Posts

Showing posts from July 12, 2016

Kituo cha Foreplan Clinic cha Tabib Mwaka Chafutiwa Usajili

Image
Serikali imekifungia kituo cha tiba asilia cha Foreplan kinachomilikiwa na Juma Mwaka kwa kukiuka masharti ya kibali alichopewa kujitangaza kuwa anatoa tiba za kisasa badala ya matibabu ya asilia. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti Wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo amesema kuwa kituo hiko kimefutiwa usajili na hakiruhusu kutoa huduma za tiba asilia na tiba mbadala kwa jamii kwa kutokidhi masharti ya usajili na kufanya kazi kinyume cha usajili wake. “Kuanzia hivi sasa tumekifutia usajili kituo cha tiba asili na tiba mbadala cha Foreplan kwa kukiuka masharti ya usajili na hivyo hakiruhusiwi kutoa huduma kwa jamii  na watanzania kwa ujumla,”amesisitiza Dk Kayombo. Ameongeza kuwa vituo vingine vilivyofungiwa kutoa huduma ni pamoja na Tabibu Abdallah Mandai wa Mandai Herval Clinic na Kituo cha Fadhaget Sanitarium Clinic kinachomilikiwa na Tabibu Fadhil Kabujanja.

KONDA WA DALADALA ACHINJWA KAMA KUKU,UNYAMA WA KUTISHA

Image
Amonike Isdori ‘Dulla’ enzi za uhai wake. Na Waandishi Wetu,   UWAZI DAR ES SALAAM: Zama za mwisho! Kijana aliyefahamika kwa jina la Amonike Isdori ‘Dulla’ (22) mkazi wa Makondeko- Golani, Kimara jijini Dar ambaye ni kondakta wa daladala, hivi karibuni alichinjwa kama kuku na watu wanaodaiwa kuwa ni walinzi shirikishi (sungusungu). Bibi wa marehemu akilia kwa uchungu. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea usiku wa siku ya Idd Mosi, majira ya saa 7 usiku ambapo marehemu inadaiwa alikuwa akirejea nyumbani kutoka kwenye sherehe za sikukuu, ndipo alipokutana na watu hao walioanza kumpiga kwa madai alikuwa mwizi. Akizungumza kwa majonzi na waandishi wetu, mama mdogo wa Amonike, Janeth alisema; “Siku ya tukio niligongewa mlango usiku na kundi la watu kama 15, ambao sikuwafahamu wakadai wao ni sungusungu na wamemkamata mwanangu kuwa ni mwizi. “Walikuwa wamemfunga Amonike kamba miguu na mikono huku utosini akiwa na jeraha kubwa na ametapakaa damu. Niliwaambia mwan...