Posts

Showing posts from August 5, 2017

Rais Magufuli Amaliza Bifu la Makonda na Ruge Jukwaani

Image
Paul Makonda akishikana mkono na Ruge Mutahaba. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli , amemaliza bifu kubwa lililokuwepo kati ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kuwakutanisha wawili hao jukwaani na kuwataka washikane mikono. Tukio hilo la aina yake, limetokea kwenye Kijiji cha Chongoleani, Tanga ambapo kulikuwa na tukio kubwa la uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda mpaka kwenye Bandari ya Tanga.

SOL CAMPBELL WA ARSENAL ANATUA DAR LEO

Image
Beki wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell. BEKI wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell anatarajiwa kutua nchini leo Jumamosi mchana kwa mwaliko wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportPesa.Campbell ambaye pia amewahi kuichezea Tottenham Hotspur ya England, akiwa nchini kesho atajumuika na baadhi ya wadau wa soka kutazama mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Arsenal na Chelsea.Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Abbas Tarimba, akiwa nchini Campbellpia atafanya mafunzo kwa timu ya Magnet kwenye Uwanja wa Gymkhana na kutembelea timu ya Muungano. “Huyu ni nyota wa pili wa zamani wa soka baada ya Leon Osman wa Everton, tunajua bado watu wanakumbuka ujio wa Everton huu ni muendelezo wa kampuni yetu kuleta hamasa ya soka nchini,” alisema Tarimba.Tarimba alisema SportPesa inaendelea kuwapa hamasa ya soka Watanzania kwa ujio wa nyota huyo ukiachana na udhamini iliyoutoa kwa Simba, Yanga na Singida United.

Povu la Ndikumana kwa Uwoya Lachafua Hali ya Hewa

Image
Ndikumana na Uwoya. Mwanasoka wa Kimataifa kutoka Rwanda, Hamad Ndikumana ambaye ni mume wa ndoa wa staa wa filamu za Bongo, Irene Uwoya , amekubali kumpa talaka Irene ili andelee na maisha yake baada ya kutengana muda mrefu huku akieleza kuchoshwa na skendo chafu za mke wake huyo. Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Ndikumana ameandika ujumbe akisema amekubali kumpa Irene talaka, hivyo asisubiri hadi afe ili aolewe, ili ampe uhuru anaouhitaji aweze kufanya mambo yake bila yeye kuhusishwa. “Ulilia muda kwamba unataka talaka ili uolewe, sina kipingamizi tafuta kila utakacho ulete nitakusainia, usisubiri nife ili uolewe maana naweza kuishi zaidi ya unavyofikiria, Mungu akusimamie”, aliandika Ndikumana. Wanandoa hao wakitambo wakiwa pamoja. (Picha na Maktaba) Pia Ndikumana amesema kitendo cha Irene kumnyima kuzungumza na mwanae tangu watengane, ni kitendo kinachomuumiza sana, lakini yote anamuachia Mungu. “Ungekuwa na roho ya kibinadamu u

Gwajima Anunua Ndege aina ya JET, Pia kuleta Umeme megawati 250

Image
Baaada ya kimya cha muda mrefu Askofu Mkuu wa kanisa la ufufuo na uzima, Mchungaji Josephat Gwajima ameibuka na kutangaza kuleta ndege aina ya 'Jet' Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma kwa watumishi wake. Mchungaji Gwajima ambaye hivi sasa yupo mjini Birmingham, Alabama nchini Marekani kwa shughuli zake za injili na mikutano mbalimbali ameahidi ataleta ndege aina ya 'Jet' "Muda si mrefu nitaleta Tanzania ndege hii 'Jet' kwa lengo la kukuza falme ya Mungu" alisema Gwajima Mbali na hilo Mchungaji Gwajima akiwa katika ziara zake hizo za kiroho alidai kuwa amepata umeme megawati 250 kutoka nchini Ujerumani ambazo anaamini zitasaidia taifa letu la Tanzania katika kukuza sekta ya viwanda. "Nimepata Umeme Megawati 250 kutoka Ujerumani kwa ajili ya Taifa letu katika juhudi za kuunga mkono Tanzania ya Viwanda. Nilimtuma Engineer Mkuu wa Ufufuo na Uzima Duniani Eng.Yeconia Bihagaze huko Ujerumani kufanya ufuatiliaji, Umeme huu ni k

