Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Jerry Muro akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Meru na Arusha. MKUU wa Wilaya ya Arumeru, Mheshimiwa Jerry Muro jana tarehe 01 Agosti, 2018 alifanya ziara ya kikazi pamoja utambulisho kwa watumishi wa Halmashauri Mbili za Meru yenye kata 26 na Arusha yenye kata 27 zilizo katika Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha. Akiwa katika halmashauri hizo, Mhe. Muro aliwataka watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia mahitaji ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo ndio anasimamia Utekelezaji wake katika halmashauri zote mbili zenye kata 53. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Jerry Muro akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Meru na Arusha. Katika Ziara Hiyo, Mhe Muro aliambatana na Mkuu wa wilaya ya Monduli, Mhe Iddi Hassan Kimanta aliyekuwa akikaimu Wilaya ya Arumeru, pamoja na Katibu Tawala, Bwana Timotheo Mzava pamoja na baadhi ya viongozi wa kamati ya ulinzi na...