Posts

Showing posts from May 30, 2016

Shilole, Vanessa Wamaliza Bifu Lao

Image
      Shilole (kulia)  akipashana jukwaani na Vanessa kabla ya shoo hiyo kuanza. Vanessa na Shilole wakijaribu kuelezea juu ya bifu lao. Mtangazaji wa kituo cha Clouds FM, Hamisi Mandi ‘B12’, akiwakaribisha Shilole na Vanessa Mdee tayari kwa kufanya shoo hiyo. Shilole akifanya makamuzi. Vanessa akikamua jukwaani. Baadhi ya mashabiki wakifuatilia shoo hiyo. WAREMBO wanaofanya vyema kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Vanessa Mdee, usiku wa kuamkia leo wameweza kuvunja bifu lao ambalo limekuwa likivuma kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukamua kwenye steji moja ndani ya ukumbi wa Bilicanas. Habari/Picha: Musa Mateja/GPL

BREAKING NEWZ:Vurugu Tena Bungeni, Ni Kuhusu Wanafunzi 7000 wa UDOM Waliotimuliwa.

Image
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kujali itikadi ya vyama vyao, leo wametoka nje ya ukumbi wa bunge hilo baada ya Naibu Spika, Tulia Ackson kukataa kujadiliwa kwa kauli ya serikali kuhusu wanafunzi 7000 wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) waliosimamishwa. Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kutekeleza agizo la Maziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako hivi karibuni kiliwasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi 7,000 wa kozi maalumu ya ualimu wa sayansi kwa ngazi ya stashahada na kuwataka waondoke chuoni hapo mara moja. Wabunge waliwasilisha hoja kwa Naibu Spika, Tulia Ackson ili kulishinikiza bunge kuijadili kauli ya serikali kuhusu wanafunzi hao waliotimuliwa ambapo Naibu Spika alikataa kusikilizwa hoja hayo ndipo vurugu zikaanza na kumlazimu Naibu Spika kufunga Kikao cha Bunge kilichokuwa kikiendelea na kuwaamuru wabunge wote watoke nje. Juzi, lilitolewa tangazo chuoni hapo likiwataka wanafunzi hao kuondoka kuondoka chuoni hapo. Tangazo hilo lilieleza kuwa k

Lungi alinanga penzi la Wolper, Harmonize

Image
Jacqueline Wolper na Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ STORI: HAMIDA HASSAN, WIKIENDA MSANII wa filamu wa kitambo, Lungi Maulanga amelinanga penzi na Jacqueline Wolper na Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ akisema kuwa, anachoona ni kama Wolper anatembea na mdogo wake. Lungi Maulanga Akiuzungumzia uhusiano wa mastaa hao, Lungi alisema alijisikia vibaya sana kuona shosti wake Wolper kafa, kaoza kwa Harmonize kutokana na tofauti kubwa iliyopo kati yao. “Unajua Wolper ni kama mdogo wangu na shosti wangu hivyo siwezi kumuacha apotee, mimi nitamuita tutaongea kwa kina, kama atashikilia msimamo wake nitamuacha kwa sababu si unajua mtu akishapenda, lakini kiukweli hawajaendana,” alisema Lungi.

WANAWAKE WAANDAMANA WAKIDAI KUKOSA WANAUME WA KUWAPA UJAUZITO

Image
Wanawake katika jimbo la Ndeiya nchini Kenya walifahamisha kuwa waume zao wanashindwa kuwapa ujauzito kutokana na mwenendo wa unywaji wa pombe haramu ambazo zinaathiri nguvu za kiume. Katika maandamano ya amani yaliofanyika katika kituo cha biashara cha Thigio, wanawake walioandamana Alhamisi walifahamisha kukerwa na wanaume wanaojihusisha na ulevi kupita kiasi. Nancy Wangare alifahamisha kuwa katika kijiji hicho wanawake wachache walioolewa wamevumilia kwa kiasi kikubwa kutokana na upungufu wa nguvu za kiume kwa waume zao kutokana na pombe wanazokunywa. Mmoja miongoni mwa wanawake walikuwa wakiandamana alifahamisha kuwa iwapo tabia hiyo ya ulevi haitorekebishwa basi itawalazimu kutoka nje ya ndoa zao na bila wao kujua lolote na kuwahudumia watoto wasiokuwa wao

Nyongeza ya Majina Kidato cha 6 Walioteuliwa Kujiunga JKT

Image
NYONGEZA YA MAJINA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA 2016. VIJANA WAFUATAO WAMEONGEZWA KUHUDHURIA MAFUNZO YA JKT KATIKA MAKAMBI MBALIMBALI KAMA INAVYOONEKANA HAPO CHINI. PIA BAADHI YA VIJANA WAMEHAMISHWA MAKAMBI KUTOKANA NA SABABU MBALIMBALI WARIPOTI KWENYE MAKAMBI KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI KABLA YA TAREHE 05 JUNI 2016. S/NO JINA SHULE KIKOSI 1 ABDILLAH RAMADHANI HAJI LILIAN KIBO MGAMBO JKT 2 ABDUL M. MTEKETA BENJAMIN WILLIAM MKAPA MGAMBO JKT 3 ABDULAZIZ SALUM AHMAD PIUS SEC.SCHOOL MARAMBA JKT 4 AGNES PETER MAGANGA FLORIAN SEC RUVU JKT 5 AGNESS EMMANUEL KITANDU ST. MARY GORETI RUVU JKT 6 AGNESS PETER MAGANGA MARAMBA JKT 7 AJUAE DAVIS AMINIELI KANEMBWA JKT 8 ALEX MLOSO BINZA HIGH SCHOOL MARAMBA JKT 9 ALFRED AIDAN MBANO KIGONSELA HIGH SCHOOL RUVU JKT 10 ALLY KAFERA ALLY MBEZI BEACH SEC. KANEMBWA JKT 11 ALVIN ISMAEL MAKUNDI ST JOSEPH CATHEDRAL HIGH SCHOOL RUVU JKT 12 AMBWENE FRANK MWAKANEMA UWEMBA SEC MARAMBA JKT 13 AMOS ASEGE NSUMBA RUVU JKT 14 AMOS KINGU OLD M