MTALII ALIYEKWAMA KILELE CHA MAWENZI MLIMA KILIMANJARO AOKOLEWA.
Mtalii Jeanne Traska kutoka Ujerumani Bi.Jeanne Traska kutoka Ujerumani na Muongoza Wageni Athumani Juma wakiwa katika Lango la Marangu pamoja na vifaa mbalimbali walivyokwama navyo katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro mara baada ya kuokolewa. Kikosi cha Uokoaji katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro kimefanikiwa kumuokoa mtalii Bi. Jeanne Traska (32) kutoka Ujerumani pamoja na muongoza wageni Athuman Juma ambao jana walikwama katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro. Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kufika eneo la kilele cha Mawenzi na kwa kutumia mbinu za uokoaji za kisasa kabisa kiliweza kuwanasua majira ya kumi na moja jioni. Licha ya hali mbaya ya hewa iliyotokana na mawingu mazito katika eneo hilo, Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kukabiliana na hali hiyo na kuweza kuwanasua na kisha kuwapeleka katika kituo cha Horombo majira ya saa mbili usiku ambapo walichukuliwa na gari kupitia nj...