Posts

Showing posts from February 22, 2015

Kiungo wa timu ya Simba SC Christopher Alex Masawe Afariki Dunia

Image
Aliyekuwa kiungo wa timu ya Simba SC Christopher Alex Masawe amefariki dunia leo saa 3 Asubuhi katika hospitali ya Milembe mkoani Dodoma baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa mama yake mzazi aliyekuwa akimuuguza, maziko yatafanyika keshokutwa siku ya Jumanne. Christopher Alex atakumbukwa kwa kufunga penati ya mwisho katika mchezo wa Simba dhidi ya Zamalek na kuifanya Simba ifuzu hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika mwaka 2003 mchezo uliopigwa nchini Misri. Baadhi ya wachezaji waliounda kikosi hicho kilichoitoa Zamalek ni pamoja na Boniface Pawasa, Juma Kaseja na Suleiman Matola. Rais wa Simba Evans Aveva ambaye yuko mjini Shinyanga katika pambano la ligi kuu dhidi ya Stand United ametuma salam za rambirambi kwa familia ya marehemu na kumuelezea marehemu kuwa aliitumikia Simba kwa juhudi, mapenzi na uaminifu mkubwa na kusema kwamba Simba itaungana na familia yake katika msiba huo.

Mrembo Huddah Monroe Asema Kazi yake ya Kuwapa Raha Wanaume Inalipa..Aonyesha Kadi ya Range Rover Analomiliki

Image
Mrembo Huddah Monroe Mrembo wa Kenya Huddah Monroe Amejitokeza na kuwaponda wale waandishi wa Habari Bloggers wanaosema gari aina la Range Rover analoendesha kwa sasa ameazima kwa mtu na kusema kuwa kazi anayofanya (Socialite ) ya Kutoa Escort kwa kuwapa raha wanaume na kuhuzuria events mbali mbali inamlipa sana kiasi hawezi azima gari ...Huddah Ameweka Mtandaoni kadi ya gari hiyo ambalo ni la gharama sana kwa mtu wa kawaida ikionyesha jina lake halisi kama mmiliki halali wa Ndinga hiyo matata Kadi ya Gari aina ya Ronger Rover ikionyesha jina halisi la Huddah

MKUU WA KITUO CHA POLISI JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA MAHABUSU HUKO NJOMBE.

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa ya Njombe, imemhukumu aliyekuwa mkuu wa kituo cha Polisi Ilembula kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtuhumiwa aliyekuwa ndani ya mahabusu. Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Augustine Rwezile, baada ya mshtakiwa huyo James Nyambenga kukiri kosa hilo mahakamani, ambapo mshakiwa huyo anadaiwa kumtoa msichana huyo kwenye chumba cha mahabusu alikokuwa anashikiliwa na kumbaka. Mwanamke huyo ambae ni mhudumu wa bar alikuwa anashikiliwa kwenye mahabusu ya kituo hicho kwa tuhuma za uzururaji. Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rwezile amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji na vielelezo vya daktari aliyempima msichana huyo viliweza kuithibitishia Mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

BINTI WA MIAKA 27 AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA.. WIVU WA KIMAPENZI WAHUSISHWA -SHINYANGA VIJIJINI

Image
Mwili wa Marehemu Huma ukiwa unachukuliwa na Maafisa wa Polisi Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Huma Simon (27) mkazi wa kitongoji cha Solwa Kata ya Solwa Wilayani Shinyanga Vijijini ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia juzi. Kwa mujibu wa Majirani Mwili wa marehemu Huma umekutwa asubuhi katika eneo la Shule ya msingi Solwa ukiwa umekatwa mapanga sehemu mbalimbali na kutelekezwa. Taarifa zimesema Huma ambaye anaishi na Mama yake Mzazi, alitoka usiku katika chumba alichokua amelala na kumuacha Mtoto wake wa kike anayekadiriwa kuwa na miaka miwili, na kukutwa asubuhi akiwa ameuawa. Wananchi wa Kata Solwa wakiutazama Mwili wa Marehemu eneo la Tukio Mwili wa Marehemu Huma Simon ukiwa eneo la tukio

BAADA YA KUSINGIZIWA KUWA AMECHAGULIWA KUWA MKUU WA WILAYA IMEFICHUKA KUWA HII NDIO KAZI YAKE

Image

Kiongozi Wa Vijana wa JKT Waliopanga Kuandamana Atekwa na Kuokotwa Akiwa Mahututi..... Walitaka awaambie aliyemtuma kati ya Lowassa na Ukawa

Image
KIONGOZI wa vijana waliopata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), waliokuwa wakiishinikiza Serikali kuwapatia ajira, George Mgoba, amelazwa katika Hospitali ya Amana, jijini Dar es Salaam, baada ya kutekwa nyara na kisha kuteswa na watu wasiojulikana.   Mgoba ni miongoni mwa vijana waliowawakilisha wenzao zaidi ya 300 kukutana na viongozi wa juu wa Serikali hivi karibuni, akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, kuzungumzia kilio chao na kupinga upendeleo wa ajira ndani ya Jeshi.    Tukio hilo ambalo kwa kiasi kikubwa linafanana na kile alichofanyiwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka au Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, lilimfika Mgoba Jumatatu wiki hii saa 11:00 jioni.   Mgoba, ambaye analindwa na vijana wenzake waliomaliza mafunzo ya JKT katika wodi namba saba aliyolazwa, anadai kufanyiwa vitendo vya kinyama ikiwa pamoja na kuchomwa sindano ambayo haijul...

