BREAKING: Wananchi wavamia tena mgodi wa Acacia
Kundi kubwa la wananchi kutoka vijiji vitano vinavyozunguka mgodi wa Acacia North Mara wamevamia mgodi huo. Taarifa kutoka eneo la tukio hivi sasa zinaeleza kuwa wananchi hao wanaendelea kukusanyika katika lango kuu la mgodi huo maarufu Boom Gate huku jeshi la polisi likijaribu kuwatawanya. Hilo ni jaribio la pili kwa wananchi hao kutaka kuingia mgodini humo baada ya lile ya jana ambapo polisi walifanikiwa kulizima. Taarifa zaidi kukujia.