Ujumbe wa Ray C kwa wavuta bangi wote...
Ray C ambaye aliathirika na matumizi ya dawa za kulevya na baadae kupona ameendelea kuwa kioo cha jamii kwa ku-share experience yake baada ya kupona kwenye ishu ya dawa za kulevya. Msanii huyo ametoa ujumbe mpya ambao ni muhimu kila mtu kuujua kwasababu kwenye mazingira yetu kuna waathirika wengi wa dawa za kulevya. Haya ndiyo maneno ya Ray C mwenyewe ambayo yana ujumbe mzuri ndani yake: “Wote hawa tuliokaa hapa(picha hapo chini) tuliathirika na dawa za kulevya na tumepona kwa kunywa dawa moja tu inayoitwa Methadone. Inapatikana Muhimbili na Mwananyamala pekee na ni bure kabisa. "Tunamshukuru sana Mh Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutuletea dawa hii.Ningependa kuwashauri walioathirika wa dawa za kulevya iwe wewe,ndugu yako,rafiki,kaka,dada,mjomba,jirani au yoyote aliye karibu na wewe. "Usiogope amua tu kwamba unataka kupona na nenda kanywe hii dawa utapona kabisa.”