LE PROJECT WEMA AMPIKIA OMMY DIMPOZ NA KUMPAKULIA

Image
Wakati mwanamziki wa Bongo Fleva,Ommy Dimpoz akiendelea kupepesa macho na kutikisa masikio kukanusha kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na mwingizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ukaribu wao bado unatia mashaka na kuendeleza sintofahamu miongoni mwa mashabiki na wapambe wao. Japo kuwa Ommy alielezakuwa yeye na Wema ni marafiki toka kitambo kabla hata ya wema kuwa na mahusiano na mwanamziki Diamond, lakini hii imezidiii. Mbali na kuonekana wawili hawa kuwa pamoja sehemu mablimbali za starehe toka Ommy atoke Marekani, hili la kupikiwa na kupakuliwa nyumbani kwa  Wema ndio limezidi kuchochea hisia kuwa wawili hao wanamahusiano zaidi ya USHKAJI. Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram mwanadada Wema ambae na folloers zaidi ya laki nne , alibandika picha hiyo hapo juu akionekana kumpakulia chakula ambacho alijisifia ni kizuri na amekipika mwenyewe na kumtania Ommy kuwa alikuwa analeta pozi kwenye kula. “Dat moment anapokuja home and umepika chakula ...

Jack: Sitaki Tena Ndoa!

Image
Mrembo na mwigizaji wa filamu, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’ ameamua kufunguka na kuweka wazi kuwa hayuko tayari kuolewa tena hii ni baada ya kupewa talaka na aliyekuwa mumewe, Gadna Dibibi. Jack alisema, kwa muda aliodumu kwenye ndoa ameshaona raha na karaha yake hivyo suala la kuolewa tena sasa hivi halipo akilini mwake “Katika ndoa lazima kuwe na mabaya na mazuri, hata hivyo siwezi kusema ndoa ni chungu hapana, ila mimi kwa sasa hivi nimeona nipumzike kwanza sitaki tena ndoa labda kwa hapo baadaye nitakapojipanga tena upya,” alisema Jack. Jack alidumu na mumewe huyo kwa miaka miwili na nusu kabla ya kupewa talaka hivi karibuni huku chanzo kikiwa ni kusalitiana katika mapenzi. GPL

Female Student Caught with Popular Politician in Hotel Room

Image
The rate at which young girls are running after married men all because of money these days is really sad. Funny enough, this same ladies will be crying one-man/one-wife when they manage to see a man who wants to marry them. So, you can do another woman's husband, but you want yours to yourself? Lol! Unfortunately for this female student, her mother has been on her track and monitoring her illicit affairs with men. So, on this day, after she left home to "service" Hon. Beno, her mother and some boys trailed her and as soon as she went on bed with the man they busted the door to the hotel room... The mother said she has been reading her daughter's sms until she saw her disappearing in a local guest house with a politician, Mr Beno. The girl's mum say they are not poor. So, what is her problem? In the words of the mother: "I began to be concerned with the conduct of my daughter after noticing some suspicion looks. She doesnt ...

Kim Kardashian Ajianika Mtupu Kama Alivyozaliwa

Image
Msaanii  wa  Kike  Kim Kardashian    ambaye  ni  mke  wa  mwanamuziki  Kanye  West   na  mama  wa  mtoto  mmoja  hivi  karibuni  alikubali  kupigwa  picha  za  utupu  kama  alivyozaliwa  kwa  ajili  ya  kurasa  za  mbele  za  gazeti  la  Love  Magazine. .... Kuona Picha  zote  na  maelezo  ya  kina......Bofya  hiyo  picha  ya  chini  ambayo  Nimeififisha  kulinda  maadili  yetu. Au  Ingia  <<  HAPA  >>

Sakata la Magari 11 Yaliyotekwa na Majambazi Juzi: Vifaa vya abiria vyazagaa Mtaani

Image
BAADHI ya vifaa vya abiria vilivyoporwa katika tukio la utekaji wa magari 11 uliofanywa na majambazi waliokuwa na silaha za jadi mkoani Manyara mwanzoni mwa wiki hii, vimekutwa vikizagaa katika maeneo yalikofanyika uporaji huo.   Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoani Manyara, Christopher Fuime alisema vitu vilivyopatikana ni pamoja na laini za simu 14 na simu zinazouzwa kwa bei ndogo na kwamba jeshi hilo linaendelea kuwasaka majambazi hao ili kuwachukulia hatua.   Kamanda Fuime alisema katika tukio hilo majambazi zaidi ya wanane wakiwa na silaha za jadi waliteka magari 11 katika kijiji cha Gehandu kilichopo katika barabara kuu ya Babati–Singida na kupora vitu mbalimbali kwa watu waliokuwa ndani ya magari hayo zikiwemo fedha taslimu na simu za mkononi.   Alifafanua kuwa katika tukio hilo kiwango cha juu cha fedha zilizoporwa ni Sh 600,000 na kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa kwa kuwa majambazi hao walipoona idadi ya magari yanazid...