Hii Ndiyo Sababu ya Lowassa Kumpigia Debe Kenyatta

Image
Rais Kenyatta na Edward Lowassa. Zikiwa zimebaki siku mbili nchi ya Kenya kufanya Uchaguzi Mkuu, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amefunguka sababu kuu zinazofanya amtetee na kumnadi mgombea Urais kupitia chama cha Jubilee Uhuru Kenyatta kuwa ni kiongozi shupavu. Lowassa ambaye jana alishiriki katika mkutano wa chama cha Jubilee alisema kuwa kuna watu wanauliza kwanini yeye pamoja na CHADEMA wanamnadi kwa kuwa kiongozi huyo ni shupavu na mpenda watu. “Kuna watu wananiuliza kwanini mnamnadi Uhuru Kenyatta, nasema tena hadharani bila aibu yoyote huyu ni kiongozi shupavu anayependa watu, anaweza kuongoza watu wetu, lakini cha pili Uhuru Kenyatta anapenda Afrika Mashariki akiingia madarakani ataturuhusu tuendelee kuzunguka zunguka kwenye mipaka hii kama Namanga pale bila hata shida, la tatu ni kwamba aliingia madarakani nchi ikiwa kwenye vita lakini amewapa suluhu ameingoza nchi imekwenda taratibu na akafanikiwa” alisema Lowassa. Kenyatta akisim

RWANDA: Rais Paul Aweka Historia Ushindi Urais

Image
Rais Paul Kagame akishangilia ushindi. Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda imemtangaza Paul Kagame kuwa mshindi wa urais wa nchi hiyo katika uchaguzi uliyofanyika jana Ijumaa, Agosti 4. Tume hiyo imesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais huyo ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 17 sasa, atahudumu muhula wa tatu wa miaka saba baada ya kushinda kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa. Wafuasi wake wanamsifu Kagame kwa kuonyesha utulivu na maendeleo ya kiuchumi nchini humo baada ya mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 ambapo maelfu ya watu waliuaawa. Kutoka kushoto Paul Kagame, Frank Habineza na Philippe Mpayimana. Wapinzani wa Kagame walikuwa ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana ambao amewaburuza vibaya kwenye matokeo hayo ambapo wapinzani hao wamelalamika kuwa wafuasi wao wamepigwa zengwe ndiyo maana imesababisha kuwepo watu wachache katika mikutano yao ya kabla ya kura. Hata hivyo chama tawala kimekana madai hayo. Rais Kagame aliingia madarakani mwa

RAIS DKT MAGUFULI AMWANDALIA RAIS MUSEVENI WA UGANDA DHIFA YA KITAIFA JIJINI TANGA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wakati wa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga. Pamoja nao meza kuu ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mama Janeth Magufuli. Hii ikiwa ni bado masaa machache kabla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga. Sehemu ya mawaziri na manaibu waziri wa Tanzania na Uganda wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa za nchi hizo mbili na wa Afrika Mashariki kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dkt. Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku Sehemu ya viongozi mbalimbali wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa za nchi hizo mbili na wa Afrika Mashariki kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dkt. Magufuli kwa heshima ya

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA

Image
Utengenezaji wa sabuni hii una njia nyingi Hatua  ya kwanza Chemsha vipimo 7 vya mafuta ya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya kimiminika chuja na yaweke kwenye chungu cha mfinyanzi au chombo cha plastiki. Hatua ya pili Pima vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa kwenye maji acha hadi mchanganyiko huo uyeyuke. Subiri mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta ukaribie kupoa. Hatua ya tatu Taratibu ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga haraka haraka bila kusitisha ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi. Njia ya pili Chemsha mafuta kwenye joto la kadiri ya 55C Changanya maji na sodium hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo. Baada ya kuandaa mchanyiko wako changanya vimiminika hivyo viwili huku ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo, taratibu sabuni itageuka kuwa laini. Kabla sabuni haijawa ngumu mwaga sabuni ndani ya