuwa namuwezea, kidogo alikuwa hapendi lakini ilivyokuja akatulia.. Watu wakamwambia bwana hawa watoto tu.. Ukimuiga mtu ana mazuri huwezi kumuiga kwa mabaya tu.. ana mazuri yake..Ikanipa wigo mpana kwenye kazi yangu ya kubuni sauti yake, vitendo.. “ “ mwisho wa siku kaondok...

ANGALIA BIG BOSS ZARI AKILA BATA KWENYE BOTI MATATA

Image
Mrembo mwenye maskani yake nchini Sauzi Zarina Hassani Zari 'thebosslady' jioni ya leo ameshare na mashabiki wake picha hizi ikimuonyesha anakula raha katika boti moja ya kifahari katika nchi ambayo hakuianisha huku ikionyesha kitumbo chake (ujauzito) ukionekana kuzidi kukua Diamond mungu akijalia ataitwa baba naniliiiiiiiiiiiiiiiiii   Tazama picha hapa chini

VIONGOZI WAONGOZA KUMUAGA MAREHEMU KOMBA KARIMJEE

Image
Rais Kikwete (katikati) akiwa na makamu wake Gharib Bilal (kushoto) na Anna Makinda katika viwanja vya Karimjee ili kumuaga marehemu Kapteni John Komba. Rais Mstaafu Benjamin Mkapa (wa pili kulia) akiwa na mkewe Anna (wa tatu kulia) wakiwasili viwanja vya Karimjee. Waziri mkuu aliyejiuzulu,Edward Lowassa (kulia)akisalimiana na Mkapa. Spika wa Bunge, Anna Mkapa (kushoto) akiwa na Mkapa. Mbunge wa Kinondoni Idd Azzan (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba (kulia) akiwa viwanja vya Karimjee. Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (kulia)akisalimiana na mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale. Wake wa marehemu Komba, katikati ni mke mkubwa, Salome, na kulia ni mke mdogo. Miongoni mwa wanafamilia wa marehemu Komba. Mwili wa marehemu John Komba ukiingia Karimjee ili kuagwa na wananchi na viongozi mbalimbali leo jijini Dar

MWILI WA KOMBA UKIWASILI KARIMJEE LEO

Image
Mwili wa marehemu John Komba ukiingia Karimjee ili kuagwa na wananchi na viongozi mbalimbali. Hali ilivyokuwa kwa ujumla viwanja vya Karimjee. (PICHA: GLOBAL WHATSAPP 0753715779/GPL , OJ)

MSIBA WA KOMBA : WEMA ATOBOA YEYE NI MWANA CCM

Image
Watu mbali mbali wakiwemo  waigizaji wa filamu hapa nchni wanaendelea kuonyesha  jinsi  walivyoguswa na kifo cha Mh. Captain John Komba kupita kurasa zao za mitandaoni usasani mtandao wa Instagram, wamekuwa kuweka picha  yake na kuandika maneno ya kumtakia kheri huko aendako.Mwigizaji  Wema Sepetu nae ni mojawapo alieguswa na msiba huu na kuandika mameno kuonyesha majonzi alionayo  na kutoa kuwa  yeye ni mwanachama wa chama cha mapinduzi  (CCM)kama alivyokuwa marehemu.“Dah ni pigo kubwa sana.... RIP Mwana CCM mwenzangu..... RIP Baba angu... RIP Captain.... Mbele yako nyuma yetu... Taifa this tym linahuzunika kwako aisee... Kwaheri Baba...”-Wema aliandika. Baadhi ya waigizaji nao waliandika kwenye kurasa zao mtandaoni kama ifuatayo; “Pumzika kwa amani kaka yangudaima tutakukumbuka”-JB “R. I. P. Mh komba kifo nimlango wote tutapita ktk mlango huo na hakuna wakukwepa mlango pole kwa familia tulimpenda ila mungu kampenda za...

AKUTWA AMEKUFA, MAITI YAKE YALIWA NA PAKA!

Image
Mwili wa Mbulu ukitolewa ndani ya jumba bovu.  Mwisho wa enzi! Jamaa mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Mbulu amekutwa kwenye jumba bovu akiwa amekufa kisha mwili wake kutoa harufu kali huku ukiliwa na paka. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, maiti ya jamaa huyo iligundulika wikiendi iliyopita katika jumba hilo maeneo ya Mtaa wa Simu B Kata ya Mji Mpya mkoani hapa ambapo wananchi wa maeneo hayo walisikia harufu kali kutoka kwenye jumba hilo, walipoingia ndipo wakakuta mwili wa jamaa huyo huku pua na sehemu za uso zikiwa zimetafunwa na paka. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mwenyekiti wa mtaa huo, Maneno Kifea ’Ticha’ alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.Licha ya harufu kali mwanahabari wetu alijitosa na kuingia kwenye jumba hilo ambapo alishuhudia mwili wa jamaa huyo ukiwa umeharibika.  ...Mwili ukipakizwa kwenye gari. Hata hivyo, serikali ya mtaa huo ilitoa taarifa polisi ambao walifika na kuuchukua kisha kwenda kuuhifadhi kwenye H...